Kubadili Kazi

Fahamu mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuamua kubadili kazi au muelekeo wa kazi, ni sawa kubadili kazi kwasababu ya mshahara pekee? Fahamu yote na mengine mengi hapa katika mywage.org/Tanzania

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA KUBADILISHA KAZI

Ni kwanini watu hubadili kazi?
Kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea watu kubadili kazi, sababu hizi ni pamoja na uhitaji wa kubadili mazingira ya kazi na kukutana na changamoto mpya. Sababu nyingine yaweza kua ni uhusiano mbovu kati ya mfanyakazi na mwajiri wake ambapo hupelekea mtu kuamua kubadili kazi, lakini sababu hii si sababu yenye mashiko kwa maana hakuna kkazi inayokosa changamoto kama hizi hivyo basi ni muhimu kutatua tatizo kuliko kulikimbia. Watu husema, watu madhubuti hudumu lakini wakati wa mashaka na matatizo hupita tu.

Ni maandalizi gani ya muhimu kufanywa kabla ya kubadili kazi?
Fanya uchunguzi yakinifu katika uzoefu wako, misimamo yako, uwezo na ujuzi wako kwa kulinganisha na kazi mpya uitakayo. Njia rahisi ya kufanya hivyo ni kupitia kazi ulizokua unazifanya na kuzimaliza ipasavyo katika kazi yako ya sasa.

Tafuta taarifa za ndani
Jaribu kupata ushauri kutoka kwa marafiki au jamaa ambao wako katika kazi ambazo unaelekea kuzifanya au kampuni unayotaka kujiunga nayo. Mara nyingi taarifa unazopata kwao sio ukweli kwa 100% hivyo ni vizuri ukachuja taarifa hizo na kutumia kama kipimo na sio taarifa kamili. Taarifa hizi pia zinaweza kusindikizwa na kusoma sehemu mbalimbali kuhusu kampuni ama kazi unayotaka kuifanya. Njia hizo zaweza kua kupitia semina mbalimbali, kusoma magazeti, makala nakadhalika pale zinapopatikana.

Je una elimu inayotakiwa katika kazi mpya?
Fanya upembuzi yakinifu wa elimu yako na ueledi wako kwa kulinganisha na kazi unayotaka kwenda kuifanya. Kuna kazi zinazohitaji elimu mahsusi kuweza kuzifanya. Hakikisha unavyo vigezo hivyo kabla ya kuamua kubadili kazi yako. Jiunge na chuo ama taasisi yoyote inayotoa elimu inayotakiwa. Hakikisha unafanya utafiti wa kutosha wa elimu uitakayo ili uweze kuvuna kikamilifu.

Ni wapi nitapata taarifa hizo?
Unaweza kupitia magazeti, majarida, blogu, tovuti nakadhalika katika kutafuta taarifa ya namna ya kubadili kazi. Kusanya maoni kadri iwezekanavyo ili kuweza kupata taarifa zinazojitosheleza kuhusu kazi mpya. Pia waweza kuomba kukutana na mwajiri mpya kama kubadili kwako kazi kunahusisha kubadili mwajiri. Ikitokea umepata fursa ya kukutana na mwajiri mpya jitahidi uvae mavazi mahusui ya ofisini. Soma zaidi kuhusu mavazi kabla ya usahili katika vidokezo vya mavazi na usahili.

Ni wakati gani wa kufanya maamuzi?
Ukishakua na taarifa zote za muhimu unazozihitaji kuhusu kazi mpya au mulekeo mpya wa kazi basi huo ndo muda muafaka wa kufanya maamuzi. Wataalam wanashauri usibalishe kazi kwasababu ya mshahara pekee au mategemeo ya kukuza kipato tu. Lazima ujuzi, uzoefu na ufanisi wako uendane na kazi hiyo uitakayo na hivyo ni vyema kuoanisha vitu hivi zaidi kuliko malipo. Baada ya kufanay yote haya sasa waweza kufanya maamuzi.

Soma Zaidi:

Kuandaa CV

Barua ya kuomba Kazi











Loading...