Sick Leave

Income

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano 2004, Kila mfanyakazi aliye pata cheti cha daktari kuwa yu mgonjwa anahaki ya kupata mapumziko yenye malipo (ruzuku ya ugonjwa) kwa kipindi cha siku 126 katika kipindi cha likizo cha miezi 36.

Kwa siku 63 za mwanzo atapata mshahara wake wote na kwa siku nyingine 63 atapata nusu ya mshahara wake.

Chanzo: §32 ya Sheria ya Ajira na Mahusiano 2004

Medical Care

Ruzuku za afya zipo kwa wafanyakazi wenye bima na zinajumuisha huduma ya kuzuia na kuponya, dawa, potholojia ya kliniki na eksirei, upimaji wa maabara, kulazwa hospitalini, upasuaji mdogo na mkubwa. Ruzuku hizi ziko tu kwa huduma za tiba zinazotolewa na madaktari, wauguzi na watoaji wengine wa tiba katika hospitali zilizoidhinishwa.

Chanzo: §42 Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Jamii 1997, §52 Sheria za Ruzuku ya Jamii (Urekebishaji) 2012

Job Security

Kwa mujibu wa sehemu ya 102 ya Sheria ya Afya na Usalama mahali pa kazi 2003, mwajiri haruhusiwi kumwachisha mfanyakazi wakati wa kuugua na magonjwa yanayotokana na kazi. Endapo hawezi kufanya kazi kutokana na sababu za kiafya, mwajiri anaweza kuvunja mkataba muda wowote kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwenye Sheria ya Ulinzi wa Ajira 1964.

Chanzo: §102 ya of Sheria ya Afya na Usalama mahali pa kazi 2003; Sheria ya Ulinzi wa Ajira 1964

Regulations on Sick Leave

  • Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004 / Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004
  • National Social Security Fund Act, 1997 / Sheria ya Mfuko wa Hifandhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) Mwaka, 1997
loading...
 

 
 
Loading...