Dondoo za kutafuta na kuandika maombi ya Ajira

Dondoo za kutafuta na kuandika maombi ya Ajira

Wapi naweza kupata Ajira/kazi Tanzania?

Nchini Tanzania unaweza kutafahamu kuhusu uwepo wa ajira kupitia njia mojawapo kati ya zifuatazo:

  • Soma/tembelea vyombo vya habari vyenye taarifa za ajira kama vile magazeti, tovuti na blogs ambazo zinafahamika sana kwa kutoa matangazo hayo;
  • Jenga tabia ya kutepekua tovuti za kampuni ambayo ungependa kufanya nayo kazi. Baadhi ya kampuni huweka nafasi za ajira walizonazo kwenye tovuti zao na sio kwenye magazeti au vyombo vinginevyo vya habari. Hivyo kama utakuwa na mazoea ya kutembelea tovuti zao utaweza kupata fursa ya kuziona nafasi za ajira zilizopo na kutuma maombi yako ya ajira kwa wakati.
  • Jadili na marafiki na jamaa ambao wanaweza kukuwezesha kupata taarifa muhimu zitakazo kwezeshe kufahamu nafasi za ajira zilizokwisha kutangazwa kama vile kwenye magazeti , mitandaoni.
  • Unaweza pia kutumia wakala wa ajira wanaotambulika nchini Tanzania. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwatembelea na kujua mahitaji yao ili waweze kukuingiza kwenye taarifa zao. Mara nyingi taarifa kama wasifu wako na barua za maombi huitajika ili kufanikisha lengo hilo. Zingatia kuainisha njia ya mawasilianao yako hususani namba za simu ambazo zinapatikana muda wote wa kazi.
  • Tembelea wakalam wa wa ajira wa taifa (TaESA- Tanzania Employment Services Agency) kwa taarifa na kujua kama kuna nafasi za ajira ambazo zinaalika maombi.
  • Pia unaweza kutuma maombi ya kazi hata kama haijatangazwa popote kwa kampuni unayopenda kufanya nayo kazi. Yaelekeze maombi yako kwa office ya Rasilmali watu ya kampuni husika ukijieleza juu ya wasifu wako hasa katika fani unayoiomba. Hii inaweza kukupa fursa ya kuitwa kwa mazungumzo zaidi hususani kama kampuni itakuwa imependezwa na wasifu wako na hasa ujuzi wako kwa nafasi ya ajira uiombayo/uitafutayo. 

Jinsi gani naweza kuomba kazi?

Mara utakapo kuwa umepata taarifa za kutosha za fursa ya ajira au unapotaka kuandia maombi yako kwa kazi ambayo haijatangazwa bado na kampuni zingatia yafuatayo:

  • Tuma barua yako rasmi ya maombi, ikiwa na kichwa cha habari kinachoendana na nafasi unayoiamba na ukielezea zaidi juu ya sifaulizo nazo ukilinganisha vigezo na sifa wazitakazo. Zingatia taratibu zote za kuandika barua za kikazi na weka mawasiliano yako ya uhakika, kasha itume na subiri mawasiliano toka kwao. 
  • Hakikisha unatuma barua kwa anwani sahihi iliyo ainishwa kwenye tangazo la nafasi ya ajira. Kama umena tuma maombi kwa nafasi ambayo haijatangazwa, unaweza kuwapigia simu kufuatilia kama wamepata maombi yako baada ya walau juma moja.
  • Hakikisha wasifu wako (CV) umebeba sifa zako zinazoendana na ajira unayoiomba na usiwe mrefu sana.
  • Andika barua yako ya maombi ukielezea kwa ufanisi na umahiri wa kutosha sifaulizo nazo juu ya kazi unayo iomba. Hii itakupa nafasi kubwa ya kuitwa kwa mashaurioano zaidi na mwajiri mtarajiwa.
  • Ambatanisha nakala za vyeti vyako vya elimu kuanzia diploma hadi shahada ya juu. Pia hakikisha unapata barua ya udhamini na kuiambatanisha kama itahitajika pia. 

Kutuma maombi yako kwa njia ya barua pepe

  • Unapotuma maombi yako kwa barua pepe tumia anwani yako na endapo unatumia sanduku la posta hakikisha sanduku hilo ni lako au ni la mtu wa karibu yako ili barua utakazo tumiwa zisipotee.
  • Kila mara barua yako ya maobi, wasifu na nakala nyinginezo unazituma kwa pamoja. Unaweza kutengeneza orodha ya nakala za kutuma ili kuhakikisha unatuma nakala stahiki bila ya kuzisahau. Soma kwa mara ya mwisho kabla ya kutuma ili kusahihisha makosa mabayo huenda umeyafanya. 
  • Baada ya kutuma subiri kupata mawasiliano toka kwao, hakikisha simu yako ipo hewani muda wote wa kazi, yaani asubuhi hadi jioni kwa kipindi cha kutosha ili kupokea mawasiliano watakayo yatuma kwako.
Loading...