Hitaji la Notisi na Kiinua Mgongo

This page was last updated on: 2023-05-21

Hitaji la Notisi

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 inataka kuwe na notisi ya kusudio la kusitisha ajira ya huduma za mfanyakazi.

Mojawapo wa wahusika ana haki ya kusitisha ajiri kwa sababu tofauti ikiwa ni pamoja na kusitisha ajira kihalali chini ya sheria zisizoandikwa; mfanyakazi kuacha kazi kwa sababu mwajiri aliendeleza uajiri usiovumilika kwa mfanyakazi; kushindwa kufanya upya mkataba wa kipindi cha kudumu kwenye kauli sawa ikiwa kulikuwa na tarajio la kufanywa upya bila shaka; kukataa mfanyakazi kurejea kazini baada ya likizo ya uzazi ambayo inatolewa chini ya sheria; kukataa kuajiri mfanyakazi upya ikiwa mwajiri amesitisha uajiri wa wafanyakazi kadhaa kwa sababu sawa na amejitolea kuajiri upya mmoja wao au zaidi.

Mojawapo wa wahusika anaweza kusitisha mkataba wa uajiri baada ya kutoa hati za sheria au kulipa badala ya notisi. Kwa kusitisha mkataba wa muda usiodhahiri, muda wa notisi unategemea na kipindi cha huduma cha mfanyakazi kama ifuatavyo:

-           siku 7 kwa huduma ya mwezi moja au chini;

-           siku 4 kwa mfanyakazi wa ajira ya kila siku; na

-           siku 28 kwa mfanyakazi wa ajira ya mwezi.

Muda mrefu wa notisi unaweza kukubaliwa kati ya wahusika ikiwa sawia kati ya mfanyakazi na mwajiri. Notisi ya kusitishwa inafaa iwe imeandikwa, ikielezea sababu za kusitishwa na tarehe ambayo notisi ilitolewa. Notisi ya kusitishwa haiwezi kutolewa wakati wa kipindi cha likizo kinachoruhusiwa chini ya sheria au notisi ambayo inaenda pamoja na kipindi kama hiki cha likizo.

Kusitishwa kwa ajira sio kwa haki ikiwa mwajiri atashindwa kuthibitisha ya kwamba sababu ya kusitishwa ni halali; ina husiana na mwenendo, uwezo au upatanifu wa mfanyakazi, au unahusiana na mahitaji ya uendeshaji ya mwajiri.

Ili kuamua ikiwa kusitishwa na mwajiri ni kwa haki, mwajiri, msuluhishi, au Kitengo cha Kazi cha Mahakama Kuu wataangalia Kanuni yoyote ya Desturi Njema.

Ikiwa msuluhishi au Mahakama ya Kazi itaamua ya kwamba kusitisha sio kwa haki, msuluhishi au Mahakama inaweza kuamuru mwajiri kurejesha mfanyakazi kutoka tarehe ya kusitisha bila kupoteza ujira wowote kwa muda ambao mfanyakazi hakuwepo kazini kwa sababu ya usitisishaji usio wa haki; au kuajiri mfanyakazi katika masharti yoyote ambayo msuluhishi au Mahakama inaweza kuamua; au kulipa mfanyakazi fidia angalau ya ajira ya miezi 12.

Agizo la fidia linalofanywa chini ya Sheria ni nyongeza kwa, na sio badala ya, kiwango chochote ambacho mfanyakazi anastahili katika masharti ya sheria au makubaliano yoyote.

Agizo la urejeshaji au uajiri likitolewa na msuluhishi au mahakama, mwajiri analipia fidia ya mshahara wa miezi 12 kwa nyongeza ya deni la mshahara na ruzuku nyingine kutoka kwa tarehe ya kusitishwa kusiko kwa haki hadi tarehe ya malipo ya mwisho.

Chanzo: § ya 36-41 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Kiinua Mgongo

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 inatoa Kiinua Mgongo. Mfanyakazi ana haki ya kiinua mgongo ikiwa amemaliza angalau mwaka wa huduma na mwajiri. Kiinua mgongo Tanzania ni sawa na angalau mshahara wa siku 7 kwa kila mwaka wa ajira uliokamilishwa hadi upeo wa miaka kumi.

Kiinua mgongo hakitalipwa iwapo mfanyakazi ataacha kazi kwa minajili ya utovu wa nidhamu, kushindwa kutekeleza majuku yake kutokana na kuumia na kama atakataa kupangiwa kazi mbadala na mwajiri husika au mwingineyo, au endapo mfanyakazi atakuwa ametimiza umri wa kustaafu au endapo mkataba wa ajira umekwisha au kusitiswa kwa mujibu wa muda wa mkataba. Malipo ya kiinua mgongo hayaathiri haki ya malipo mengineyo ambayo ni stahiki kwa mfanyakazi husika.

Chanzo: § ya 42 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Loading...