Makubaliano ya Pamoja

fahamu kuhusu makubaliano ya pamoja kama ilivyoelezewa katika sheria ya ajira na mahusiano ya kazi ya mwaka 2004, pata yote haya katika mywage.org/tanzania

Ni nini makubaliano ya pamoja?

Makubaliano ya pamoja ni makubaliano ya maandishi juu ya masuala ya ajira kati ya chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa na mwajiri au chama cha Waajiri kilichosajiliwa. Hivyo inamaanisha  mwajiri hawezi kufanya makubaliano ya pamoja na kikundi cha wafanyakazi au mfanyakazi mmoja.
Makubaliano ya pamoja yanakusudia  kuboresha masuala ya ajira na kazi kama yalivyopangwa chini ya sheria na mikataba ya ajira. Sheria inatoa viwango vya chini lakini vinaweza kuboreshwa kupitia makubaliano ya pamoja. Maridhiano ya makubaliano Na 87 juu ya Uhuru wa kuungana na ulinzi wa haki kwa kiasi kikubwa imepelekea kuwapo kwa kipengele kizima cha VI juu ya Makubaliano ya Pamoja katika Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 na Kanuni za Utendaji bora za mwaka 2007. 

Je sheria inamruhusu mwajiri kufikia makubaliano ya pamoja tofauti na vyama viwili vya wafanyakazi?

Hapana! Chama cha wafanyakazi ambacho kinauwakilishi mkubwa wa wafanyakazi  ndo chombo sahihi cha majadiliano na lazima kitambulike kama wakala pekee wa majadiliano na ndio wenye haki ya kutia saini makubaliano ya pamoja na mwajiri kuwakilisha wafanyakazi katika majadiliano. 

Ni masuala gani yanaweza kujadiliwa na kuafikiwa katika makubaliano ya pamoja?

Kipengele cha 68 cha Sheria ya Ajira na mahusiano ya kazi, 2004 inaeleza kwamba “suala lolote la kazi” linaweza kujadiliwa wakati kipengele cha 4 cha sheria kinatoa ufafanuzi wa masuala ya kazi  “kama suala lolote linalohusiana na ajira au mahusiano ya kazi”. Kanuni ya 55 inaeleza masuala ya kujadiliana ni pamoja na:
•    Ujira, mishahara na aina nyingine za tunzo;
•    Masharti ya ajira;
•    Posho na maslahi ya ajira;
•    Sera na taratibu za ajira zinazohusu kuajiri, uteuzi, mafunzo, uhamisho, kupandisha cheo, kusimamisha kazi, nidhamu na kuwaachisha kazi wafanyakazi;
•    Masuala ya afya na mafao
•    Masuala yahusuyo Haki za Shirika, majadiliano na mgogoro;
•    Taratibu za kutoa malalamiko, nidhamu na kuachisha kazi.
•    Mambo yoyote yaliyokubaliwa.
Masharti ya ajira yatajumuisha masharti yalioelezwa au yaliyoonyeshwa kwenye mkataba wa ajira kama vile saa za kazi, likizo, muda wa kutoa taarifa. Masharti kwa kawaida yanayohusiana na ajira kama vile kanuni zinazoongoza tabia mahali pa kazi, suhula za kantini, afya na usalama.
Mambo mengine yaliyoelezwa hapo juu yanaweza kuwamo katika sera na makubaliano ya pamoja yatajaribu kuboresha. 

Mimi si mwanachama wa chama cha wafanyakazi je makubaliano ya pamoja yatanifunga na mimi?

Ndio! Kwa kuzingatia ni muhusika wa chombo cha majadiliano ambao unawakilishwa katika makubaliano ya pamoja hivyo utafungwa na masharti ya makubaliano kwa kua chama cha wafanyakazi kinajulikana kama wakala wa pekee wa majadiliano ya wafanyakazi.
Chama cha wafanyakazi kinachowakilisha wanachama wengi kinaweza kufikia makubaliano ya pamoja yanayotoa duka la uwakala. Duka la uwakala ni mpango wa usalama wa chama ambao wafanyakazi katika chombo cha majadiliano ambao si wajumbe wa chama cha wafanyakazi kinachotambulika wanatakiwa kulipa ada ya wakala kwenye chama cha wafanyakazi. Hitaji hili ni kwa ajili ya kuwapata wafanyakazi katika chombo cha majadiliano ( ijapokua si wajumbe wa chama cha wafanyakazi) kuchangia kwa sababu mara zote wananufaika kwa kile ambacho kinajadiliwa na chama cha wafanyakazi. Kiasi kinachohitajika kulipwa kitajadiliwa baina ya chama cha wafanyakazi kinachotambulika na mwajiri, lakini haitakiwi kua zaidi ya ada inayolipwa na wanachama wa chama cha wafanyakazi. Ada hii hutumika kukuza au kulinda maslahi ya kijamii na kiuchumi ya mfanyakazi katika mahali pa kazi. 

Ni upi utaratibu wa kufikia makubaliano ya pamoja?

Baada ya kua ndio mwakilishi mkubwa wa wafanyakazi ni lazima umfahamishe mwajiri au chama cha Waajiri kwa kupitia fomu maalumu kwamba unahitaji utambulisho kama wakala wa pekee wa majadiliano katika chombo cha majadiliano.
Ndani ya siku 30 toka kupokea taarifa, mwajiri atahitajika kukutana na wawakilishi wa chama cha wafanyakazi kuweza kufikia makubaliano ya utambulisho wa chama cha wafanyakazi. Baada ya kufikia makubaliano ya utambulisho upande wowote unaweza kuanzisha pendekezo la kua na makubaliano ya pamoja. 

Ni nini kitatokea kama mwajiri atakataa kukubaliana na makubaliano ya pamoja?

Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, 2004 inaeleza kwamba panapokua hakuna makubaliano au mwajiri kashindwa kukutana na chama cha wafanyakazi ndani ya siku 30 zilizotolewa chama cha wafanyakazi kinaweza kupeleka mgogoro kwenye Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA). Kama usuluhishi utashindwa upande wowote unaweza kupeleka mgogoro Mahakama ya Kazi kwa maamuzi.

Ni wapi pa kupeleka mgogoro unaohusiana na makubaliano ya pamoja?

Mgogoro unaohusiana na matumizi, tafsiri au utekelezaji wa makubaliano ya pamoja utapelekwa kweney Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA). Kama usuluhishi hautazaa matunda basi upande wowote utapeleka suala Mahakama ya Kazi kwa maamuzi.

Loading...