Kujiandaa na Usahili

fahamu yote kuhusu kujiandaa na usahili na kupata kazi katika mywage.org/tanzania, na mengine mengi juu ya kufungua biashara yako na kuandika CV bomba pamoja mishahara na masuala ya kazi na ajira

Hongera! Umeitwa kwenye usahili wa kazi, hakikisha uko tayari.


Maandalizi

Jiandae kwa kufanya utafiti wa sekta au kampuni uliyoitwa kwa ajili ya usahili wa kazi

( tovuti, vipeperushi na vijarida ni vyanzo vizuri vya habari)

Jiandae kwa maswali. Waajiri wanatumia maswali ya jumla kama vile “ Ni upi ubora wako na udhaifu wako?” na “ kuna waombaji 10, kwanini tukuchague wewe?”. Orodhesha maswali yanayoweza kuulizwa na muombe rafiki au jamaa yako mfanye mazoezi kwa kukuuliza maswali hayo. Epuka majibu yenye silabi moja, kwa mfano ukiulizwa kama unajali muda, usijibu “NDIO” pekee, jaribu kuelezea kuthibitisha jibu lako, kama vile “Ndio, hata marafiki zangu nawakera kwa sababu mimi huwahi angalau dakika 10 kila tunapokua na miadi”. Wakati wa usahili kua tayari na maswali usiyoyategemea au ambayo hukujiandaa nayo. Kitu cha muhimu ni kua mkweli, usiigize na kua mtulivu.

Andaa maswali yako mwenyewe. Unapoulizwa kama unaswali lolote la kuuliza, panga swali lako katika mpangilio ambao utaonyesha una ufahamu na shughuli za kampuni au kiwanda husika. Mpangilio unaweza ukawa, “ Ninafahamu kwamba….”. Pia unaweza kuuliza zaidi juu ya aina ya utawala wa kampuni ama mipango ya kupanuka siku za mbeleni. Vile vile unahitaji kujua ni kitu gani wanategemea kutoka kwako.


Njia ya pande mbili
Katika usahili kila upande una nafasi ya kupata utakacho. Ni muhimu kutambua kua usahili ni jambo la ushirika wa pande mbili. Anaekusahili anaweza kua mwongozaji lakini pia anahitaji maelezo yako. Kupata kwako ni kwa kuuliza maswali ambayo yatakusaidia kufanya maamuzi fasaha.

Uliza maswali haya ( kama hayajaongelewa katika usahili):

 

  • Ni nini utahitajika kufanya? Ni kitu gani kinategemewa katika nafasi hii?
  • Vipi kuhusu kazi fulani fulani na muda utakaotumika katika utekelezaji wake?
  • Ni sifa zipi wanazihitaji kwa mtu wa nafasi hii?
  • Uliza pia kuhusu muda wa kawaida wa kufanya kazi na masharti pindi inapotokea kufanya kazi muda wa ziada.
  • Je hii ni kazi mpya? Ni kwa kiwango gani inafaa katika muundo wa idara au kampuni?
  • Uliza kuhusu njia za ukuwaji ndani ya kampuni. Pia usisahau kuuliza kuhusu fursa za kukua kikazi na kupanda cheo. Usipouliza maswali kama haya msahili anaweza kudhani hauna malengo ya kukua katika kazi ama kupanda cheo.

 

  • Je kampuni inatoa mafunzo wakati wa kazi au hata nje ya kazi?
  • Ni kwa namna gani utakua unapimwa utendaji wako wa kazi? Je vipimo hivi vinaendana na kuongwezwa mshahara au cheo?
  • Uliza kuhusu mshahara kama una uhakika wewe ni mshindani mwenye nguvu katika kazi hiyo na kama msahili hajataja kuhusu mshahara. Ni vizuri kumwacha mwajiri ataje mshahara aliopanga kwa nafasi hiyo. Hii ni kwa sababu kiwango cha mwajiri kinaweza kua kikubwa kuliko kiwango utakachotaja wewe. Kama mwajiri hatozungumza chochote kuhusu mshahara, mwisho wa usahili unaweza kuulizia kuhusu kiwango cha mshahara.
  • Mwisho wa usahili uliza utarajie kitu gani, hatua zinazofuata na kwa wakati gani?


Epuka kuuliza maswali kama haya:

  • Maswali yanayoonekana kama vile unamfanyia usahili msahili. Weka maswali yako katika namna ya kutaka kujua kuhusu kampuni na kazi na sio kumuhusu mtu anaekusahili.
  • Maswali binafsi kuhusu taarifa za elimu au kazi ya mtu anaekusahili. Hapa ndipo usahili unapokua ni mawasiliano ya njia moja kwani msahili anaweza kukuuliza kuhusu elimu yako.
  • Maswali ambayo yanaweza kumuweka msahili njia panda, kama vile vipengele vizuri au vibaya vya kazi? Je idara yake inachukuliwa kama idara bora? Je yeye ni bosi mzuri?

 

  • “Wewe unafanya kazi gani hapa?” Hili ni moja ya maswali ambayo yanaweza kumuudhi msahili. Ni vizuri ukafanya utafiti wewe mwenyewe.
  • Maswali yanayoonyesha kama vile umeshapata kazi, kama vile ni lipi eneo langu la kazi?
  • Maswali kuhusu marupupu – usiulize katika kipindi hiki cha usahili. Una haki zote za kufahamu kuhusu haya lakini subiri mpaka utakapoitwa kwa ajili ya kazi.

Soma zaidi

Fahamu zaidi kuhusu masuala ya kazi na sheria za kazi

Loading...