Hifadhi ya Jamii

This page was last updated on: 2023-05-21

Haki ya Pensheni

Sheria ya Hifadhi ya jamii, 1997 inaelezea juu ya pensheni kamili na isiyo kamili. Kwa pensheni kamili, mfanyakazi anapaswa awe amefikia umri wa miaka 60 na walau miezi 180 (miaka 15) ya kuchangia. Pensheni ya awali pia inaweza kutolewa kwa mfanyakazi aliyefikia umri wa miaka 55. Ni programu isiyo timilifu ya bima kamilin na hilipwa kati ya umri wa miaka 55 hadi 59 (kwa wanaume) au 50 hadi 54 (wanawake).

Kiwango cha mafao kinakokotolewa kwa kutumia Kikokotoo limbikizi cha 1/580, zidisha kwa Malipo ya Mkupuo kwa kiwango cha asilimia 25, zidisha kwa Malipo ya pensheni ya mwezi kwa kiwango cha asilimia 75 gawanya kwa 12.5 ikiwa ni makadirio ya miaka ya kuishi baada ya kustaafu. Endapo mnufaika ataamua kuchukua malipo kwa mkupuo, basi ukokotoaji utakuwa ni asilimia 75 ya malipo ya pensheni ya mwezi. Kiwango hiki ni sawa na kuzidisha kikokotoo limbikizi cha 1/580 zidisha kwa jumla ya miezi iliyo changiwa na kwa asilimia 25 ya kiasi cha pensheni cha mwaka, ikizidiswa kwa 12.5, wastani wa miaka ya kuishi baada ya kusfaafu.

Katika hali ya kustaafu mapema, pensheni inapunguzwa kwa 3.6% ya mapato yenye bima yanayotumika kuhesabu pensheni kwa kila kipindi cha miezi 12, pensheni inachukuliwa chini ya umri wa miaka 60. Lazima pensheni lazima angalau iwe sawa na pensheni ya chini.

Ridhia ya umri wa uzee inatolewa katika umri wa miaka 60 ikiwa na chini ya mchango wa miezi 180 na ni sawa na wastani wa miezi tisini ya michango kabla ya kustaafu na kuzidishwa na idadi ya miezi ya michango.

Chanzo: §23-27 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997 (na marekebisho yake ya 2015); ISSA Nchi ya Tanzania, 2017

Fao la Wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki

Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii, 1997 inatoa fao la wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki wategemezi hawa ni pamoja na mjane/kizuka na watoto chini ya umri wa miaka 18 (umri wa miaka 21, ikiwa ni mwanafunzi, hakuna kikomo cha mlemavu). Ikiwa mfanyakazi anafariki na ametimiza matakwa ya haki kwa umri wa uzee au pensheni batili au alikuwa anaipata tayari, wategemezi wake wanahaki ya ruzuku ya wasaliaji.

Kama hakuna watoto tegemezi, 100% ya pensheni ya marehemu itaenda kwa mjane/mgane wa marehemu.

Pensheni hii italipwa kwa miaka 2 kama mjane/mgane ana umri chini ya miaka 45 au hana mtoto chini ya miaka 15 wakati wa kifo cha mfanyakazi aliye na bima. Endapo kuna watoto tegemezi, mjane/mgane atapewa 40% ya pensheni na 60% itagawanywa kati ya watoto. Pensheni ingawanywa sawia ikiwa kuna zaidi ya mjane/mgani mmoja.

Kama hakuna mjane/mgane, 100% ya pensheni itagawanywa kwa watoto tegemezi (Chini ya miaka 18 au 21 kama bado anahudhuria masomo).Pensheni ya wasaliaji inapatikana milele ay hadi ndoa ya mjane/mgane wa zaidi ya miaka 45.

Wategemezi wanaweza kuchukua sehemu ya pensheni kwa mkupuo, ambapo itakokotolewa kwa kuzidisha asilimia 25 ya kiasi cha pensheni kwa mwaka na asili ya 12.5

Na endapo hakuna mgane/mjane, wala watoto tegemezi basi 100% itagawanywa kwa wazazi wa marehemu.

Chanzo: §33-36 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997 (na marekebisho yake ya 2015); ISSA Nchi ya Tanzania, 2017

Fao la kuumia kazini na kutoweza kuendelea na Kazi

Sheria ya Hifadhi ya Jamii, 1997 inaelezea kuwepo kwa fao la ulemavu unaopatikana kwa sababu zisizo husiana na kazi ya muathirika.  Mfanyakazi mwenye bima ana haki ya ruzuku isio batili kwa angalau kupoteza kiwango cha mapato cha 66.7% na angalau miezi 180 ya mchango au miezi 36 ya michango, ikiwa ni pamoja na angalau miezi 12 katika miezi 36 baada ya ulemavu kuanza. Uchunguzi wa matibabu unaweza kuhitajika na bodi ya tiba ya madaktari iliyoteuliwa na Wizara ya Afya inakagua ulemavu.

Pensheni ya mwezi hukokotolewa kwa kuzidisha kikokotoo limbikizi kwa miezi ya kuchangia zidisha kwa malipo ya pensheni ya mwezi (APE), gawanya kwa 12. Endapo mnufaika atapenda kuchukua sehemu ya pensheni kama malipo ya mkupuo, kiwango cha mwezi kita kokotolewa kwa kutumia asilimia 75% ya malipo ya pensheni ya mwezi. Kiwango cha mkupuo kita kokotolewa kwa kwa kuzidisha kikokotoo limbikizi kwa jumla ya miezi ya uchangiaji na kwa asilimia 25 ya malipo ya pensheni ya mwezi, zidisha kwa 12.5, wastani wa miaka ya kuishi baada ya kustaafu. Kikokotoo limbikizi cha 1/580 kwa miezi ya mwazo 180 ya kuchangia na 1/2000 kwa mezi itakayo zidi.

Ridhia ya ulemavu inalipwa kama mkupuo ikiwa mfanyakazi aliye na bima amekadiriwa na angalau kupoteza 66.7% kiwango cha mapato lakini ana chini ya miezi 180 ya michango.

Chanzo: §28-32 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997 (na marekebisho yake ya 2015); ISSA Nchi ya Tanzania, 2017

Taratibu juu ya Hifadhi ya jamii

  • Sheria ya Mfuko wa Hifandhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) Mwaka, 1997 / National Social Security Fund Act, 1997
Loading...