Kazi na Kuugua

Likizo ya kuugua yenye malipo

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano 2004, Kila mfanyakazi aliye pata cheti cha daktari kuwa yu mgonjwa anahaki ya kupata mapumziko yenye malipo (ruzuku ya ugonjwa) kwa kipindi cha siku 126 katika kipindi cha likizo cha miezi 36. Ili kuwa na sifa za likizo ya ugonjwa, mfanyakazi mgonjwa lazima awe amefanyakazi kwa mwajiri huyokwa kipindi kisicho pungua miezi sita ndani ya miezi 12 (mwaka mmoja) kabla ya kuugua, au awe ameajiriwa kwa mkataba wa kazi maalum na mwajiri huyo.

Kwa siku 63 za mwanzo atapata mshahara wake wote na kwa siku nyingine 63 atapata nusu ya mshahara wake.

Chanzo: §32 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano 2004; ISSA Nchi ya Tanzania, 2017

Huduma ya matibabu

Ruzuku za afya zipo kwa wafanyakazi wenye bima na zinajumuisha huduma ya kuzuia na kuponya, dawa, potholojia ya kliniki na eksirei, upimaji wa maabara, kulazwa hospitalini, upasuaji mdogo na mkubwa. Ruzuku hizi ziko tu kwa huduma za tiba zinazotolewa na madaktari, wauguzi na watoaji wengine wa tiba katika hospitali zilizoidhinishwa.

Chanzo: §42 Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997, §52 Sheria za Ruzuku ya Jamii (Urekebishaji) 2012

Usalama wa kazi wakati wa kuugua

Kwa mujibu wa sehemu ya 102 ya Sheria ya Afya na Usalama mahali pa kazi 2003, mwajiri haruhusiwi kumwachisha mfanyakazi wakati wa kuugua na magonjwa yanayotokana na kazi. Endapo hawezi kufanya kazi kutokana na sababu za kiafya, mwajiri anaweza kuvunja mkataba muda wowote kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwenye Sheria ya Ulinzi wa Ajira 1964.

Chanzo: §102 ya of Sheria ya Afya na Usalama mahali pa kazi 2003; Sheria ya Ulinzi wa Ajira 1964

Taratibu juu ya Kazi na Kuugua

  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Sheria ya Mfuko wa Hifandhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) Mwaka, 1997 / National Social Security Fund Act, 1997
loading...
Loading...