Likizo ya uzazi kwa Mwanaume/ baba
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004 inatoa likizo ya malipo ya uzazi kwa baba kwa angalau siku 3 (katika kipindi cha likizo cha miezi 12) kwa baba mgebi ikiwa likizi hii itachukuliwa katika siku 7 za kuzaliwa kwa mtoto.
Mwajiri anaweza kuhitaji uthibitishaji usio na shaka wa kuzaliwa kwa mtoto kabla ya kulipia likizo ya uzazi kwa baba. Mfanyakazi lazima awe ameajiriwa na mwajiri husika kwa kipindi kisicho pungua miezi sita katika miezi 12 kabla ya kuzaliwa mtoto au awe ameajiriwa kwa mkataba wa kazi maalumu na mwajiri husika.
Chanzo: § ya 34 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004; ISSA Nchi ya Tanzania, 2017