Fahamu namna ya kuandika Barua Bomba ya kuomba Kazi

Jifunze namna ya kuandika barua nzuri ya kuomba kazi, mbinu za kuandika barua za kuomba kazi, namna ya kuandaa CV nzuri, yote kupitia mywage.org/Tanzania

Vidokezo vya namna ya kuandaa barua bomba ya kuomba kazi

Je ni ipi barua ya kuomba kazi? Ni tofauti na barua nyingine?
Barua ya kuomba kazi ni tofauti na barua nyingine. Barua ya kuomba kazi ina madhumuni ya kukutambulisha kwa mwajiri mtarajiwa. Hii ni nafasi adhimu ambayo inabidi itumiwe vizuri. Taarifa zote zinazokuhusu wewe ni muhimu zikawepo katika barua hii ili  kuweza kumshawishi mwajiri mtarajiwa. Hakikisha unaweka ujuzi, taaluma na uzoefu ulionao ambao utakufanya wewe kua mtahiniwa unaehitajika kujaza nafasi iliyopo. Hizi ndio taarifa ambazo Waajiri huangalia wanaposoma barua yako.

Ni kwanini unatakiwa kuambatanisha barua pamoja na CV wakati wa kuomba kazi?
Barua hii huwekwa kwa madhumuni ya kujitambulisha kwa mwajiri mtarajiwa kwa kuzingatia nafasi uiombayo. Kwa kawaida taarifa unazoziweka katika barua hii hua ni kama kujitangaza mwenyewe na sifa zako na kwa namna gani sifa na ujuzi ulionao utakusaidia katika kufanaya kazi unayoiomba. Barua hii ikiandikwa vizuri humpelekea mwajiri kupitia CV yako kama hatua nyingine.

Ni wakati gani na ni wapi utume barua yako?
Barua hii huitajika pale ambapo nafasi ya kazi hua imetangazwa. Hata kama tangazo la kazi halijakutaka uandike barua hii, siku zote ni vizuri na huongeza uzito kama itaambatanishwa na CV. Barua hii ni tangazo kuhusu wewe, ni vizuri ukaiandika katika namna ambayo itakuuza vizuri katika soko la ajira.
Vile vile unaweza kutuma barua ya kuomba kazi isiyokua mahsusi kama mawakala wa kuajiri (recruitment agent) hawajatangaza kazi. Katika hali kama hii jitahidi barua yako iwe na taarifa zote muhimu ambazo zitakusaidia kupata kazi. Ni kama unatuma barua katika jopo la Waajiri ambao kila mmojawapo ana vitu vyake anavyovipenda hivyo ni vizuri ukajielezea kiundani zaidi ili kuwapa fursa ya kukuona wewe katika muonekanao tofauti tofauti. Kila barua ni vizuri ikaandikwa kwa kuzingatia mahitajai ya kazi iombwayo.

Kuomba kazi bila kuona tangazo la kazi
Wakati mwingine unaweza kuamua kuandika barua ya kuomba kazi katika kampuni Fulani hata kama hawajatangaza kazi. Kitu cha muhimu ni kuandika barua hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya mwajiri unaemlenga.
Uandishi wa barua hii ni tofauti huanza kwa kufanya tafiti inayojitosheleza katika kampuni unayoilenga. Lengo likiwa ni kufahamu majukumu, itikadi na malengo ya kampuni husika ambayo yatakusaidia wewe kuandika barua yenye mvuto na inayoendana na mahitaji ya kampuni. Vile vile barua yako ni vizuri ikaomba kukutana na mwajiri kwa ajili ya majadiliano zaidi, kama vile kuombwa kuitwa kwenye usahili.
Hakikisha mara zote unaonyesha ujuzi na utaalamu unaohitajika, mwajiri hatokuchagua wewe dhidi yaw engine wengi kwasababu ya kiingereza chako kizuri, uzuri wako lakin atakuchagua kwasababu ya ujuzi ulionao unaohitajika katika kazi. Ni muhimu kuhakikisha kua kila unapokutana na mwajiri mtarajiwa unaonyesha ujuzi na utaalamu ulionao ili kukurahisishia kupata kazi.

Ni ipi njia muafaka ya kutuma barua yako?
Katika hili hakuna unashauriwa utumie njia amabayo ni rahisi na nafuu kwako. Kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia, mfumo wa barua pepe ni njia muafaka na nafuu zaidi kutuma barua hizi. Hakikisha unafuata mahitaji yote muhimu ya kuandika barua maalumu wakati wa kuandika barua ya kuomba kazi. Vile vile hakikisha kua ujuzi na uzoefu wote ulioweka katika barua yako pia upo katika CV yako ambayo utaiambatanisha na barua hiyo. Ukitekeleza haya utakua na nafasi kubwa ya kuitwa kwenye usahili. Ukiitwa kwenye usahili hakikisha unafahamu vidokezo muhimu vya kuzingatia wakati wa usahili.

Soma Zaidi:

Kuandaa CV Bomba

Loading...