Muda wa Kusafiri kwenda na kutoka Kazini

Fahamu kuhusu gharama za kusafiri kutoka kazini na kwenda kazini, ni nani wa kulipia gharama hizo, je mwajiri anawajibika kulipia gharama hizo? ni zipi njia za kukwepa foleni ili kukuza uzalishaji? fahamu haya na mengineyo kupitia Mywage.org/Tanzania

Ni upi muda wa kusafiri tunaouongelea hapa?
Huu ni ule muda wa kusafiri unaofanywa na mfanyakazi kila siku kutoka nyumbani kwenda kazini na kutoka kazini kwenda nyumbani

Je sheria za kazi za Tanzania zinaongelea muda huu?
Sheria za kazi za Tanzania hazitoi maelekezo yoyote juu ya malipo kwa ajili ya usafiri wa kutoka nyumbani kwenda kazini na kurudi nyumbani. Mfanyakazi hulipwa kwa saa alizofanya kazi.

Je muda huu unahesabiwa katika saa za kazi?
Muda huu wa kusafiri kutoka nyumbani kwenda kazini na kurudi nyumbani hauhesabiwi katika saa za kazi na hivyo haulipwi.

Je kuna hali inayoweza kupelekea kulipwa muda huu wa kusafiri?
Sheria za kazi za Tanzania hazitoi muongozo wa kulipa ama kufidia gharama za usafiri anazoingia mfanyakazi kila siku kutoka nyumbani kwenda kazini na kurudi nyumbani. Hata hivyo, kabla ya Mei 2010 sheria ilikua ikitoa muongozo wa kumpa mfanyakazi pesa ya usafiri wanaposafiri kwenda mikoa mingine, hii ilikua kwa sekta Fulani Fulani. Sekta hizi ni pamoja na Sekta ya huduma za kilimo, sekta ya biashara na viwanda, sekta ya uvuvi na uanamaji na sekta ya ulinzi binafsi.
Sheria mpya ilipokuja na kutoa  Agizo la Mishahara 2010 ikafuta kipengele hiki. Hata hivyo, mwajiri hakatazwi kulipa gharama hizi. Mwajiri na mfanyakazi au chama cha wafanyakazi wanaweza kuamua kuiweka hii katika makubaliano ya pamoja au hata katika sera ya rasilimali watu au mikataba ya kazi.

Inakuaje kama muda huu wa kusafiri unachukua hata zaidi ya muda wa kazi?
Kutokana na kwamba sheria haijatoa muongozo juu ya hili hivyo basi si lazima kwa mwajiri kulipa. Hata hivyo, mwajiri na mfanyakazi wanaweza wakakubaliana kuweka kipengele hicho katika mkataba wa kazi au sera nyingine za ndani ya kampuni.
 

Loading...