Usawa Mahali pa kazi

This page was last updated on: 2023-05-21

Usawa wa malipo

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, watu wote wanazaliwa sawa na wapo sawa mbele ya Sheria. Katiba pia inatambua haki ya kufanya kazi na haki ya mapato sawa. Watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wanalipwa kulingana na kiwango na uwezo wa kazi. Aidha Katiba inatambua haki ya kupata kazi na haki ya kupata malipo stahiki.

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004 pia inamtaka kila mwajiri kuhakikisha kuwa wanaume kwa wanawake aliowaajiri wanapata malipo sawa kwa kazi zenye thamani sawa wazifanyazo.

Chanzo: §12-13 & 23 ya Katiba ya Tanzania; §7(10) Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004

Kutokubagua

Kwa mujibu wa Katiba, kubagua kunamaanisha kuridhisha mahitaji, haki au mahitaji mengine ya watu tofauti kwa misingi ya kitaifa, lugha, asili, mwelekeo wa siasa, rangi, dini, jinsiaa au hadhi maishani hadi kitengo fulani cha watu kinachukuliwa kama hakina nguvu na wanapewa vikwazo au hali wakati watu wa vitengo vingine wanachukuliwa tofauti au wanapewa nafasi au manufaa nje ya hali zilizobainishwa au uwezo uliotolewa isipokuwa ya kwamba neno “kubagua” halitatfsiriwa katika njia ambayo itazuia Serikali kuchukua hatua za maana za kutatua ulemavu katika jamii.

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini , 2004 pia inakataza ubaguzi, wa moja kwa moja au usio dhahiri, dhidi ya mfanyakazi katika sera yoyote ya ajira kwa misingi ya rangi, utaifa, mahali pa kuzaliwa, jinsia, ujauzito, hali ya kuoa au kutooa, asili ya mtu, mwelekeo wa kisiasa, ulemavu au UKIMWI, umri au Nyanja ya maisha. Haita chukuliwa kama ubaguzi pale ambapo hatua madhubuti za kusaidia kukuza ajira kwa kundi lilio sahauliwa au ambalo limekuwa likibaguliwa kwa muda mrefu katika soko la ajira; kama vile kupendelea, kutenga au kuchagua mtu yeyote kwa minajili hii ya kazi, au kuajiri wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira 1999.  Mtu yeyote atakaye vunja sehemu hizi anakosea. Ikiwa atahukumiwa, mtu kama huyu atawajibika kulipa faini isiyo zidi shilingi milioni tano za Tanzania.

Source: §13 ya Katiba ya Tanzania, § 7 & 102 (3) ya Sheria ya Huduma ya Ukuzaji Ajira wa Kitaifa 

Haki ya Kufanya Kazi

Wanawake wanaweza kufanya kazi katika kiwanda kimoja na wanaume. Hakuna sheria inayokataza hili.

Taratibu juu ya Usawa Mahali pa kazi

  • Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004 / Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004
  • Kanuni za adhabu, 1945 / The Penal Code, 1945
  • Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (imefanyiwa marekebisho mwaka 1995) / The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 (amended in 2005)
Loading...