Ulemavu / Fao la kuumia kazini

This page was last updated on: 2023-05-21

Ulemavu /Fao la kuumia kazini

Majeraha ya kazini inajumuisha ajali za kusafiri, ajali zinazopatikana wakati wa masaa ya kazi; katika mahali pa kazi; au mahali ambapo hangekuwepo isipokuwa kwa ajira yake. Zimegawanywa katika vitengo vinne: (i) kutoweza kabisa kwa kudumu (ii) kutoweza kwa sehemu (iii) kutoweza kwa kudumu na (iv) jeraha kufisha mfanyakazi.

Endapo mfanyakazi atapata ajali itakayo mfanya kushindwa kabisa kufanya kazi, mfuko wa fidia kwa wafanyakazi utamlipa kiasi cha asilimia 70 ya mshahara wake wa siku hadi atakapo pona au atakapo dhihirika kuwa amepata ulemavu wa kudumu kwa cheti cha daktari.

Ikititokea mfanyakazi amepata ulemavu, lakini bado anaweza kufanya kazi, kiasi cha fidia kitategemea tathimini ya kiwango cha ulemavu aliopata. Kama kiwango cha ulemavu ni chini ya asilimia 30, atalipwa kiasi kitakachokubaliwa kwa mkupuo. Kiwango cha juu cha fidia ya ulemavu huu ni mara 84 ya mshahara wa mwezi wa mfanyakazi aliye na bima, kulingana na kiwango cha ulemavu alicho tathiminiwa.

Ikiwa mtu mwenye bima anahitaji kushughulikiwa na wengine ili kutekeleza kazi za kila siku, fidia ya 25% ya ulemavu wa kudumu utalipwa.

Na endapo mfanyakazi atapata ulemavu wa muda, na ikiwa amejiunga na bima, baada ya bodi ya madaktari kujiridhisha, ataweza kulipwa mafao ya ulemavu wa muda yapatayo asilimia 70 ya mshahara wake wa siku kabla ya kupatwa na ajari, kwa kipindi cha hadi miezi 24 au hadi atakapo pona au cheti cha daktari kuthibitisha ulemavu wa kudumu. Hali ya kushindwa kufanya kazi sharti iwe imedumu kwa walau siku tatu tangu kupatwa na ajari.

Na endapo mfanyakazi atafariki kutokana na ajari, watengemezi (Mke/mme, watoto wadogo au wazazi) wata lipwa fao la wategemezi. Mjane/mgane au mwezi wa mfanyakazi huyo ana haki ya kulipwa pension ya kila mwezi sawa na asilimia 40 ya kiasi ambacho mfanyakazi aliye fariki angelipwa endapo angepata ulemavu wa kudumu, au mara mbili ya kiasi hicho iwapo kitalipwa mara moja kwa mkupuo. Watoto walio achwa watalipwa sawa na asilimia 20, iwapo wamebaki na mzazi mmoja, au asilimia 40 iwapo wamepoteza wazazio wote, ya kiasi ambacho mzazi (mfanyakazi) aliyefariki angelipwa endapo angepatwa na ulemavu wa kudumu. Umri wa watoto hao usizidi miaka 18 (Sheria haitamki chochote juu ya watoto walio zidi umri huo na wangali wanafunzi au ni walemavu, hivyo ni wategemezi kwa namna ya pekee kwa mzazi aliyefariki).

Endapo hakuna wategemezi wenye sifa, asilimia 40 yote ya malipo ya siku endapo mfanyakazi angepatwa na ulemavu wa kudumu italipwa kwa wazazi tegemezi wa mfanya kazi aliye fariki, ndugu, wajukuu, babu/bibi; na endapo hawa sio watengemezi kwa asilimia 100, watalipwa kiasi Fulani kwa mkupuo.

Chanzo: § 39-40 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997 (na marekebisho yake ya 2015); ISSA Nchi ya Tanzania, 2017

Loading...