Andika CV Bomba

Namna ya kuandika CV bomba/nzuri, kila kitu kuhusu kuandika CV bomba/nzuri, andika CV bomba upate kazi nzuri, yote haya na mengine mengi katika Mywage Tanzania.

CV yenye kujitosheleza ni njia muafaka ya kumfanya bosi wako mtarajiwa kukufahamu wewe. CV nzuri inakupa nafasi ya kung’aa katika kikundi na kupata fursa ya usahili na baadae kazi.


Pitia matangazo ya kazi
Unapopitia matangazo ya kazi katika magazeti, kuta za matangazo au barua pepe hakikisha unapitia matangazo hayo kwa umakini. Fanya maamuzi ya kipi kati ya ujuzi, sifa ama uzoefu utatumia katika kazi yako mpya.

Orodhesha vitu hivi na tumia maneno yenye kuonyesha vitendo kwa mfano : Mimi ni mtu mwenye mpangilio, ufanisi na mchapa kazi, nimeongoza na kusimamia watu na matukio.  Nimesoma na kufikia ubora katika weledi na kumaliza shahada ya kwanza katika…..


Kua sahihi kwa kutoa maelezo mafupi yenye kueleweka
Usizidishe maelezo kwa kutoa maelezo yote kukuhusu wewe, hakuna anayetegemea wala kutaka kuyasikia hayo kwa hiyo usifanye hivyo.


CV inatakiwa kumwelezea mtu lakini si kama kitabu kinachoelezea wasifu wako lakini pia si aya/ibara ama kitabu unachoelezea hadithi ya maisha yako ya weledi! Hakikisha huweki taarifa zako binafsi ambazo hazihusiani na nafasi unayoomba.


Sema ukweli
Kua mkweli. Kwa kufanya hivyo unaonyesha kujiamini na mafanikio yako na hii itakusaidia inapokuja kukaa kwa ajili ya usahili. Huwezi kuzungumza kuhusu uzoefu wako kama mwanasayansi wa nyuklia kama hukufaulu masomo ya sayansi shuleni!


Epuka makosa haya
Vitu vichache vya kuepuka kufanya: Usidanganye, usizidishe chumvi, usiweke ahadi usizoweza kuzitimiza.


Vidokezo katika kujielezea
Orodhesha majumuisho yako.
Elezea CV yako katika lugha chanya
Inasaidia kama utaandika sentensi fupi na zenye kuonyesha uhai na kuepuka kutumia vivumishi vingi.
Anza na mafanikio yako ambayo yanawiana na mahitaji muhimu ya kazi. Usimweleze mwajiri ni kwa vipi atakusaidia bali mueleze ni kwa vipi wewe utamsaidia.
Tia msisitizo katika uzoefu unaohusiana na biashara ama kazi husika. Kama una uhusiano mzuri wa kazi na wataalamu katika fani yako unaweza kuwaomba kuwatumia kama wadhamini.


Pata ushauri kabla hujatuma CV yako. Tafuta mtu unaemjua katika fani husika ili apitie CV yako. Jiandae kurekebisha vitu ulivyoandika.


Jaribisha CV yako kwa kuomba nafasi mbalimbali katika kiwango chako lakini pia kiwango cha juu kidogo. Hii itakusaidia kujua soko la ajira na thamani yako.


Isiwe sawa kila wakati
CV yako inabidi iwe inaendana na kazi unayoomba. Hivyo basi wakati unaomba kazi tofauti kwa kutumia CV ile ile ni vizuri ukajaribu kuiweka CV ikaendana na nafasi unayoomba.


Usikate tamaa
Tumia CV yako kuitwa kwenye usahili. Huko utapata fursa ya kuelezea mafanikio yako.
Kitu cha muhimu, USIKATE TAMAA! Kwa kila CV 100 unazotuma unaweza kuitwa kwenye usahili mara 10, na katika mara kumi hizi utapata kazi moja tu- kazi yako ipo inakusubiria. Kua makini na mwenye malengo na muda si mrefu utakua mmoja ya watu katika dunia ya kazi.

Loading...