Unyanyasaji wa Kimapenzi

Unyanyasaji, unyanyasaji wa kimapenzi, kijinsia, kingono, udhalilishaji, ubakaji, mzozo, familia, kazini, wafanyakazi, makosa, jinai, sheria, ubaguzi, mapendeleo, unajisi, malalamiko, mlalamishi, upatanishi

Je, sheria inasema nini kuhusu Unyanyasaji wa Kimapenzi?

Sheria hukataza aina yoyote ya unyanyasaji wa kimapenzi katika maeneo ya kazi na hata pia katika mazingira mengine yoyote. Sheria  ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004, imesema unyanyasaji wa kimapenzi kuwa aina ya ubaguzi, imeukataza na imetoa hukumu ya faini isiyozidisha shilingi milioni tano.

Kanuni za Maadili Mema za Utumishi wa Umma ziko wazi na kwa undani kabisa kuhusu vipengee vya unyanyasaji wa kimapenzi na unyanyasaji wa kimapenzi unajumuisha nini katika ajira. Zinasema:

  • Mtumishi wa umma anapaswa kujiepusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi kazini. Vivyo hivyo atajiepusha na tabia za aina zote ambazo zinaweza kujumuisha unyanyasaji wa kimapenzi ambazo ni pamoja na:

i) Shinikizo la shughuli ya kimapenzi au fadhila za kimapenzi na wafanyikazi wenza.
ii) Ubakaji, ushambulizi na udhalilishaji wa kimapenzi au unajisi wowote wa kimapenzi.
iii) Tabia ya kimwili ambayo asili yake ni ya kimapenzi kama vile kumgusa, kumchuna, kumgonga, kumkamata, na au kumpapasa mwili, nywele au mavazi ya mfanyikazi mwingine.
iv) Masengenyo, ishara,  kelele, vichekesho, maoni ya kimapenzi kwa mtu mwingine kuhusu jinsia au mwili wa mtu mwingine.
v) Kutoa au kutendewa kwa mapendeleo, ahadi au zawadi na kutoa au kukubali fadhila za kimapenzi.

Je, kuna sheria nyingine yoyote nchini Tanzania ambayo inashughulikia Unyanyasaji wa Kimapenzi?

Sheria ya Matoleo Maalum ya Makosa ya Kimapenzi ya 1998 inaadhibu pia unyanyasaji wa kimapenzi na zifuatazo zinachukuliwa kama aina ya tabia zinazojumuishwa katika unyanyasaji wa kimapenzi: kusababisha usumbufu wa kimapenzi kwa mtu, kusema neno lolote, kutoa sauti au ishara yoyote, au kuonyesha kitu chochote, ikiwa ni pamoja na kiungo chochote iwe cha kike au cha kiume kwa lengo kwamba neno au sauti hiyo itasikika, au kwamba ishara itaonekana na mwanamke.

Je, kuna hatua zozote zilizowekwa na sheria kwa waajiri kukomesha Unyanyasaji wa Kimapenzi mahali pa kazi?

Sheria inamuhitaji kila mwajiri kujitahidi kukomesha unyanyasaji/ubaguzi wa kimapenzi katika sera yoyote ya ajira. Sheria imeendelea na kutaka mwajiri kuanzisha mpango wa kukomesha ubaguzi kazini na Kamisha wa Wafanyikazi.

Ninawezaje kuwasilisha malalamiko ya Unyanyasaji wa Kimapenzi?

Unyanyasaji wa kimapenzi unashughulikiwa kama malalamiko na kwa mashirika ambayo yana Mwongozo wa Utaratibu wa Malalamiko, utahitajika kufuata utaratibu ulioangaziwa hapo. Utaratibu wa kawaida ulioangaziwa chini ya sheria ni kwa mlalamishi/wewe kuwasilisha malalamiko kwa kuandika kwa meneja au msimamizi wako. Meneja huyo atampigia simu mlalamishi na mshukiwa na ikihitajika, waakilishi wao, na kutatua tatizo. Ikiwa meneja/msimamizi huyo mmoja ndiye mshukiwa basi meneja mkuu zaidi ataitwa.

Malalamiko hayo basi yatashughulikiwa kindani na kama upande wowote hautaridhishwa na matokeo ya malalamiko au njia ambayo yameshughulikiwa sheria inaruhusu mtu huyu kukata rufaa kwa Tume ya Upatanishi na Maamuzi. Katika Tume ya Upatanishi na Maamuzi mzozo utapitia kwanza hatua ya upatanishi; ikiwa upatanishi utashindwa basi utaelekezwa kwa maamuzi. Ukifanikiwa basi suala litaishia hapa na wahusika warejelea kazi zao za kawaida.

Kwa mashirika ambayo hayana utaratibu wa kindani wa malalamiko, malalamiko yanaweza kuwasilishwa moja kwa moja kwa Tume ya Upatanishi na Maamuzi kama kama mzozo.

Soma zaidi

Ng’ amua ikiwa unapata pesa zaidi au kidogo kuliko wenzi wako kwa kutumia Ukaguzi wa Mishahara .

Loading...