Uzazi na Kazi

This page was last updated on: 2023-05-18

Likizo ya Uzazi

Kwa ujumla, wafanyakazi wana haki ya miezi 03 (wiki 13) ya livu ya uzazi. Livu ya lazima ni wiki 10 (wiki 4 kabla na wiki 6 baada ya kujifungua). Katika hali ya kujifungua mara kadhaa, livu ya uzazi huongezwa hadi siku 100. Mfanyakazi mwanamke anaweza kuchukua livu ya uzazi kama livu ya kulipwa mara moja kila miaka 03. Hata hiyo, katika hali ya mimba kuharibika au kifo cha mtoto wakati wa livu ya uzazi, livu hii hukatizwa baada ya wiki sita ya kujifungua au mimba kuharibika. Ikiwa ni mfanyakazi mwanamke, ambaye livu yake ya uzazi ilikatizwa kwa misingi ya mimba kuharibika au kifo cha mtoto, apate mimba tena kabla ya kukamilisha miaka 03 kuanzia tarehe ya kujifungua kwake kwa kwanza, anastahiki livu kamili ya uzazi ya miezi 03. 

Mfanyakazi amehakikishiwa pia haki ya kutokuwepo kazini bila kupoteza malipo kwa kuhudhuria vipimo vya kabla na baada ya kujifungua.

Huenda mfanyakazi wa kudumu akapewa pia livu bila malipo kwa kipindi kisichozidisha miezi 03 ikiwa atajifungua kabla ya kukamilika kwa mwaka mmoja wa huduma. 

(§ 70 and 71.1.a ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005) 

Mshahara

Wakati wa kipindi cha livu ya uzazi (miezi 03 kwa visa vya kawaida; siku 100 kwa kujifungua mara kadhaa), wafanyakazi hulipwa malipo yao kamili na hata pia faida zingine kama vile faida ya uzazi.

Wafanyakazi pia wana haki ya faida ya uzazi chini ya Sheria ya Ruzuku ya Serikali. Faida hii inapatikana kwa wafanyakazi wanawake mara moja kila miaka mitatu. Kiwango cha juu ambacho kinaweza kuchukuliwa ni limbikizo la michango kwa 3% ya mapato yenye bima na faida. Kiwango cha mchango ni 15% (10% kutoka kwa mwajiri na 05% kutoka kwa mfanyakazi)

chanzo: §70 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005; §26, 29 na Ratiba 01 ya Sheria ya Ruzuku ya Serikali ya 2005

Huduma ya bure ya matibabu

Sheria ya Hazina ya Ruzuku ya Serikali ya Zanzibari 2005 inatoa faida za huduma ya matibabu. Mfanyakazi anahitajika kusajili wafanyakazi wote ndani ya siku kumi na nne ya kuanza ajira na Hazina ya Ruzuku ya Serikali. Kwa faida za huduma ya matibabu, kizuizi kimewekwa katika sheria. Kiwango cha juu ambacho kinaweza kuchukuliwa ni limbikizo la michango kwa 3% ya mapato yenye bima na faida. Kiwango cha mchango ni 15% (10% kutoka kwa mwajiri na 05% kutoka kwa mfanyakazi)

chanzo: §26, 29 na Ratiba 01 ya Sheria ya Hazina ya Ruzuku ya Serikali ya Zanzibari 2005

Loading...