Vidokezo vya Kuandika Barua Nzuri ya kuomba ajira

Vidokezo vya Kuandika Barua Nzuri ya kuomba ajira

Barua ya kuomba ajira ni nini?

Hii ni barua inayolenga kukuwezesha wewe kujitambulisha kwa mwajiri mpya/mtarajiwa juu ya sifa ulizonazo dhidi ya nafasi ya/za ajira zilizotangazwa au unayoiomba toka kwake kama haijatangazwa. Hivyo ni vizuri ukaiandika kwa umahiri mkubwa ukiweka mkazo zaidi juu ya sifa zako za kitaaluma, kiustadi, uzoefu wa kutenda kazi, na mengine mengi ukizingatia zaidi sifa walizoziainisha katika tangazo la kazi, endapo ilitangazwa. Mara zote mwajiri bora huangalia sifa hizi kwanza awali ya yote. Kumbuka utaajiriwa kwa sababu mwajiri anafikiri utaweza kufanya kazi na si kwa sababu nyingine yeyote.

Kwanini uandike barua ya maombi ya ajira wakati tayari umeshaandika wasifu wako?

Barua ni fursa yko wewe kumshawishi mwajiri mtarajiwa kuwa unazo sifa stahiki. Yawezekana hazipowazi sana kwenye wasifu wako, lakini kwa kupitia barua yako, utaweza kumpa mwajiri au msomaji wa barua yako hamu ya kuona wasifu wako na maranyinge hamu ya kukuona na kuhojiana na wewe zaidi. Hivyo hupelekea kukuongezea nafasi ya wewe kuitwa kwenye usaili. Vilevile barua huonyesha kuwa umejidhatiti na unajiamini na sifa ulizonazo. Hivyo inashauriwa kuandika wasifu na kuuambatanisha na barua ya maombi ya ajira marazote unapo omba ajira mpya.

Lini na wapi utapeleka barua yako ya maombi ya kazi/ajira?

Mara zote unapoomba kazi, ni vizuri ukaandika barua ya maombi. Kumbuka ni fursa yako kujieleza japo kwa kifupi kabya ya kuonana na mwajiri uso kwa uso. Hivyo hakikisha inaelezea zaidi sifa ulizonazo juu ya kazi unayoiomba. Ili kuiandika vizuri, soma sifa za mwombaji wa kazi kama ambavyo zimeainishwa kwenye tangazo la kazi na kisha zijibu kwa kuonyesha unazo au jinsi gani umezifikia kupitia barua yako ya maombi.

Vilevile unaweza kuandika barua ya kuomba kazi isiyo rasmi na kuituma kwa wakala wa kuajiri (recruitment agency) ambako kwa kawaida huwi na ufahamu wa sifa za kazi za mwombaji ambazo mwajiri anazitaka. Kwani hujui ni mwajiri yupi atapewa barua yako toka kwa wakala. Kimisingi wakala atakacho kifanya ni kupitia wasifu zote alizonazo na pia kuangalia sifa anazotaka mteja wake (mwajiri) kisha atawaita wale ambao wametimiza au wanakaribia sifa hizo. Sasa basi ili kukupa fursa wewe kuitwa, hakikisha barua yako na wasifu wako unaelezea zaidi kazi kadhaa ambazo unafikiri kwa ujuzi au taaluma uliyonayo unaweza kuzifanya.

Zingatia kufuata taratibu zote za uandishi wa barua za kikazi unapo andikika barua yako ya maombi.

Kutuma maombi kwa kazi ambazo hazijatangazwa

Hii ni tofauti na kutafuta kazi kupitia wakala wa ajira, hapa unatuma barua na wasifu wako kwa mwajiri ambaye umemuainisha tayari. Hivyo zingatia yafuatayo:
Kwanza chukua muda wako kutafuta taairifa muhimu zitakazo kuwezesha kuifahamu vizuri kampuni husika. Hii ni pamoja na kazi wanazozifanya na sifa au taaluma za wafanyakazi walipo humo. Kisha tumia taarifa hizo kujitathmini wewe binafsi ili kujua ni kwa jinsi gani unafaa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Pili, hakikisha unaandika barua yako na wasifu wako kwa umahiri ukielezea kwa kiasi kikubwa sifa au weredi/taaluma uliyonayo inayo endana na mahitaji ya kampuni. Kwa kuandika hivyo, utaweza kumshawishi mwajiri kuandaa mahojiano maalumu na wewe na kisha au kukuajiri au kukuweka kwenye orodha ya wafanyakazi watarajiwa ambao atawajiri pindi fursa stahiki itakapo patikana.

Ipi ni njia nzuri ya kutuma barua ya maomni ya kazi?

Waweza kutumia njia yeyote ambayo umeizoea na unaweza kumudu gharama zake. Lakini kwa maendeleo ya kisayansi, siku hizi wengi hutumia nija ya barua pepe ambayo ni ya haraka na nafuu sana kuliko nyinginezo. Zingatia kufuata taratibu zote za uandishi wa barua ikiwa pamoja na kuwa na mwandiko unaosomeka vizuri. Kama unatumia email, unaweza kuandika barua bila ya sahihi yako, jina litatosha. Zingatia yote tuliyo yaainisha hapo juu kuhusu kuandika barua au wasifu bomba kwwajiri ya kazi yako unayo itafuta.Pia hakikisha mastarti ya kutuma barua, kama yaliainishwa kwenye tangazo unayazingatia yote. Endapo utaiwa kwenye usaili au mawasikiano zaidi na mwajiri, hakikisha unapitia vidokezo vya maandalizi ya usaili kama ambavyo yameelezwa katika tovuti hii.

Loading...