Mikataba na Kuachishwa kazi

This page was last updated on: 2025-11-15

Hati ya Maandishi ya Ajira

Sheria ya kazi ya Tanzania inahitaji kwamba wafanyakazi wapewe mkataba ulioandikwa wa ajira wanapoanza ajira isipokuwa kwa wale ambao wanafanya kazi chini ya siku 6 kwa mwezi kwa mwajiri fulani. Huenda mkataba wa ajira ukuwa wa kipindi chenye kikomo au kisichokuwa na kikomo au kazi maalum. Lazima mkataba wa ajira uwe umeandikwa ukiwa unampa mfanyakazi huyo kufanya kazi nje ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania.

Mkataba wa ajira lazima ueleze maelezo yafuatayo. Jina, umri, anwani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali pa kuajiriwa; ufafanuzi wa kazi; tarehe ya kuanza; aina na muda wa mkataba; mahali pa kazi; saa za kufanya kazi; ujira, mbinu ya hesabu yake, na maelezo ya faida aiu malipo ya aina yoyote, na suala lingine lililofafanuliwa. Hata hivyo, ikiwa vipengele hivi vimetolewa tayari katika mkataba wa ajira, huenda mwajiri asijaze hali iliyoandikwa ya vipengele vya ajira.

Lazima mwajiri ahakikishe kwamba vipengele vyote vilivyoandikwa vimefafanuliwa wazi kwa mfanyakazi kwa njia inayoeleweka na mfanyakazi. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote katika kipengele chochote kilichoandikwa, mwajiri anahitajika kupitia upya vipengele vilivyoandikwa kwa kushauriana na mfanyakazi ili kuangazia mabadiliko hayo. Lazima mwajiri amfahamishe mfanyakazi kuhusu mabadiliko hayo kwa kuandika.

Mwajiri anawajibika kuweka vipengele vilivyoandikwa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya ajira kuisha. Ikiwa mwajiri atashindwa kutoa mkataba ulioandikwa katika kesi zozote za kisheria, mzigo wa kuthibitisha au kukataa masharti fulani ya ajira uko kwa mwajiri. Kila mwajiri lazima aonyeshe taarifa ya haki ya wafanyakazi katika mahali panapoonekana.

Chanzo: Sehemu ya 14-16 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004.

Mkataba wa kazi wa kipindi maalumu

Kwa mujibu wa sheria za kazi za Tanzania, ni marufuku kuajiri mfanyakazi kwa kipindi cha muda maalumu uliotajwa kwa kazi zenye asili ya kudumu. Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina kati ya zifuatazo-(a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa; mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kazi za wataalamu na mameneja, mkataba wa kazi maalumu. Hakuna sehemu yeyote kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004 inayotoa maelezo juu ya kuendeleza mkataba au muda wa juu wa mkataba wa kipindi maalumu.

Chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004, mikataba ya muda maalum iliruhusiwa tu kwa makundi ya kitaalamu na usimamizi au kwa kazi za muda maalum au miradi maalum. Hata hivyo, kulingana na Marekebisho ya 2025, waajiri sasa wanaweza kuajiri wafanyakazi wa mikataba ya muda maalum katika kesi zifuatazo:

  1. Kuongezeka kwa mzigo wa kazi kwa muda: Wakati kiasi cha kazi kinapoongezeka ghafla kwa kipindi kifupi na hakitarajiwi kudumu zaidi ya miezi 12.
  2. Wanafunzi wahitimu: Ili kutoa mafunzo yaliyopangwa au uzoefu wa kazi kwa wahitimu wa hivi karibuni kwa kipindi cha hadi miezi 24.
  3. Wafanyakazi wa msimu: Kufunika kazi inayopatikana tu katika misimu fulani, kama vile vipindi vya mavuno au miezi ya kilele cha utalii.
  4. Kazi maalum ya mradi: Kufanya kazi kwenye mradi maalum, kwa mkataba unaomalizika mradi huo ukikamilika au baada ya kipindi kilichobainishwa wazi.
  5. Wafanyakazi wahamiaji wa kigeni: Kuajiri wafanyakazi wahamiaji wa kigeni ambao mikataba yao imeunganishwa na, na haizidi, kipindi kinachofunikwa na vibali vyao vya kazi.
  6. Mpango wa kazi za umma: Kuajiri wafanyakazi chini ya mpango wa kazi za umma au uundaji ajira wa serikali, kwa muda wote mpango huo utakapokuwa ukiendelea.
  7. Nafasi zinazofadhiliwa kutoka nje: Kuajiri wafanyakazi katika kazi zilizopo kwa sababu tu ya ufadhili kutoka chanzo cha nje (kwa mfano, mradi unaofadhiliwa na mfadhili), na kwa kipindi tu ambacho ufadhili huo unapatikana.
  8. Wastaafu: Kuajiri watu ambao tayari wamefikia umri wa kawaida wa kustaafu lakini wameajiriwa tena kwa msingi wa muda maalum.
  9. Kazi zinazotegemea zabuni: Kuajiri watu katika majukumu yanayotegemea mwajiri kushinda zabuni au mkataba maalum, na ambayo hudumu tu kwa kipindi cha zabuni hiyo.

Kanuni kuu za sheria ua Ajira na uhusiano, 2017 ina ainisha kwamba mkataba wa kipindi maalumu kwaajiri ya wafanyakazi wenye ujuzi na mamenaja hautakuwa wa kipindi kisichofikia miezi 12.

Ikiwa mfanyakazi ataendelea kufanyakazi baada ya kipindi maalum kuisha, haki na majukumu hubaki sawa, bila kuwa kwa makubaliano yoyote yanayopinga, kama yalivyokuwa mwisho wa kipindi. Ikiwa hakuna muda maalum wa ushirikiano, mwezi yeyote anaweza kubainisha ushirkiano wakati wwote baada ya kutoa ilani ya lengo lake kwa wenza wale wengine.

Chini ya Marekebisho ya 2025, ikiwa msuluhishi au Mahakama ya Kazi itabaini kwamba mwajiri amevunja kwa kiasi kikubwa mkataba wa muda maalum (ukiukaji mkubwa wa makubaliano), wanaweza kuamuru mwajiri amlipe mfanyakazi fidia sawa na mshahara ambao angekuwa amepata kwa kipindi kilichobaki cha mkataba.

Chanzo: Sehemu ya 14 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004. Sehemu ya 197 na 200 ya Sheria za Mkataba Kifungu cha 345

Kipindi cha majaribio kazini

Sheria za kazi katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 hazisemi wazi ni kwa muda gani mfanyakazi atakuwa katika majaribio kazini chini ya mwajiri wake. Hata hivyo, sheria hii inatamka japo si wazi sana kwamba Mafanyakazi mwenye chini ya miezi 6 kazini iwapo ataachishwa kazi hawezi kulalamika kuwa ameachishwa kwa hila.

Chanzo: Sehemu ya 35 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Kumalizwa kwa ajira

Kumalizika kwa ajira kunasimamiwa chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004.

Mikataba ya ajira inaweza kuisha kwa njia zifuatazo:

  1. Kumfuta kazi na mwajiri
  2. kujiuzulu kwa hiari na mfanyakazi
  3. makubaliano ya pande zote kati ya mwajiri na mfanyakazi
  4. kuachishwa kazi kwa muhtasari (katika kesi ya uzembe mkubwa wa mfanyakazi)
  5. kupunguzwa kwa wafanyakazi (mahitaji ya kiutendaji)
  6. Uwezo mdogo wa mfanyakazi (utendaji duni au ugonjwa)
  7. kumalizika kwa muda wa mkataba au kukamilika kwa kazi iliyokubaliwa
  8. Kifo cha mfanyakazi
  9. kuachishwa kazi kwa njia isiyo ya moja kwa moja (mwajiri alifanya kazi isivumilike kwa mfanyakazi)

Kuachishwa kazi ni halali inapokuwa imejengwa juu ya sababu ya msingi inayohusiana na mwenendo au uwezo wa mfanyakazi, au kwa hitaji la kiutendaji la mwajiri. Taratibu za haki hufuatwa kwa kuachishwa kazi kwa mfanyakazi mmoja mmoja na kwa pamoja. Kuachishwa kazi hakuruhusiwi kujengwa juu ya ubaguzi au juu ya misingi yoyote iliyokatazwa kisheria.

Ajira inamalizwa bila taarifa ya awali kwa uzembe mkubwa kazini. Hii inahusisha ukiukaji mkubwa wa masharti ya ajira au maadili kazini. Hata hivyo, mwajiri lazima afuate taratibu za haki, ikiwa ni pamoja na uchunguzi na vikao vya kinidhamu, ili kuhakikisha kuwa kufukuzwa kuna msingi.

Sio sababu ya haki kumfuta kazi mfanyakazi ikiwa:

  • Wanashiriki taarifa ambazo kisheria wanaruhusiwa au wanatakiwa kuzifichua.
  • Wanakataa kufanya kitu kisicho halali ambacho mwajiri hana haki ya kuwaomba wafanye.
  • Wanatumia haki yoyote waliyopewa chini ya mkataba wao wa ajira, sheria za ajira, au sheria nyingine yoyote.
  • Ni mwanachama (au alikuwa mwanachama) wa chama cha wafanyakazi.
  • Washiriki katika shughuli halali za chama cha wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na mgomo halali.
  • Sababu ya kumaliza mkataba inahusiana na ujauzito wao au ulemavu wao, au ni ubaguzi chini ya sheria.

Kuachishwa kazi kunachukuliwa kuwa si halali ikiwa hakuna sababu ya msingi au ikiwa taratibu za haki hazijafuatwa. Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi inatoa ulinzi dhidi ya kuachishwa kazi isivyo haki, na wafanyakazi wanaweza kutafuta haki kupitia Tume ya Upatanishi na Usuluhishi (CMA). CMA au mahakama ya kazi inaweza kuamuru kurejeshwa kazini, kuajiriwa tena au fidia (ikiwa kurejeshwa kazini si jambo linalowezekana), au mafao ya kuachishwa kazi.

Chini ya vifungu vya awali, mfanyakazi aliyeshinda kesi ya kufukuzwa kinyume cha sheria alikuwa na haki ya kupata mshahara wa angalau miezi 12 kama fidia, bila kikomo cha juu kilichobainishwa. Chini ya Marekebisho ya 2025, kikomo cha kisheria na mpangilio wa viwango vimeanzishwa kwa ajili ya fidia ya kufukuzwa kinyume cha sheria. Chini ya sheria iliyorekebishwa, fidia kwa kufukuzwa kinyume cha sheria sasa imewekewa kikomo cha mishahara ya miezi 24 na huwekwa kulingana na ukali wa kosa: k.m. kwa ujumla miezi 6–12, hadi miezi 12–24 kwa kesi zinazohusisha taratibu zisizo za haki, sababu isiyo ya haki, ubaguzi au unyanyasaji.

Chanzo: §37-44 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004

Taratibu/mwongozo wa hali za ajira

  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Sheria ya sikukuu za kitaifa, 1966 / Public Holidays Ordinance, 1966
Loading...