Kinga

This page was last updated on: 2023-05-21

Kutokufanya kazi hatarishi

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano 2004, mwajiri haruhusiwi kumtaka au kumruhusu mfanyakazi mjamzito au mfanyakazi anaye nyonyesha mtoto kufanya kazi katika mazingira hatarishi kwa afya yake au ya mtoto wake.

Ikiwa mfanyakazi wa kike anahusika katika kazi hatarishi, mwajiri wake anahitajika kutoa kazi mbadala, ikiwa inafanyika, kwa vigezo na masharti kama yale ambayo angepewa kwa kazi yake ya kawaida.

Chanzo: §33 (5 & 9) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Kinga dhidi ya Kuachishwa kazi

Ni kinyume cha sheria kwa mwajiri kumwachisha kazi mfanyakazi kutokana na ujauzito au sababu nyingine yoyote inayohusiana na ujauzito wake katika hali zote za uajiri.

Chanzo: § ya 37(3b) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Haki ya kurejea kwenye nafasi ya kazi

Kulingana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, mfanyakazi wa kike ana haki ya kurudi kwenye nafasi yake ya kazi ile ile aliyokuwa katika sheria na masharti sawa baada ya kukamilisha likizo yake ya uzazi.

Chanzo: § 33 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004

Loading...