Hitaji la Notisi na Kiinua Mgongo

This page was last updated on: 2023-05-18

Hitaji la Notisi

Uhusiano wa ajiri hukatika wakati muda uliobainishwa unapokwisha (uliowekwa au wa muda maalum); kufikia umri wa kustaafu; kifo cha mfanyakazi; kifo cha mwajiri ikiwa biashara itakoma baada ya kifo chake; ulemavu wa kimatibabu uliyothibitishwa na bodi ya matibabu; tabia isiyokubaliwa au mfanyakazi kutofanya kazi vizuri; mfanyakazi kukataa kuhamishwa kutoka mahali pamoja hadi pengine; kukomeshwa kwa biashara baada ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ya mwajiri kufilisika au kufunga kazi. Sheria ya Ajira inahitaji kwamba kuwa na sababu nzuri ya kukatiza mkataba husika na (i) uwezo/ustadi wa mfanyakazi kufanya kazi; au tabia ya mfanyakazi mahali pa kazi; au kulingana na mahitaji ya kufanya kazi au huduma. Mwajiri anahitaji kumwarifu mfanyakazi kwa kuandika kuhusu uamuzi wa kupigwa kalamu, sababu za hatua hiyo na tarehe ambayo uamuzi huo utatekelezwa.

Kupigwa kalamu/kukatiziwa kazi huzingatiwa kuwa sio haki ikiwa msingi wake ni, kati ya mambo mengine, misingi ifuatayo: jamii, rangi, dini, jinsia, ndoa, majukumu ya kifamilia, ujauzito, maoni ya kisiasa, uhusiano wa kisiasa, asili ya kitaifa, jamii na mahali pa kuzaliwa; ulemavu au hali ya HIV/Ukimwi; livu ya uzazi, kutokuwepo kazini kwa muda kwa sababu ya ugonjwa; uhusiano na chama cha wafanyakazi; kutenda au kutafuta kutenda kama mwakilishi wa wafanyakazi; na kuhusika katika shughuli halali za chama cha wafanyakazi ikiwa ni pamoja na migomo.

 Katika tukio la kufutwa kazi bila haki, Mahakama ya Viwanda inaweza kuagiza urejeshewe au uhusishwe tena katika kazi uliokuwa ukifanya au upewe fidia. Agizo la kurejeshwa au kuhusishwa tena hutolewa baada ya kuzingatia matakwa ya mfanyakazi, hali zinazosababisha kufutwa kazi na mchango wa mfanyakazi kuwadia kufutwa kazi na usahihi wa agizo kama hilo. Huenda mahakama ikatoa pia fidia ambayo sio chini ya mshahara wa miezi sita.

  Kabla ya kukatiza mkataba wa ajira, mwajiri anahitajika kuzingatia kipindi kifuatacho cha ajira kulingana na urefu wa ajira ya mfanyakazi: angalau wiki 2 kwa miezi zaidi ya 06 lakini chini ya mwaka mmoja wa ajira; angalau mwezi 01 kwa zaidi ya mwaka 01 lakini chini ya miaka 05 ya ajira; na angalau miezi 03 kwa kipindi cha ajira cha miaka mitano au zaidi.

Vipindi hivyo pia vya notisi vinatumika ikiwa mfanyakazi atakatisha ajira. Hata hivyo, ikiwa mfanyakazi amekuwa na tabia isiyokubaliwa au kosa la jinai, hatakuwa na haki ya kipindi cha ilani.

chanzo: §52-54,111-112 & 118-120 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005 

Kiinua Mgongo

Ikiwa mfanyakazi atapatikana kuwa na hatia ya tabia isiyokubaliwa au kosa la jinai kabla ya muda wake uliowekwa kuisha, anaweza kufutwa kazi bila malipo au faida zozote za kukatizwa kazi (malipo ya kukatiziwa ajira) isipokuwa mgao wake wa mchango kwa pensheni au ruzuku ya serikali. (111.3)

Malipo ya Kukatiziwa kazi hutolewa tu iwapo mfanyakazi amefutwa kwa msingi wa kufukuzwa kazi (mahitaji ya kufanya kazi). Katika hali hiyo, mfanyakazi hupewa notisi ya miezi 03 au malipo badala ya notisi, malipo ya kukatiziwa kazi na  bahashishi. Malipo ya Kukatiziwa kazi nchini Zanzibari ni sawa na mshahara wa kawaida wa siku saba kwa kila mwaka uliokamilishwa wa huduma na mwajiri hadi miaka isiozidi 10. Kwa hivyo, malipo ya juu ya kukatiziwa kazi  ambayo mfanyakazi anaweza kupata ni mshahara wa kawaida wa siku 70. Huenda makubaliano ya pamoja yakatoa kiwango kikubwa kama malipo ya kukatiziwa kazi.  

chanzo: §111(3) & 121(6-8) ya Ajira Sheria Nambari 11 ya 2005

Loading...