Udhalilishaji kijinsia Mahali pa Kazi

Udhalilishaji kijinsia Mahali pa Kazi

Unyanyasaji wa kimapenzi ni aina yoyote ya tabia isiyohitajika ya kunena, isiyo ya kunena au ya kimwili ambayo ina umaana wa kingono (na ahadi ya moja kwa moja au ya kudokeza ya kupendelewa kwa ajira ya sasa ya ya usoni) ambayo, kwa hali yake au marudio, ina athari kwa ajira ya mwafanyakazi, utendakazi au kuridhishwa kikazi.

Sheria ya Ajira imepiga marufuku aina yoyote ya unyanyasaji wa kipamenzi wa mfanyakazi na mwajiri, mwakilishi wake au mtu yeyote yule.

Mhasiriwa wa unyanyasaji wa kimapenzi anaweza kulalamika kwa afisa wa kazi. Waajiri wote wanaoajiri zaidi ya wafanyakazi 25 wanahitajika kuwa na hatua zilizowekwa za kuzuia unyanyasaji wa kimapenzi katika mahali pa kazi. Waziri anaweza, kwa kuwasiliana na Bodi ya Ushauri wa Kazi, akatoa sheria maalum ya kuzuia unyanyasaji wa kimapenzi katika maeneo ya kazi yenye chini ya wafanyakazi 25.

Kwa kosa la kwanza, mtekelezaji wa unyanyasaji wa kimapenzi hupewa onyo. Kwa kosa la pili, mkataba wa ajira wa mtekelezaji hukatizwa.

chanzo: §11 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005 

loading...
Loading...