Kazi na Sikukuu

This page was last updated on: 2023-05-18

Likizo yenye malipo

Sheria ya Ajira hutoa siku 21 za kalenda (siku 07 kwa kila miezi 04 ya huduma) za livu ya kila mwaka baada ya mwaka mzima wa huduma. Wafanyakazi hulipwa mishahara yao kamili wakati wa livu yao ya kila mwaka. Hali ya kuhitimu ni kwamba lazima mfanyakazi awe amefanya kazi angalau miezi sita mwaka huo. Wafanyakazi wa muda maalum wanastahili livu ya kila mwaka kwa msingi wa uwiano.

Muda wa livu ya kila mwaka lazima ukubaliwe kati ya mfanyakazi na mwajiri. Huenda livu ya kila mwaka ikagawanywa kwa sehemu mbili bora sehemu hiyo iwe angalau livu ya wiki mbili za kufanya kazi bila kutatizwa na ipeanwe ndani ya mwaka mmoja wa kustahiki na salio ndani ya miezi 18 ya mwisho wa mwaka wa kustahiki. Makubaliano ya kuachilia livu ya kila mwaka au kuipuuza ili kufidiwa haitumiki. Hata hivyo, mfanyakazi anaweza kupokea fidia kwa livu yoyote ya kila mwaka isiyotumiwa mkataba wake wa ajira unapokatizwa.

chanzo: § 67 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

Malipo siku za mapumziko kitaifa

Wafanyakazi wana haki ya sikukuu zinazolipwa wakati wa sikukukuu (za umma na za kidini). Hizi zinajumuisha sikukuu za makumbusho na sikukuu za kidini (za Kikristro na Kiislamu). Sikukuu za Umma kwa kawaida huwa kumi na nne (14) kwa nambari. Siku hizi kuu ni Siku ya Mwaka Mpya (Januari 01), Siku ya Mapinduzi ya Zanzibari (Januari 12), Siku ya Maulid (Kuzaliwa kwa Nabii PBUH) , Ijumaa Kuu, Jumatatu ya Pasaka (Aprili 01), Siku ya Sheikh Abeid Amani Karume (Aprili 7), Siku ya Umoja (Aprili 26), Siku ya Wafanyakazi (Mei 01), Siku ya Wakulima (Agosti 08), Eid-el-Fitr (siku mbili, Eid-el-Hajj (siku moja), Siku ya Jamhuri (Desemba 09), na Siku ya Krisimasi (Novemba 25). Ikiwa sikukuu ya umma inaingiliana na siku ya kutofanya kazi au Jumapili, huwekwa siku hizo na haibadilishwi tena. Sikukuu za Waisilamu hulingana na kuonekana kwa mwezi na tarehe zake hubadilika kila mwaka. 

Siku ya Mapumziko ya juma

Kipindi cha kupumzika cha wiki hutolewa chini ya Sheria ya Ajira. Kila mfanyakazi ana haki ya kufurahia siku ya kupumzika kila wiki angalau kwa saa 24 mtawalia. Mfanyakazi hastahili kufanya kazi kwa zaidi ya siku sita mtawalia bila siku ya kupumzika.

chanzo: § 65 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

Loading...