Kazi na Kuugua

This page was last updated on: 2023-05-18

Likizo ya kuugua yenye malipo

Mwajiri anahitajika kumpa mfanyakazi livu ya ugonjwa ikiwa bodi ya matibabu imethibitisha kwamba mfanyakazi ni mgonjwa, amepata ajali, ameambukizwa maradhi yanayotokaka na au akiwa kazini na kwa hivyo hawezi kufanya kazi. Hata hivyo, sheria inatofautisha kati ya magonjwa/maradhi ya kawaida na maradhi ya kikazi (yanayotokana na au ukiwa kazini). Mfanyakazi ana haki ya kupata siku zifuatazo za ugonjwa ikiwa yeye ni mgonjwa kwa sababu ambazo hazihusiani na ajira: miezi miwili ya livu ya muda na malipo kamili; na livu ya ugonjwa ya miezi mitatu na malipo nusu (ikiwa bodi ya matibabu itahakikisha kwamba mfanyakazi hawezi bado kufanya kazi). Ikiwa baada ya miezi 05 kuisha, bado mfanyakazi haiwezi kufanya kazi, huenda mwajiri akakatiza mkataba wa ajira.

Katika hali magonjwa ya kikazi au hatari za kikazi, haki za livu ya ugonjwa ni kama ifuatavyo: Miezi 06 ya livu na mshahara kamili; miezi 03 ya livu ya ugonjwa na mshahara nusu (ikiwa bodi ya matibabu itathibitisha kwamba mfanyakazi hawezi bado kufanya kazi).  Ikiwa baada ya miezi 09 kuisha, bado mfanyakazi haiwezi kufanya kazi, huenda mwajiri akakatiza mkataba wa ajira.

Ikiwa mfanyakazi ni mgonjwa sana kufanya kazi kwa sababu ya HIV/Ukimwi, huenda mwajiri akakatiza kazi kwa sababu ya kutoweza kufanya kazi kama ilivyotolewa chini ya Sheria ya Ajira (kutoweza kufanya kazi ni moja ya misingi halali ya kusimamishwa kazi).

Ugonjwa wa mfanyakazi sio sababu nzuri ya kukatiza mkataba wa ajira na mfanyakazi haiwezi kusimamishwa kazi kwa sababu ya kutokuwepo kazini kwa sababu ya ugonjwa.

chanzo: § 60 & 69 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

Huduma ya matibabu

Faida za matibabu zinapatikana kwa wafanyakazi wenye bima na zinajumuisha huduma ya kawaida ya matibabu, huduma ya mtaalamu, dawa, kulazwa, na usafiri.

Sheria ya Kuwafidia Wafanyakazi inamlazimisha mwajiri kugharimia gharama alizopata mfanyakazi ndani ya Zanzibari au kwa idhini ya Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu, nje ya Zanzibari kama matokeo ya ajali inayotokana na kazi, gharama hizi zinahusiana na dawa, upasuaji na matibabu ya hospitali, huduma ya wauguzi wataalamu na utoaji wa dawa; utoaji wa udumishaji, ukaratabati na ubadilishaji wa viungo na vifaa bandia. 

Usalama wa kazi wakati wa kuugua

Ajira ya mfanyakazi ni dhabiti wakati wa ugonjwa na maradhi/ugonjwa hauwezi kivyake kuwa msingi wa kusimamishwa kazi. Katika hali ya ugonjwa wa kawaida, sheria inatoa kwamba ajira ya mfanyakazi iwe dhabiti kwa miezi 05 ya kwanza ya ugonjwa na katika hali ya maradhi ya kikazi, ajira iwe dhabiti wakati wa miezi 09 ya kwanza ya ugonjwa. Matoleo haya sio ya mwisho na makubaliano ya pamoja yanaweza kutoa vipindi virefu zaidi wakati ajira ya mfanyakazi mgonjwa nio dhabiti.

Mfanyakazi ambaye amekuwa akimfanyia kazi mwajiri kwa kipindi cha miezi sita anastahiki livu ya ugonjwa.

chanzo: § 69 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

 

Loading...