Haki za Vyama vya Wafanyakazi

This page was last updated on: 2023-05-21

Uhuru wa Kujiunga na chama cha wafanyakazi / waajiri

Katiba ya Tanzania inatoa Uhuru wa ushirika wakati Sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi inaruhusu wafanyakazi na mwajiri kuanzisha muungano.

Kulingana na Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, chama cha wafanyakazi ni idadi yoyote ya wafanyakazi inayohusiana pamoja kwa madhumuni, ikiwa kipekee au kwa madhumuni mengine, ya kusimamia uhusiano kati ya wafanyakazi na waajiri wao au mashirika ya waajiri ambayo waajiri wao ni wanachama. Wanaweza kutunga sheria zao na kanuni za usimamizi, kanuni hizi zisiwe kinyume na sheria zilizopo.

Lazima mashirika yasajiliwe na Wizara kwa kusajili sheria na kanuni zao; fomu iliyoagizwa (ikamilishwe inavyostahili na kutiwa saini na katibu wa shirika au shirikisho); nakala iliyodhibitishwa ya rejesta ya kuhudhuria na kumbukumbu za mkutano wake wa kuanza; na maelezo yoyote zaidi yanayohitajika na Msajili. Chama cha wafanyakazi kinasajaliwa ikikwa Msajili ametosheka ya kuwa shirika limetimiza mahitaji na anatoa cheti cha usajili kwa shirika. Kujaza kwa fomu ya usajili unafaa kufanywa tena ikiwa kuna mabadiliko yoyote katika sheria na usimamizi.

Mwajiri haruhusiwi kuingilia katika maswala ya chama cha wafanyakazi. Mwajiri anaweza kupunguza madeni ya shirika kutoka kwa mishahara ya wanachama baada ya idhini iliyoandikwa kutoka kwao

Chanzo: §20 ya Katiba ya Tanzania; §9, 45-50 & 61 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi 2004

Uhuru wa makubaliano ya hiyari

Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, 2004 inaruhusu makubaliano ya hiari katika shughuli zote za biashara. Makubaliano ya hiyari ni makubaliano yalioandikwa na kutamatishwa na chama kilichosajiliwa cha wafanyakazi na mwajiri au shirika liliosajiliwa la waajiri kuhusu suala lolote la kazi.

Ili kukubaliana kwa hiyari, shirika la mwajiri na chama kinachotambulika cha wafanyakazi lazima kikubaliane kwa nia njema na katika hali sawa. Lazima pia mwajiri atoe rasilimali na maelezo sawa kwa mashirika yanayohusika katika makubaliano ya hiyari. Lazima watu wanaohusika katika makubaliano waweke maelezo watakayo pewa na mwajiri kwa siri.

Lazima makubaliano ya makubaliano ya hiyari yaandikwe na kutiwa saini na wahusika. Makubaliano ya hiyari ni ya kubana kwa wahusika kwa makubaliano, wanachama wowote wa wahusika kwa makubaliano, na wafanyakazi ambao sio wanachama wa chama cha wafanyakazi kinachohusika kwa makubaliano (ikiwa chama cha wafanyakazi kinatambulika kama ajenti wa kipekee wa makubaliano) ila kama makubaliano yanasema vingine. Nakala ya makubaliano lazima yashtakiwe kwa Kamishna wa Kazi.

Chama cha wafanyakazi kinachotambulika pamoja na mwajiri au shirika la waajiri linaweza kubuni makubaliano ya pamoja yanayoanzisha mdahalo wa kuhusika kwa wafanyakazi katika mahali pa kazi. Tume ya Wafanyakazi husimamia mazungumzo yoyote yanayohusiana na kubuniwa kwa mdahalo wa kuhusika kwa wafanyakazi katika mahali popote pa kazi kwa kuzingatia kanuni zozote za maadili mema ya kufanya kazi zilizochapishwa na Baraza kuhusu kuhusika kwa wafanyakazi.

Baraza linalo shukulikia masuala ya kazi, uchumi na jamii (LESCO), limeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi za kazi, na lina jumla ya wajumbe 16 ambapo, wa 4 ni wawakilishi mmoja kutoka Serikali, makundi ya waajiri na wafanyakazi. Wajumbe wengine wa 4 wanateuliwa kwa mujibu wa utaalamu wao kwenye masuala ya kazi, uchumi na jamii. Baraza linamshauri Waziri kwenye masuala ya Soko la ajira la taifa na sheria yeyote kabla ya kupifikishwa kwenye Baraza la Mawaziri. Aidha, Baraza lina wajibu wa kukusanya na kuwasilisha taarifa na takwimu zinazohusu masuaæa ya usimamizi wa sheria za kazi nchini.

Chanzo: §66-74 ya Sheria za Ajira na Kazi 2004; §9 ya Sheria za Ajira na Kazi (Marekebisho ya Ziada), 2015; §66-74 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, 2004; §9 ya Sheria ya Kazi na Ajira (Marekebisho madogo), 2015; §3-11 ya Sheria ya Taasisi za Kazi, 2004

Haki ya Kugoma

Kulingana na sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, kugoma kunamaanisha kuwacha kazi kwa wafanyakazi kikamili au kwa sehemu ikiwa kuwacha kunamaanisha kulazimisha mwajiri, mwajiri mwingine yoyote, au shirika la waajiri ambapo mwajiri anashiriki, ili kukubali, kurekebisha au kuwacha dai lolote ambalo linaweza kuleta mzozo.

Njia ya lazima ya usuluhishaji, upatanisho mrefu na changamani na utaratibu wa upatanisho kabla ya vitendo vya mgomo kijumla huzuia haki ya kugoma. Kuna kipindi cha lazima cha upatanisho cha siku 30 kabla ya mgomo wa kisheria uchukuliwe. Mgomo unazuiwa kwa wafanyakazi wanaohusika katika huduma muhimu isipokuwa wakati makubaliano ya hiyari yanatoa huduma chache wakati wa mgomo na ya kwamba mgomo umeidhinishwa na Kamati ya Huduma Muhimu.

Mgomo pia unazuiliwa kwa mfanyakazi aliyebanwa na makubaliano ambayo yanahitaji masuala katika mzozo kurejelewa kwa upatanishaji; au kubanwa na makubaliano ya hiari au tuzo la usuluhishaji ambao unasimamia mzozo unaolalamikiwa; au kubanwa na uamuzi wa mshahara ambao unasimamia masuala yanayozozaniwa wakati wa mwaka wa kwanza wa uamuzi. Wanachama wa shirika lazima wa idhinishe mgomo kwa kura ya siri. Mgomo ni halali ikiwa mzozo na mbinu zote za kusuluhisha mzozo (upatanishi, usuluhishi na usuluhushi) zitashindwa.

Lazima wanachama wa shirika wajulishe mwajiri masaa arobaini na nane kabla ya nia yao kugoma.

Wagomaji wanazuiwa kushawishi wengine kugoma (katika kuunga mkono mgomo au katika kupinga mgomo halali), kufungia waajiri katika mahala pa kazi na kuzuia waajiri kuingia mahala pa kazi.

Sheria inazuia mwajiri kuajiri mfanyakazi mbadala wakati wa mgomo halali au katika kufungia wafanyakazi nje. Chama cha wafanyakazi kinaweza kufanya mgomo wa pili katika kuunga mkono mgomo halali (mgomo wa kwanza) ikiwa notisi ya siku kumi na nne imepewa mwajiri wa pili. Mgomo wa pili unaweza kushurutisha mwajiri kutatua mzozo ambao unaleta mgomo wa kwanza.

Waajiri pia wanahaki ya kufungia wafanyakazi nje. Haki hii iko chini ya kanuni na vikwazo sawa kama haki ya kugoma.

Chanzo: §20 ya Katiba ya Tanzania, §75-85 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004

Loading...