Hifadhi ya Jamii

Haki ya Pensheni

Umri halali wa chini wa kustaafu ni miaka 60 (sawa na wafanyakazi wanawake). Pensheni ya uzee inapatikana kuanzia umri wa miaka 55, hata hivyo kwa kiwango kilichopunguzwa. Hakuna pensheni ya chini au ya juu. Lazima mfanyakazi awe amelipa michango yake kwa kipindi kisichopungua miezi 60. Wafanyakazi hao ambao wamelipa michango kwa chini ya miezi 60 hufidiwa michango yao pamoja na faida. Faida za uzee hujumuisha pensheni na bahashishi ya uzeeni. Pensheni ya uzeeni uhesabiwa kama wastani wa malipo ya miezi 60 iliyopita ikizidishwa na idadi ya miezi ya michango ikigawanywa na 30.

Pensheni kamili ni sawa na 3.33% ya wastani wa miaka tano ya mwisho ya mshahara kwa kila mwaka wa mchango. Pensheni ya kila mwezi ni theluthi mbili ya pensheni kamili kwa msingi wa kila mwezi. Bahashishi, malipo taslimu, ni sawa na theluthi moja ya pensheni kamili ikizidishwa mara 20. 

chanzo: §26, 29, 31 na Ratiba 01 ya Sheria ya Hazina ya Ruzuku ya Serikali ya Zanzibari 2005

Fao la Wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki

Sheria inatoa faida kwa waliosalia. Faida kwa Waliosalia hulipwa kwa Wakf na Tume ya Hazina (WTC kwa wanachama Waisilamu) au Msajili Mkuu (kwa wanachama wengine) ili kusambazwa kwa wanaofaidika. Ikiwa mfanyakazi amechangia hazina ya ruzuku ya serikali kwa angalau miezi 60, pensheni kamili ni sawa na 3.33% ya wastani wa miaka mitano ya mwisho ya mshahara kwa kila mwaka wa michango. Bahashishi, inayolipwa kama pesa taslimu, ni sawa na theluthi moja ya pensheni kamili ikizidishwa mara 20.

chanzo: §26, 29 na Ratiba 01 ya Sheria ya Hazina ya Ruzuku ya Serikali ya Zanzibari 2005

Fao la kuumia kazini na kutoweza kuendelea na Kazi

Ili kustahiki faida ya kutojiweza, aliye na bima lazima awe na umri mdogo kuliko umri wa kawaida wa kustaafu na kunastahili kuwa na ushahidi wa kimatibabu kuwa mfanyakazi hawezi kufanya kazi kabisa.

Hali za kuhitimu za faida za kutojiweza ni sawa na faida za uzeeni, i.e., angalau michango ya miezi 60. Pensheni kamili ni 3.33% ya wastani wa miaka 5 ya mwisho ya mshahara kwa kila mwaka wa mchango. Pensheni ya kutojiweza ya kila mwezi ni sawa na theluthi mbili ya pensheni kamili kwa msingi wa kila mwezi. Bahashishi ni sawa na theluthi moja ya pensheni kamili ikizidishwa mara 20.

chanzo: §26, 29 na Ratiba 01 ya Sheria ya Hazina ya Ruzuku ya Serikali ya Zanzibari 2005

loading...
Loading...