Likizo ya Ubaba

Ubaba, uzazi, likizo, sheria, ugonjwa, huruma, kila mwaka, mfanyikazi, mwajiri, mkataba, mtoto, ujauzito, kujifungua, kuzaa, sera Mywage Tanzania

Kando na Likizo ya Kila Mwaka, kuna aina nyingine za likizo ninazostahili?

Zaidi ya Likizo ya Kila Mwaka unastahili Likizo ya Uzazi/Ubaba, Likizo ya Ugonjwa na Likizo ya Huruma. Kuna aina za likizo zinazotolewa chini ya sheria. Hata hivyo, Mkataba wa Pamoja au sera ya kindani inaweza kutoa aina zaidi za likizo.

 Je, ninastahili siku ngapi za Likizo ya Ubaba?

Muda wa Likizo ya Ubaba ni siku tatu katika mzunguko wa likizo ambayo ni miezi thelathini na sita. Siku hizo tatu ni jumla ya siku haijalishi idadi ya watoto ambao wamezaliwa katika mzunguko huo wa likizo.

Je, kuna kikomo cha mara ambazo ninaweza kuchukua Likizo ya Ubaba?

Kulingana na sheria zinazosimamia sekta binafsi mfanyikazi anaweza kuwa na hadi mihula minne ya Likizo ya Ubaba katika muda wake wa ajira akiwa na mwajiri mmoja.

Je, ni lini ninaweza kuanza Likizo yangu ya Ubaba?

Likizo ya Ubaba inaweza kuchukuliwa ndani ya siku saba za mtoto kuzaliwa.

Loading...