Kazi na Sikukuu

This page was last updated on: 2023-05-21

Likizo yenye malipo

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 inatoa livu ya kila mwaka baada ya kukamilisha mwaka mmoja wa huduma na mwajiri. Mfanyakazi anastahili siku 28 za livu yenye malipo ya kila mwaka, pamoja na sikukuu zozote za kitaifa ambazo zinaweza kuwa wakati wa kipindi hicho cha livu. Siku za mfululizo pia inamaanisha kwamba mwishoni mwa wiki pia ni pamoja na wakati wa kuondoka kwa kila mwaka.

Livu ya kila mwaka inaweza kupunguzwa na idadi ya siku wakati wa mzunguko wa livu, ambazo hutolewa kama livu yenye malipo na mwajiri iwapo mfanyakazi atakubali.

Mfanyakazi mwenye miezi chini ya sita kazini hatakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya ajira na mahusiano kazini. Hii haita husisha mfanyakazi aliyeajiriwa kwa msingi wa musimu au mfanyakazi, mwenye utumishi wa chini ya miezi sita na ambaye amefanya kwa zaidi ya mara moja katika mwaka.

Mwajiri anaweza kuamua muda wa livu ya kila mwaka bora livu hiyo isizidishe miezi sita baada ya muda wake kufikia. Muda wake unaweza kuongezwa hadi kipindi cha miezi 12 iwapo mfanyakazi atakubali na ikiwa kirefusho hicho kinakubaliwa na mahitaji ya utendakazi ya mfanyakazi.

Huenda mwajiri asimruhusu mfanyakazi kuchukua livu ya kila mwaka kwa niabaya livu nyingine ambayo mfanyakazi anastahili. Mwajiri akiwa na kibali kutoka kwa mfanyakazi, anaweza kumhitaji au kumruhusu mfanyakazi huyo kumfanyia kazi mwajiri wakati wa kipindi cha livu ya kila mwaka kwa masharti kwamba mfanyakazi huyo hatafanyakazi kwa kipindi kinachoendelea cha miaka miwili. Mwajiri anastahili kumlipa mfanyakazi mshahara wa mwezi mmoja kufidia livu ya kila mwaka ambayo mfanyakazi anastahili au alihitajika kufanya kazi. Mfanyakazi anastahiki mishahara yake ya kawaida wakati wa kipindi chake cha livu ya kila mwaka. Lazima malipo yalipwe kabla ya livu kuchukuliwa.

Mwajiri amekatazwa kulipa fidia inayotokana na livu ya kila mwaka isipokuwa wakati wa kukatishwa kwa ajira au kuisha wa kila kipindi kulingana na mfanyakazi aliyeajiriwa kulingana na msimu. Kando na toleo hili, makubaliano yoyote yanayotoa fidia kwa niaba ya livu ya kila mwaka ni batili na sio halali. Kiwango cha fidia uhesabiwa kwa kiwango cha mshahara wa kawaida wa siku kwa kila siku 13 ambazo mfanya kazi alifanya kazi au alistahili kufanya kazi.

Chanzo: Sehemu ya 29-31 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004; §6 ya Sheria za Ajira na Kazi (Marekebisho ya Ziada), 2015

Malipo siku za mapumziko kitaifa

Wafanyakazi wana haki ya kuendelea kulipwa ujira wao  wakati wa mapumziko ya kitaifa (za dini na za kiserikali). Siku za mapumziko kwa kawaida hutangazwa na serikali (kwa kawaida zipo siku za mapumziko 17 kwa mwaka).

Siku za mapumziko husimamiwa na sheria ya Siku za mapumziko ya mwaka wa 1966. Hujumuisha siku zifuatazo za mapumziko ya kitaifa. Mwaka mpya (1 Januari), Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar (12 Januari), Siku ya Maulidi (Januari 03), Ijumaa kuu (Aprili 03), Jumapili ya Pasaka (Aprili 05), Jumatatu ya Pasaka (Aprili 06), Siku ya Sheikh Abeid Amani Karume ( Aprili 07), Siku ya Muungano (Aprili 26), Siku ya wafanyakazi (Mei 01), Siku ya Maonyesho ya Kibiashara ya Kimataifa/ Saba Saba (Julai 07), Nane nane (Wakulima) (Agosti 08), Eid-el-Fitri( Julai 17 ), Siku ya Mwalimu Nyerere (Oktoba 14), Idd-El-Hajj (September 23), Siku ya Uhuru na wa Jamhuri ya Tanzania (Desemba 09), Siku ya Krismasi (Desemba 25), Boxing Day (Desemba 26). Sikukuu za kiislamu zinategemea sana mwandamo wa mwezi na kwa hivyo zinaweza kubadilika.

Sikukuu zinazokuwa Jumamosi au Jumapili huzingatiwa siku hizo. Sheria Nambari 10 ya 1994 ime badilishwa na sikukuu zinazokuwa Jumamosi au Jumapili hazifidiwi tena.

Chanzo: Sheria ya Siku za Mapumziko ya mwaka wa 1966

Siku ya Mapumziko ya juma

Wafanyakazi wana haki ya kupata saa 24 mtawalia za mapumziko kila wiki kati ya siku ya mwisho ya kufanya kazi katika wiki moja na siku ya kwanza ya kawaida ya kufanya kazi ya wiki inayofuata. Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inahitaji kwamba siku ya mapumziko ya kila wiki, kikanuni, inapaswa kuwa Jumapili kwa wafanyakazi wote.

Makubaliano yaliyoandikwa yanaweza kutoa kipindi cha mapumziko cha angalau saa 60 mtawalia baada ya wiki mbili au kipindi cha mapumziko cha kila wiki kinaweza kupunguzwa hadi saa 8 ikiwa kipindi cha mapumziko katika wiki inayofuatia kimeongezwa kwa usawa.

Mfanyakazi atakapo fanya kazi kwa masaa matano mfululizo, atastahili kupewa muda wa kupumziki usio pungua saa moja. Mwajiri anaweza kumtaka mfanya kazi kufanya kazi wakati wa saa ya mapumziko, endapo kazi husika haiwezi kusubiri au kufanywa na mfanya kazi mwingineyeyo.

Sheria inatoa kipindi cha mapumziko kisicho pungua masaa 12 mfululizo kati ya kumaliza juma na kabla ya kuanza juma jipya la kazi. Kipindi hiki cha mapumziko, kinaweza kupunguzwa hadi masaa 8 endapo yapo makubaliano ya kimaandishi, au endapo masaa ya kazi ya kawaida yana athiriwa na kipindi cha walau masaa matatu au endapo mfanyakazi anaishi ndani ya eneo la kazi.

Hata hivyo, sehemu ya mapumziko ya kila siku nay ale ya mwishoni wa juma haitahusika kwa wafanyakazi wenye hadhi ya umaneja au wale wanaofanya kazi za dharura.

Chanzo: Sehemu ya 17, 23 (1 & 2) na 24 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Taratibu juu ya Kazi na Sikukuu

  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Sheria ya sikukuu za kitaifa, 1966 / Public Holidays Ordinance, 1966
Loading...