Social Security

Pension Rights

Sheria ya Hifadhi ya jamii, 1997 inaelezea juu ya pensheni kamili na isiyo kamili. Kwa pensheni kamili, mfanyakazi anapaswa awe amefikia umri wa miaka 60 na walau miezi 180 (miaka 15) ya kuchangia. Pensheni ya awali pia inaweza kutolewa kwa mfanyakazi aliyefikia umri wa miaka 55. Ni programu isiyo timilifu ya bima kamilin na hilipwa kati ya umri wa miaka 55 hadi 59 (kwa wanaume) au 50 hadi 54 (wanawake). Kama mfanyakazi hana vigezo vya kupata pensheni kamili au isiyo kamili, anaweza akapata mafao ya uzeeni. Pensheni kwa mwezi ni 30% ya mshahara wa mfanyakazi aliye katika mfuko wa hifadhi ya jamii kwa miaka yake aliyolipwa vizuri mitano kati ya kumi ikiongezwa na 1.5% ya wastani wa mshahara wake wa mwezi kwa kila miezi 12 ya kipindi chote kinachozidi miaka 15. Malipo ya mkupuo ya mara 24 ya pensheni ya mwezi italipwa kwa mara ya kwanza na baada ya hapo atapata pensheni yake stahiki ya mwezi. Kiwango cha chini cha pensheni ni 80% ya kiwango cha chini cha mashahara cha kisheria.

Katika hali ya kustaafu mapema, pensheni inapunguzwa kwa 0.5% ya mapato yenye bima yanayotumika kuhesabu pensheni kwa kila kipindi cha miezi 12, pensheni inachukuliwa chini ya umri wa miaka 60. Lazima pensheni lazima angalau iwe sawa na pensheni ya chini.

Ridhia ya umri wa uzee inatolewa katika umri wa miaka 60 ikiwa na chini ya mchango wa miezi 180 na ni sawa na wastani wa miezi tisini ya michango kabla ya kustaafu na kuzidishwa na idadi ya miezi ya michango.

Chanzo: §23-27 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997

Dependents' / Survivors' Benefit

Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii, 1997 inatoa fao la wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki wategemezi hawa ni pamoja na mjane/kizuka na watoto chini ya umri wa miaka 18 (umri wa miaka 21, ikiwa ni mwanafunzi, hakuna kikomo cha mlemavu). Ikiwa mfanyakazi anafariki na ametimiza matakwa ya haki kwa umri wa uzee au pensheni batili au alikuwa anaipata tayari, wategemezi wake wanahaki ya ruzuku ya wasaliaji.

Kama hakuna watoto tegemezi, 100% ya pensheni ya marehemu itaenda kwa mjane/mgane wa marehemu.

Pensheni hii italipwa kwa miaka 2 kama mjane/mgane ana umri chini ya miaka 45 au hana mtoto chini ya miaka 15 wakati wa kifo cha mfanyakazi aliye na bima. Endapo kuna watoto tegemezi, mjane/mgane atapewa 40% ya pensheni na 60% itagawanywa kati ya watoto. Pensheni ingawanywa sawia ikiwa kuna zaidi ya mjane/mgani mmoja.

Kama hakuna mjane/mgane, 100% ya pensheni itagawanywa kwa watoto tegemezi (Chini ya miaka 18 au 21 kama bado anahudhuria masomo).Pensheni ya wasaliaji inapatikana milele ay hadi ndoa ya mjane/mgane wa zaidi ya miaka 45. 
Pesa zenye thamani ya mara 24 ya pensheni kwa mwezi zitalipwa kwa mara ya kwanza na baada ya hapo itafuatiwa na pensheni ya mwezi. Kiwango cha chini cha pensheni ni 80% ya Viwango vya chini cha mshahara vya kisheria.  Ridhia ya msaliaji na ridhia ya mazishi pia inalipwa kwa wategemezi.
Na endapo hakuna mgane/mjane, wala watoto tegemezi basi 100% itagawanywa kwa wazazi wa marehemu.

Chanzo: § 33-36 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997

Invalidity Benefit

Sheria ya Hifadhi ya Jamii, 1997 inaelezea kuwepo kwa fao la ulemavu unaopatikana kwa sababu zisizo husiana na kazi ya muathirika.  Mfanyakazi mwenye bima ana haki ya ruzuku isio batili kwa angalau kupoteza kiwango cha mapato cha 66.7% na angalau miezi 180 ya mchango au miezi 36 ya michango, ikiwa ni pamoja na angalau miezi 12 katika miezi 36 baada ya ulemavu kuanza. Uchunguzi wa matibabu unaweza kuhitajika na bodi ya tiba ya madaktari iliyoteuliwa na Wizara ya Afya inakagua ulemavu.

Pensheni ya kila mwezi ni 30% ya wastani mshahara wa mfanyakazi aliye na bima kwa miaka mitano kati ya kumi aliyofanya kazi pamoja na 1% ya wastani wa mshahara wake wa mwezi kwa kila miezi 12 inayozidi miaka 15. Malipo ya mkupuo ya mara 24 ya pensheni yake ya mwezi yatalipwa kwa mara ya kwanza na kufuatiwa na pensheni ya mwezi. Kiwango cha chini cha Pensheni ni 80% ya kima cha chini kisheria cha mshahara. Kitalipwa hadi mfanyakazi atakapotimiza umri wa kupata pensheni (ambapo ataingia kwenye programu ya pensheni ya uzeeni) au kufariki, chochote kitakacho tangulia kutokea.

Ridhia ya ulemavu inalipwa kama mkupuo ikiwa mfanyakazi aliye na bima amekadiriwa na angalau kupoteza 66.7% kiwango cha mapato lakini ana chini ya miezi 180 ya michango.

Chanzo: §28-32 ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997

Regulations on Social Security

  • National Social Security Fund Act, 1997 / Sheria ya Mfuko wa Hifandhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) Mwaka, 1997
loading...
 

 
 
Loading...