Kazi na Ujira

This page was last updated on: 2023-05-18

Kima cha Chini cha Mshahara

Kulingana na matoleo ya Sheria ya Ajira, huenda mishahara ikawekwa kulingana na mkataba wa ajira, makubaliano ya pamoja na kupitia agizo la mshahara kutoka kwa Rais kulingana na mapendekezo ya Bodi ya Ushauri kuhusu Mishahara.  Bodi ya Ushauri kuhusu Mishahara in uwakilishi kutoka kwa washirika wote wahusika wa jamii, k.m., wafanyakazi, waajiri, serikali, waakilishi wa sekta isio rasmi na washauri wataalamu. Bodi hushauri serikali (Waziri wa Kazi) kuhusu mishahara na masuala mengine yanayohusu malipo ya mishahara na kipunguzo cha mishahara katika sekta ya umma na ya kibinafsi. Inaweza pia kushauri Waziri kuhusu kima cha chini cha mishahara na mapendekezo ya kuweka kima cha chini cha mishahara kwa wote au kikundi chochote cha waajiri Zanzibari. Wakati wa kuweka au kupendekeza mishahara, uwezo (wa waajiri) kulipa mishahara, gharama ya maisha nchini, na athari kwa ajira, upunguzaji umasikini na shughuli za biashara ndogo huzingatiwa. Kima cha chini cha mishahara kwa waajiri wa sekta ya umma na ya kibinafsi Zanzibari hutangazwa kupitia Agizo la Rais.

Hakuna mfanyakazi anayeweza kulipwa chini ya kima cha chini hata hivyo waajiri hawajapigwa marufuku dhidi ya kulipa zaidi ya kima cha chini cha mishahara kilichokubaliwa chini ya makubaliano ya pamoja au mkataba wa ajira wa kila mtu. Kima cha chini cha sasa cha mishahara Zanzibari ni shilingi 145, 000 kwa mwezi.

Ufikiano wa kima cha chini cha mishahara huthibitiwa na Wizara ya Kazi. Sheria ya Ajira nambari 11 ya 2005 inaweza kutumika katika uafikiano. 22.(1) Kamishna, mkaguzi wa ofisi ya kazi au Kazi aliye na idhini ya Mwendesha mashtaka atakuwa na uwezo wa kuanzisha utaratibu wa jinai mbele ya mahakama yeyote katika kushindiwa kutii na miongozo ya sheria iliyotolewa chini au uvunjaji wa sehemu yeyote ya Sheria hii au sheria zingine zozote za kazi. Kulingana na  106(4) Mwajiri anayelipa mapato chini ya viwango vilivyoagizwa na Waziri, atakuwa na hatia ya kosa na baada ya kuhukumiwa atalipa faini isiyo chini ya shilingi elfu mia nne au kifungo kisicho chini ya miezi mitatu. Mtu binafsi anaweza kulalamika kwa Wizara ya Kazi na Huduma za Umma ikiwa anafikiria anapokea chini ya kima cha chini cha mishahara.

chanzo: § 91-97 & 106 ya Ajira Sheria Nambari 11 ya 2005

Malipo ya kawaida

Sheria ya Ajira inahitaji kwamba malipo yalipwe katika pesa halali, k.m., Shilingi za Tanzania na makubaliano yoyote kinyume na hiyo huchukuliwa kuwa hayatumiki. Agizo la waziri linaweza kutoa malipo nusu ya mishahara hata hivyo sio katika njia ya vileo na dawa zenye madhara. Mishahara, iwe imelipwa kupitia pesa taslimu au cheki, lazima ilipwe wakati wa saa za kufanya kazi wakati wa siku za kufanya kazi na kazini. Kwa kawaida mishahara hulipwa kupitia pesa taslimu hata hivyo na kibali kutoka kwa mfanyakazi, huenda mishahara ikalipwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki iliyoteuliwa na mfanyakazi. Lazima mishahara ilipwe mfanyakazi mwenyewe na katika tukio la kifo cha mfanyakazi huyo, mwakilishi wa kisheria hulipwa mishahara na faida nyingine za kukatiziwa ajira.

Mwajiri anahitajika kulipa mishahara kwa wafanyakazi ikiwa mfanyakazi alikuwa kazini hata kama mwajiri alishindwa kumpa kazi kulingana na mkataba. Mfanyakazi, upande ule mwingine, hastahili mishahara kuhusiana na kipindi chochote ambacho hakuwa kazini bila sababu nzuri. Isipokuwa kuwe na makubaliano ya mapema yaliyoandikwa kati ya mfanyakazi na mwajiri, mfanyakazi anayefanya kazi kwa siku moja hulipwa mwisho wa siku hiyo; mfanyakazi anayefanya kazi kwa saa hulipwa mwisho wa saa, siku au wiki hiyo; mfanyakazi anayelipwa baada ya wiki mbili au mwezi hulipwa mwisho wa wiki hizo mbili au mwezi; na mfanyakazi anayefanya kazi kulingana na matokeo hulipwa kulingana na vipindi ambavyo havipiti wiki mbili.

Mfanyakazi hawezi kuwajibika kutumia maduka yoyote yaliyoanzishwa na mwajiri ili kutumiwa na wafanyazi wake au huduma zinazoendeshwa kulingana na kazi yake. Mkataba unapokatizwa, lazima mfanyakazi alipwe mishahara na malipo yoyote na faida zilizolimbikizana ambazo anastahili.

Vipunguzo kutoka kwa mishahara ya wafanyakazi haviruhusiwi isipokuwa vipunguzo hivi viwe vinahitajika au vinaruhusiwa kwa malipo fulani na mwajiri kwa niaba ya mfanyakazi ikiwa ni pamoja na ushuru au michango inayostahili kutoka kwa mfanyakazi hadi kwa hazina yoyote ya akiba, matibabu au pensheni au hazina yoyote iliyoidhinishwa; viwango vyovyote vilivyoagizwa na mahakama ili kutolewa moja kwa moja kwa mwenzi au jamaa yeyote anayemtegemea mfanyakazi; na michango inayostahili ya chama cha wafanyakazi.

Kipunguzo kinaweza pia kufanywa ili kufidia mfanyakazi kwa uharifibu ikiwa tu hasara au uharibifu huo ulifanyika wakati wa ajira na ulikuwa sababu ya mfanyakazi hata hivyo vipunguzo jumla havistahili kuzidisha robo moja (25%) ya mshahara wa mfanyakazi.

Waajiri wanahitajika kutoa risiti ya malipo kwa wafanyakazi inayoashiria kiwango na njia ambayo malipo yalihesabiwa; iashirie vipunguzo, lengo lake na malipo taslimu yaliyolipwa.

Kutolipa mishahara na vipunguzo visivyo halali kutoka kwa mishahara ni hatia inayoweza kuadhibiwa kwa faini au angalau shilingi 400,000 na kifungo cha angalau miezi mitatu (katika kesi ya vipunguzo visivyo halali tu).

chanzo: § 98-106 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

Loading...