Saa za Kazi na saa za ziada

Kutokana na sheria za kazi za Tanzania, muda wa saa za kazi ni saa nane kwa siku na saa 48 kwa wiki na ukijumlisha na saa za chakula na kuomba au shughuli za kidini zinatakiwi zisizidi saa 9 kwa siku.

Je Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasemaje kuhusu muda wa kazi?

Katiba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) iliyokubaliwa mwaka 1919, inazingatia uboreshaji katika mazingira ya kazi hususani kanuni za muda wa kazi ikiwa ni pamoja na kuwepo na kikomo cha muda wa kufanya kazi kwa siku na kwa wiki ili kuwepo na amani na utulivu duniani. Amani ya kudumu duniani inajengwa na kuwapo kwa haki katika jamii na ni kupitia uboreshaji wa mazingira ya kazi zetu za kila siku.
Kutokana na ripoti ya ILO muda wa kufanya kazi umekua suala nyeti katika mazingira ya kazi mwanzoni mwa mapinduzi ya viwanda  na kupelekea kua sera ya msingi ya kazi toka kupitishwa kwa sheria ya viwanda ya mwaka 1844 na United Kingdom. Sheria hii iliweka mipaka ya muda wa kazi kwa wanawake na watoto pekee.
Kudhibiti muda wa kazi ni jukumu kubwa na la mwanzo kabisa la sheria za kazi. Kwa kuelewa umuhimu wake, ILO ilipitisha azimio lake la kwanza mwaka 1919 ambayo iliweka mipaka ya saa za kazi ( saa 8 kwa siku na 48 kwa wiki). Azimio hilo pia linaeleza juu ya muda wa mapumziko ( kwa siku na kwa wiki).
Kutokana na maazimio namba 1 na 30 ya ILO kiwango cha saa za kazi kwa kawaida hakitakiwi kuzidi saa 48 kwa wiki na saa 8 kwa siku. Azimio namba 1 linatumika kwa shughuli za viwanda ambazo ni pamoja na migodi, uchimbaji na shughuli nyingine za uchimbaji wa madini, ujenzi, urekebishaji wa majengo, reli, wawekaji wa nyaya za simu, kazi za gesi, huduma za usafirishaji n.k. Kwa upande mwingine, azimio namba 30 linahusu wafanyakazi katika sekta ya biashara na shughuli za kiutawala ( kazi za maofisini)

Je ILO inaunga mkono saa 40 za kazi kwa wiki kama zinavyotumika katika  nchi nyingi za Ulaya?
Ndio, Shirika la Kazi Duniani (ILO) linaunga mkono mpango huu wa kupunguza saa za kazi. Kipindi cha mtikisiko wa uchumi duniani, ILO ilipitisha azimio jingine ambalo lilitaka kupunguzwa kwa saa za kazi ( kua saa 40 kwa wiki) ilikusaidia mishahara na kiwango cha maisha cha wafanyakazi kutoathirika vibaya katika mtikisiko wa uchumi. Ni vizuri ikatambulika kwamba azimio hili lilithibitishwa kwa kiasi kikubwa na nchi za Ulaya na nchi za Urusi ya zamani ( kwa ujumla hadi sasa kuna nchi 15 tu zilizothibitisha)
Hatua ya kupunguza saa za kazi zinachukuliwa pia kama hatua bora za kupunguza ukosefu wa ajira na kazi katika uchumi.

Je Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasemaje kuhusu kufanya kazi kwa taarifa ya muda  mfupi?

Kufanya kazi kwa taarifa ya muda mfupi kwa kawaida hutambulika kama kazi zisizokua na ulinzi, za muda mfupi na kazi zisizokua rasmi. Hakuna azimio au chombo maalumu cha ILO kinacholinda maslahi ya wafanyakazi wanaofanya kazi za aina hizi. Maendeleo ya utandawazi yamepelekea kuongezeka kwa ajira zisizokua rasmi. Ajira za muda mfupi ni asilimia 15% ya jumla ya ajira zinazolipa katika Umoja wa Ulaya (EU) na asilimia 12% ya jumla ya ajira zinazolipa kwa nchi za OECD.

Kutokana na ILO, “vibarua ni wale wafanyakazi ambao wanaitwa kazini pale tu wanapohitajika”. Hivyo saa za kazi za vibarua zinapishana na zinategemea na ukubwa wa kazi.Zaidi ya hayo pia mkataba wa kazi unaweza kuonyesha muda wa chini na wa juu kabisa wa kazi, ijapokua kama mkataba hauonyeshi muda wa chini wa saa za kazi basi mkataba huo huitwa mkataba wa saa sifuri.

Kazi za muda mfupi au vibarua zinaweza kuonekana kama zina faida kwa mwajiri         ( kufikia mahitaji yake ya msimu, kujaza nafasi kwa muda mfupi na hakuna gharama za ziada) na wafanyakazi ( hususan vijana na wafanyakazi wanafunzi ambao utaratibu huo unawapa fursa ya kuingia katika soko la ajira) ijapokua wafanyakazi wa aina hii huzalisha kidogo, kuacha kazi kwa wingi, ulinzi mdogo wa kazi na hisia za kutoridhishwa na kazi na hakuna mafao kama pensheni au likizo yenye malipo.
Kazi za aina hii zimetokea kwa sana katika miongo miwili au mitatu iliyopita wakati maazimio mengi ya ILO yalipitishwa kabla ya muda huo. Hii ndo sababu kwamba hakuna azimio lolote la ILO linaloelezea kazi za muda mfupi (vibarua). Hatahivyo kamati ya wataalamu wa ILO imerejea muda na vile vile maazimio ya ILO na mapendekezo yana matumizi ya jumla labda kama imeelezwa tofauti. Hivyo tunasema vibarua wana haki zote alizonazo mfanyakazi wa kawaida.

Vipindi vya mapumziko na chakula cha mchana

Je Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasemaje kuhusu vipindi vya mapumziko?

Maazimio ya ILO hayaelezi kwa uwazi muda wa mapumziko wakati wa saa za kazi, hatahivyo sheria za kazi za nchi kwa kawaida hueleza mapumziko haya ili kuweza kuwapo kwa afya na usalama na maisha bora ya wafanyakazi. Wafanyakazi wanahitaji mapumziko haya kwa ajili ya kupumzika, kupata mlo na shughuli za kidini. Katika nchi nyingi kipindi cha mapumziko hua hakilipwi kwasababu wafanyakazi hua hawapo kazini katika vipindi hivi. Hatahivyo, nchi nyingine zinahesabu muda huu wa mapumziko kama muda wa kazi. Jedwali hapo chini linaonyesha takwimu ya muda wa mapumziko na jumla ya saa za kazi zinazofuzu kupata mapumziko.

Nchi Kipindi cha mapumziko Jumla ya muda wa kufanya kazi *
Misri Angalau saa 1 kwa chakula na mapumziko

Kikomo cha kazi kwa siku : Saa 8

Kipindi cha mapumziko kabla ya kumaliza saa 8 za kazi

Guatemala Angalau dakika 30 za mapumziko zenye malipo

Kikomo cha kazi kwa siku: saa 8

Kipindi cha mapumziko kabla ya kumaliza saa 8 za kazi

India Mapumziko ya dakika 30 Baada ya kumaliza saa 5 za kazi
Indonesia Angalau mapumziko ya dakika 30 Baada ya kumaliza saa 4 mfululizo za kazi
Kenya Hakuna maelezo juu ya muda wa mapumziko
Msumbiji Kipindi cha muda wa kupumzika kati ya dakika 30 hadi saa 2 Baada ya kumaliza saa 5 mfululizo za kazi
Pakistani Dakika 30 hadi saa 1 Dakika 30 baada ya kumaliza saa 5 za kazi; saa 1 ya kupumzika baada ya saa 6 za kazi
Paraguay Angalau dakika 30 Baada ya kumaliza saa 4 za kazi
Peru Angalau dakika 45 Katika kipindi cha saa 8
South Africa Saa 1 Baada ya kumaliza saa 5 za kazi
* Muda wa kufuzu kwa mfanyakazi kupata muda wa mapumziko

Kufanya kazi usiku

Je Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasemaje kuhusu kufanya kazi jioni, usiku na asubuhi na mapema?

Kutokana na azimio la 171 la ILO, kazi za usiku “kazi zote zinazofanywa katika kipindi kisichopungua saa saba mfululizo ikiwa ni pamoja na kipindi kutoka saa sita za usiku mpaka saa kumi na moja asubuhi”. Kipindi hiki na kikomo cha muda kilichoelezwa kinapangwa na taasisi husika za ajira ( katika nchi) baada ya majadiliano na Waajiri na wafanyakazi katika kampuni.

Kwa kuelewa ukweli kwamba kazi za usiku zina madhara kwa afya ya mfanyakazi, azimio hapo juu la ILO linahitaji hatua zichukuliwe katika

i.     Kulinda afya ya mfanyakazi
ii.     Kulipa fidia kama ipasavyo ( fidia ya kufanya kazi usiku)
iii.     Kutoa fursa ya kuendelea kikazi (kupanda cheo)
iv.    Kuhakikisha usalama wao na kulinda haki za wajawazito na wazazi

Sheria za kazi za nchi huko Pakistani zinakataza kazi za usiku kwa wanawake. Sera hii ilikua sambamba na azimio la 89 la ILO, ambalo linakataza kazi za usiku kwa wanawake. Hatahivyo, azimio hili lilikosolewa kwa kua linabagua wanawake kwa kuwazuia fursa za ajira hasa katika sekta ya viwanda, ambayo huajiri wafanyakazi wengi kwa kazi za usiku. Idadi kubwa ya wafanyakazi wa usiku siku hizi wanaajiriwa na sekta ya huduma.

Katika kuitikia wito wa makosa yaliyotolewa dhidi ya azimio la 89, azimo jipya (Na. 171) lilipitishwa mwaka 1990 ambapo ilitumia njia isiyoonyesha jinsia na haikatazi kazi za usiku kwa wanawake.

Kuna faida na hasara zinazotokana na kazi za usiku. Kama inavyoonekana kua na faida kwa mwajiri ( kuna matumizi sahihi ya mashine na vifaa vingine kwa uzalishaji mkubwa) na mfanyakazi ( malipo makubwa kama fidia ya kufanya kazi usiku itatolewa) katika upande mmoja wakati kwa upande mwingine ina athari hasi kwa wafanyakazi na Waajiri. Kwa wafanyakazi, kukosa muda wa kulala wa kutosha una athari katika utendaji kazi wa mfanyakazi na kuna hatari ya ajali zitokanazo na kazi na magonjwa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya homa za matumbo na magonjwa ya moyo. Pia kuna hatari kubwa ya kupata kansa ya matiti kwa wanawake wanaofanya kazi za usiku. Vile vile kwa mwajiri, kazi za usiku zinaongeza gharama za utawala katika kulipa fidia wafanyakazi wanapopata ajali na magonjwa.

Wanawake na saa za kazi zisizo za kawaida

Je wanawake wanalindwa na kazi za usiku?

Azimio la 171 la ILO linaongelea juu ya haki ya ulinzi kwa wajawazito na wazazi wanaofanya kazi za usiku. Azimio hili linaeleza kwamba mfanyakazi mjamzito apewe kazi mbadala na kazi za usiku kabla na bada ya kujifungua kwa kipindi cha angalau wiki 16 ambazo angalau wiki 8 zitakua kabla ya tarehe anayotegemea kujifungua. Kipingi hiki cha msamaha wa kazi za usiku (wiki 16) kinaweza kuongezwa kama cheti cha daktari kitatolewa kikisema kua kazi za usiku zinaweza kua hatari kwa afya ya mama au mtoto. Katika kipindi hiki mfanyakazi mwanamke hawezi kufutwa kazi au kupewa notisi ya kufutwa kazi isipokua kwa sababu ambayo haihusiani na ujauzito au mtoto.



Marejeo
Azimio la Saa za Kazi (Viwanda), 1919; Azimio la Saa za Kazi ( Biashara na maofisi), 1930;Azimio la saa 40 za kazi kwa wiki,1935; Azimio la kazi za usiku, 1990

Benki ya taarifa ya ILO juu ya hali za kazi na ajira

“Sera na Kanuni ya kupambana na ajira zisizokua rasmi”, imechapishwa na ILO

“Saa za kazi zenye staha”, imechapishwa na ILO

“ Mikataba ya saa sifuri na kuitwa kazini katika kipindi cha muda mfupi”, imechapishwa na ILO

“Kazi za Usiku”, imechapishwa na ILO

Soma zaidi:

Likizo ya mwaka

Likizo ya uzazi/ulezi

Loading...