Afya na Usalama Mahali pa Kazi

This page was last updated on: 2023-05-18

Wajibu wa mwajiri

Mwajiri anastahili kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi. Inahitajika pia mwajiri kutekeleza biashara yake kwa njia ambayo inahakikisha kwamba hata wale wasio wafanyakazi ambao wanaathiriwa na shughuli hawako hatarini. Huenda eneo la kazi likaagizwa kufungwa kulingana na ushauri kutoka kwa mkaguzi wa usalama na afya (kwa kushauriana na afisa wa kazi) ikiwa kuna hatari yoyote iliyopo au inayowezekana kwa afya na usalama wa wafanyakazi.

chanzo: § 16.2 & 17.3 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005; §27-40 ya Sheria ya Usalama na Afya Kazini Nambari 08 ya 2005     

Kukingwa Bure

Utoaji na udumishaji wa vifaa vya kinga vya kibinafsi ni kazi ya mwajiri. Mwajiri anahitajika kutoa sare za kazi, mavazi maalum ya kinga na vifaa vingine vya kinga kwa wafanyakazi kwa gharama yake mwenyewe. Mavazi na vifaa kama hivyo vya kinga vitakuwa mali ya mwajiri.

Kulingana na Sheria ya OSH, vifaa vinavyofaa vya kinga lazima vitolewe na kudumishwa na mwajiri ili kutumiwa na wafanyakazi ikiwa wafanyakazi wameajiriwa katika shughuli yoyote inayoweza kusababisha majeraha au hali au mazingira makali. Ikiwa kazi inahusisha kutengeneza, kushughulika, kutumia au kuhifadhi nyenzo au vitu vyenye simu, huenda mwajiri akahitajika kutoa mavazi ya ziada ya kuwakinga wafanyakazi. Ikiwa hali inahitaji mfanyakazi kuingia katika maeneo yenye kolezo nzito ya vitu hatari, mwajiri anahitajika kuwajulisha wafanyakazi kuhusu hatari zote zilizopo na kuwapa wafanyakazi hawa vifaa vinavyofaa. 

chanzo: § 82 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005; § 36, 90.6.c na 96.6  ya Sheria ya Usalama na Afya Kazini Nambari 08 ya 2005

Mafunzo

Waajiri wanahitajika kuwafunza wafanyakazi kuhusu afya na usalama kazini, hasa kuhusiana na uzuiaji hatari mahsusi za kazi zingine. Kulingana na Sheria ya OSH, hakuna mtu anayeweza kuajiriwa kwenye mashine au mchakato wowote (ikiwa mchakato huo unaweza kusababisha majeraha kwa mwili au majeraha kwa afya), isipokuwa mfanyakazi huyo awe amefunzwa kabisa kuhusu hatari zinazoweza kutokea kuhusiana na mashine au mchakato. Lazima mfanyakazi apokee mafunzo ya kutosha kuhusu kutumia mashine au mchakato huo; lazima asimamiwe kabisa na mtu ambaye ana ufahamu na uzoefu wa kutosha wa mashine au mchakato. Ni jukumu la mwajiri kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wanaoathirika wameelekezwa kuhusu hatari zilizopo katika mahali pa kazi, hatua za usalama zimechukuliwa ili kuepuka majeraha, na kwamba mafunzo hayo yametolewa angalau mara moja kila miaka miwili.

chanzo: §68 ya Sheria ya Usalama na Afya Kazini Nambari 08 ya 2005

Mfumo wa Kukaguliwa na Mkaguzi wa Ajira

Mfumo wa ukaguzi wa kazi hutolewa chini ya Sheria ya Ajira na Sheria ya OSH. Jukumu kuu la ukaguzi wa kazi ni la Wizara ya Maendeleo ya Kazi, Vijana, Wanawake, na Watoto. Tume ya Kazi, ambayo hufanya kazi moja kwa moja chini ya Wizara ya Kazi, ina udhibiti wa moja kwa moja wa masuala ya ukaguzi wa kazi wakati shughuli ya OSH inatekelezwa na Wasimamizi wa Usalama na Afya Kazini. Kuna mifumo huru ya ukaguzi wa kazi nchini Tanzania na Zanzibari. Hata hivyo, mfumo wa ukaguzi unategemea mkoa na hakuna mamlaka kuu ya ukaguzi.

chanzo: § 13 -22 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005; §4-19 ya Sheria ya Usalama na Afya Kazini Nambari 08 ya 2005

Loading...