Compensation

Overtime Compensation

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka wa 2004; mfanyakazi anaweza akahitajika kufanya kazi kwa siku 6 kwa juma. Masaa ya kazi ya kawaida kwa siku na juma ni saa 9  kwa siku na saa 45 kwa wiki isipokuwa kwa wale ambao wanawasimamia wafanyakazi wengine kwa niaba ya mwajiri na ambao wanaripoti moja kwa moja kwa usimamizi mkuu. Huenda wafanyakazi wakahitajika kufanya kazi kwa saa za ziada, kufanya kazi zaidi ya saa za kawaida za kufanya kazi, lakini sio zaidi ya saa 12 kwa siku na saa 50 katika mzunguko wa wiki 4 isipokuwa katika hali ya dharura. Mkataba ulioandikwa utatakiwa kumtaka au kumruhusu mfanyakazi kufanya kazi mpaka saa 12 kwa siku, ikijumuisha kipindi cha kula, bila kupokea malipo ya masaa ya ziada. Makubaliano hayo hayatakiwi kumtaka au kumruhusu mfanyakazi kufanya kazi- (a) kwa zaidi ya siku tano kwa wiki; (b) kwa zaidi ya saa 45 kwa wiki; (c) kwa zaidi ya saa ya ziada 10 kwa wiki.

Mkataba wa pamojo unatakiwa kutoa wastani wa saa za kawaida na saa za ziada za kazi kwa kipindi kilichokubaliwa (kisichozidi mwakaa mmoja) hata hivyo mkataba kama huo hautakiwi kumtaka au kumruhusu mfanyakazi kufanya kazi kwa zaidi ya wastani wa saa 40 za kawaida kwa wiki zikihesabiwa kwa kipindi kilichokubaliwa na saa kumi za ziada kwa wiki zikihesabiwa kw kipindi hicho kilichokubaliwa.

Kikomo cha saa za ziada hakitumiki kwa wafanyakazi wanaowasimamia wafanyakazi wenzao kwa niaba ya mwajiri na ambao wanaripoti moja kwa moja kwa usimamizi wa juu; au kazi ya dharura ambayo haiwezi kufanywa na wafanyakazi wakati wa saa za kawaida za kazi; na au pale ambapo makubaliano ya pamoja yanatoa mwongozo wa kuwa na wastani wa saa za ziada za kazi kwa kipindi kilicho kubaliwa kisichozidi mwaka mmoja, kulinga na kikomo cha wastani cha saa 10 za ziada za kazi kwa wiki.

Ikiwa mfanyakazi anafanya kazi zaidi ya saa zilizowekwa za kufanya kazi, anastahiki malipo ya saa za ziada ambfazo ni saa moja na nusu (1.5 ya X au 150%) ya kiwango cha malipo yake ya kawaida.

Chanzo: Sehemu ya 17-22 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Night Work Compensation

Kulingana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, usiku ni kipindi kati ya 20.00 na 06:00 (ya siku inayofuatia).

Kazi ya usiku hulipwa kwa kiwango cha asilimia 5% juu ya kiwango cha kawaida cha mshahara. Ikiwa kazi ya usiku imefanywa kama kazi ya ziada, saa hizo za ziada hulipwa kwa kiwango cha usiku (ambacho ni asilimia 105% cha kiwango cha kawaida cha siku).

Chanzo: Sehemu ya 20 (4) ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Compensatory Holidays / Rest Days

Sheria haitamki wazi ikimtaka mwajiri kutoa mapumziko ya fidia kwa mfanyakazi aliyefanya kazi siku ya mapumziko ya Juma au Kitaifa. 

Weekend / Public Holiday Work Compensation

Huenda wafanyakazi wakahitajika kufanya kazi katika siku za kupumzika za wiki na siku za mapumziko. Katika hali kama hizo wakati wafanyakazi wanalazimika kufanya kazi siku rasmi za mapumziko, wanastahiki kupokea mishahara kwa kiwango cha asilimia 200% cha kiwango cha kawaida cha mshahara wa kila saa. Wafanyakazi wanaofanya kazi katika siku za kupumzika za kila wiki wanastahili malipo kwa kiwango cha asimila 200% cha kiwango cha kawaida cha mshahara.

Chanzo: Sehemu ya 24 na 25 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004, Sehemu ya 7 ya Agizo la Mishahara 2010

Regulations on Compensation

  • Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004 / Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004
loading...
 

 
 
Loading...