Minors and Youth

Minimum Age for Employment

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Kazi, 2004, mtoto chini ya miaka 14 hapaswi kuajiriwa. Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu, ambazo haziwezi kuwa na madhara kwa afya ya mtoto na maendelo yake. Uajiri wa mtoto kamwe usimzuie mtoto kuhudhuria masomo shuleni, kushiriki kwenye ufundi stadi au miradi ya mafunzo yaliodhibitishwa na mamlaka yenye madaraka au uwezo wa mtoto kufaidi maelekezo anayoyapata.

Katiba ya Tanzania inatoa ufikiaji sahihi ili kufikia elimu na kila mwanainchi ako huru kutafuta masomo na uwezo wake na kulingana na uwezo wao.

Chanzo: §5 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Kazi, 2004; §11 ya katiba ya Tanzania

Minimum Age for Hazardous Work

Umri wa chini kwa kazi hatarishi ni miaka 18. Mtu yeyote haruhusiwi kumwajiri mtoto kwenye ajira- (a) ambayo haifai kwa mtu mwenye umri huo; (b) sehemu ambayo inayohatarisha hali nzuri ya mtoto, elimu, afya ya mwili na akili, au roho, maadili au maendeleo ya kijamii. Mtu anaye ajiri mtoto kwenye kazi yeyote inayo ashiria utumikishwaji wa watoto anafanya kosa na atakapo kutwa na hatia, anaweza kupata adhabu isiyo pungua faini ya shilingi laki moja au kifungo cha miezi mitatu au vyote.

Ni kinyume na sheria kwa mtu yeyote kuajiri mtoto katika aina ya kazi hatarishi. Kazi yeyote ambayo inaweza kupelekea adhari za kiafya, usalama au maadili ya mtoto ni hatarishi. 

Kazi hatarishi ni pamoja na Kazi za kwenye vyombo vya majini kama vile meli, migodini, kubeba mizigo (kuli), kazi za viwadani ambako kemikai zina zalishwa au kutumika, kazi zinazotumia mashine, kazi kama vile za vilabu vya pombe (bar), nyumba za wageni (hotels), na sehemu za starehe. Kazi za usiku pia ni marufuku kwa mtoto. 

Chanzo: § 5(3) ya Sheria za Kazi na Ajira, 2004; § 77-86 ya Sheria ya Ajira ya Mtoto ya 2009

Regulations on Minors and Youth

  • Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004 / Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004
  • The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 (amended in 2005) / Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (imefanyiwa marekebisho mwaka 1995)
  • Law of the Child Employment Act, 2009 / Sheria ya Haki za Mtoto, 2009
loading...
 

 
 
Loading...