Forced Labour

Prohibition on Forced and Compulsory Labour

Katiba ya Tanzania inazuia aina zote za kazi za shuruti. Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 pia inzauia aina zote za kazi za dhamana. Hivyo mtu yeyote anaye ajiri, lazimisha au sababisha kazi za shuruti anafanya jinai. Mtu yeyote anaye washurutisha wengine kufanya kazi kinyume cha matakwa yao anafanya makosa. Sheria ya mtoto inakataza kumfanyisha mtoto kazi za shuruti au kazi za dhamana. Mtu yeyote anaye jihusisha na utumikishaji wa watoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto anafanya kosa, na akipatikana na hatia, anaweza kupata adhabu ya kulipa faini ya si chini ya shilingi laki mbili au kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.

Vyanzo: §25(2) ya Katiba ya Tanzania; §6 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004,  §80 ya Sheria ya Mtoto 2009

Freedom to Change Jobs and Right to Quit

Wafanyakazi wana haki ya kubadilisha kazi baada ya kutoa notisi kwa waajiri wao. Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejelea sehemu katika usalama wa ajira.

Chanzo: §41 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini 2004

Inhumane Working Conditions

Wakati wa kufanya kazi unaweza kuongezwa zaidi ya masaa ya kawaida ya kazi ya masaa arobaini na tano kila wiki na masaa tisa kwa siku. Hata hivyo, jumla ya masaa ya kazi ikiwa ni pamoja na saa za ziada usizidi masaa kumi na mbili kwa siku na masaa 50 katika kipindi cha wiki 4 katika hali za dharura.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejelea sehemu ya fidia.

Chanzo: § 19 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano 2004

Regulations on Forced Labour

  • Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004 / Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004
  • The Penal Code, 1945 / Kanuni za adhabu, 1945
  • The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 (amended in 2005) / Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (imefanyiwa marekebisho mwaka 1995)
loading...
 

 
 
Loading...