Ulemavu / Fao la kuumia kazini

Ulemavu /Fao la kuumia kazini

Majeraha ya kikazi yamegawanywa katika kategoria nne: (i) ulemavu wa kudumu kabisa (11) ulemavu nusu wa kudumu (iii) ulemavu wa muda na (iv) jeraha mbaya linalosababisha kifo kwa mfanyakazi.

Mwajiri anahitajika kumfidia mfanyakazi ikiwa mfanyakazi ataumia kwa bahati mbaya akiwa kazini. Hata hivyo, mwajiri hana jukumu lolote la kulipa ikiwa itathibitishwa kwamba jeraha kwa mfanyakazi limetokana na makosa ya mfanyakazi. Licha ya hayo, hakuna fidia itakayolipwa kuhusiana na kutoweza kufanya kazi au kifo kinachotokana na kujijeruhi mwenywe.

Ulemavu wa muda huchukuliwa kama livu ya ugonjwa. Maelezo zaidi kuhusu haya yametolewa chini ya livu inayolipwa ya ugonjwa.

Katika hali ya ulemavu nusu wa kudumu, kiwango cha fidia ni sawa na asilimia ya kupoteza uwezo wa mapato unaothibitishwa na mtaalamu wa kimatibabu na kuzidishwa kwa miezi 48 ya mapato.

Katika hali ya ulemavu wa kudumu kabisa, kiwango cha fidia ni miezi 48 ya mapato au Shilingi milioni 05 yoyote ambayo iko juu.

Ikiwa mfanyakazi atafariki wakati wa kipindi cha ajira yake, na daktari athibitishe kwa kuandika kwamba kifo hicho kilisababishwa na sababu za kikazi, mwajiri wake anawajibika kwa gharama za mazishi za mfanyakazi marehemu, kuwafidia warithi wa mfanyakazi kulingana na matoleo ya Sheria ya Kuwafidia Wafanyakazi ya 1986, na pia kuwalipa warithi faida zozote za mkataba zilizolimbikizana za mfanyakazi marehemu. Lakini ikiwa kifo cha mfanyakazi aliyeaga hakijasababishwa na sababu zozote za kikazi, mwajiri anawajibika tu kwa theluthi moja ya gharama za mazishi ya marehemu, na kuwalipa warithi wa marehemu faida zozote za mkataba zilizolimbikizana za mfanyakazi marehemu kulingana na Sheria.

Katika hali ya kifo cha mfanyakazi, walioachwa/warithi hulipwa kima cha pesa sawa na malipo ya miezi 36. Ruzuku ya mazishi/gharama ya mazishi (ambayo haiwezi kuwa chini ya 33% ya gharama kwa jumla) hulipwa pia kwa walioachwa.

chanzo: § 69 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 of 2005; §4, 10, 11 & 12 ya Sheria ya Kuwafidia Wafanyakazi ya 1986, ilirekebishwa 2005

loading...
Loading...