MKATABA WA HIARI WA HALI BORA ZA WAFANYAKAZI KATI YA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA WAKULIMA WA TUMBAKU KANDA YA MAGHARIBI (WETCU LTD) NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI MASHAMBANI NA KILIMO TANZANIA - (TPAWU)

New2

WESTERN ZONE TOBACCO CROWERS COOPERATIVE UNION LTD (WETCU LTD)

REG No. 5483

TAREHE 1 JULAI, 201 2 - 30 JUNI, 201 5

1.0 UTANGULIZI:

1.1 Chama cha Wafanyakazi Mashambani na Kilimo Tanzania kwa kifupi (TPAWU) na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU LTD) kwa hiari yetu na katika hali ya maelewano tumefikia makubaliano katika masuala muhimu yaliyomo katika Mkataba huu ambayo yanaweka hali bora zaidi za kazi kwa manufaa ya Mfanyakazi na Mwajiri.

2.0 UTAMBUZI:

2.1 Chama cha Wafanyakazi Mashambani na Kilimo, Tanzania TPAWU, kinatambua Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU Ltd) kama ndiye Mwajiri pekee wa Wafanyakazi wa Chama Kikuu.

2.2 Vile vile, Chama Kikuu cha ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU Ltd) wanatambua Chama cha Wafanyakazi Mashambani na kilimo (TPAWU) kuwa ndicho chombo pekee kinachowakilisha wafanyakazi katika hali zote za ajira yao.

2.3 Kwa ujumla kila chombo kimoja kinatambua kuwepo kwa chombo kingine, kwani vyombo hivyo vinakuwepo mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na kwamba wafanyakazi ni kiungo kikubwa cha ushirikiano baina ya vyombo hivyo.

3.0 WAHUSIKA:

3.1 Mkataba huu utawahusu wafanyakazi wote wa kudumu na wa Mkataba wa muda Maalumu wanaowakilishwa na TPAWU isipokuwa Wafanyakazi wa Kigeni.

4.0 KUDUMU KWA MKATABA

4.1 Pande zote mbili tumekubaliana kuwa tarehe ya kuanza kwa mkataba huu ni baada ya pande zote mbili tulipokubaliana na kutia saini mkataba huu. Na utadumu kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu (3).

4.2 Endapo kutakuwa na kubadili kifungu chochote katika mkataba huu, kuondoa au kuongeza kifungu, upande unaohusika utatoa taarifa kwa upande wa pili kwa kufuata sheria ya mahakama ya kazi zilizopo.

4.3 Mkataba huu utaendelea kutambuliwa mpaka utakapokuwa umetayarishwa mkataba mwingine wa kuendeleza au kurekebishwa bila kuathiri muda wa mkataba huu.

5.0 UANACHAMA WA TPAWU:

5.1 Kila mfanyakazi atalazimika kuingia uanachama wa TPAWU.

6.0 KULIPA MICHANCO YA TPAWU:

6.1 Kila mwanachama atalipa michango ya kila mwezi ya TPAWU ambayo ni 2% ya mshahara.

7.0 KIPINDI CHA MAJARIBIO BAADA YA KUAJIRIWA:

7.1Kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi (Staff Regulations) za WETCU Ltd kifungu Na. 5.7 kuwa:-

“Waajiriwa wote chini ya masharfi ya kudumu (yasiyo ya mkataba wa muda maalum au kibaruaj watakuwa kwenye kipindi cha majaribio kwa muda wa mwaka 1. Muda usiozidi miezi sita (6) unaweza ukaongezwa endapo uongozi ufaona kuwa kuna ulazima wa

kufanya hivyo".

8.0 VIWANGO VYA MISHAHARA:

8.1Pande zote mbili zimekubaliana kuwa viwango vya mishahara vitazingatia sheria mbalimbali zilizopo na zitakazotolewa na Serikali kwa kutilia maanani hali halisi ya maisha na uwezo wa mwajiri ili mradi kiwango cha chini cha mshahara hakitakuwa chini ya kile kilichotangazwa na Serikali.

9.0 SIKU NA MUDA WA SAA ZA KAZI:

Kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi za WETCU Ltd kifungu Na. 5.16 kama

(a) Muda rasmi wa kazi utakuwa saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni, kuanzia Jumatatu hadi ljumaa kila wiki isipokuwa siku za sikukuu za kitaifa.

(b) Saa za ziada zinabaki kama zilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi (Staff

Regulations) za WETCU Ltd kifungu Na. 6.19.

(c) Kuwa malipo ya saa za ziada kwa idhini ya Mkuu wa Idara, yatakuwa mara mbili ya kiwango cha kawaida cha malipo ya saa za kazi zilizofanywa katika siku za Jumamosi na Jumapili na siku za Sikukuu.

10.0 KINCA YA AFYA ZA WAFANYAKAZI:

(a) Mwajiri atawajibika kuweka hali bora ya usalama na Afya Bora ya wafanyakazi kwa kuweka mazingira safi na salama.

(b) Mwajiri atatoa mavazi/vifaa vya kinga kwa wafanyakazi kwa kulingana na sehemu na aina ya kazi aifanyayo.

(c) Wafanyakazi watatakiwa kuvivaa na kuvitumia vifaa vyote vya kinga watakavyopewa na mwajiri vinginevyo watahesabika kuwa watovu wa nidhamu.

(d) Wale wote ambao mazingira ya kazi yao wanahitaji kupewa maziwa mwajiri awape maziwa badala ya Fedha wafanyakazi hao ni: Watunza Stoo,Computer operator, Mabwana Shamba, Madereva wanaosafirisha Madawa, watumishi wa masjala na watunza fedha kulingana na ushauri wa kitaalamu.

11.0 HUDUMA ZA MATIBABU:

11.1 Huduma za tiba zitatolewa na mwajiri kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi (Staff Regulations) za WETCU Ltd kifungu Na, 8.1 na 8.2 na nyongeza yake kama ifuatavyo:-

8.0 Mwajiriwa Mke/Mume pamoja na Wategemezi wao watastahiki kupatiwa huduma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kipengele hiki hakijumuishi meno bandia. Miwani itatolewa kwa mfanyakazi atakayekuwa na matatizo ya macho kwa uthibitisho wa

Daktari.

KUONANA NA DAKTARI BINGWA:

8.1 Mwajiriwa atastahiki pale tu ambapo Daktari anayetambulika atakapokuwa ameshauri Mwajiriwa aonane au atibiwe na Daktari Bingwa.

maalum Itigi, Nkinga, Mt. Anna Ipuli n.k. Mwajiri atagharamia

matibabu hayo.

8.4 Endapo mfanyakazi atamjulisha kwa hiari yake mwajiri, na kuleta uthibitisho wa daktari kwamba anaishi na WU. Mwajiri atawajibika

yafuatayo:-

i. Kutomnyanyapaa/Kumbagua.

ii. Taarifa hiyo ibaki kuwa siri ya mwajiri na mwajiriwa.

iii. Ikiwa afya ya mfanyakazi huyo itaonekana kudhoofika, mwajiri ampunguzie kazi au kumubadilisha sehemu ya kazi kulingana na mazingira.

iv. Mwajiriwa mwenye matatizo hayo, asihusishwe kwenye zoezi la upunguzaji kazi, labda akiomba kwa hiari yake mwenyewe.

v. Mwajiri atampatia posho ya lishe isiyopungua Ths. 150,000/= kwa mwezi.

vi. Mwajiri ahakikishe dawa zinatumika ipasavyo.

12.0 POSHO YA NYUMBA NA USAFIRI:

(a) Mwajiri kila inapowezekana atawapatia nyumba za kuishi watumishi wake, na endapo nyumba hazitoshi mwajiri atampa mtumishi posho ya nyumba kulingana na makisio yaliyoidhinishwa na Mrajis.

(b) Watumishi waliopangishiwa au wanaoishi nyumba za Mwajiri hawatalipwa posho ya nyumba, na ukarabati wa nyumba za mwajiri utafanywa na mwajiri mwenyewe.

(c) Watumishi wanaoishi nyumba zao wenyewe na wanastahili kupewa nyumba na mwajiri (Entitled Officers) watalipwa posho ya nyumba kwa viwango vya kulingana na makisio ya kila mwaka yaliyoidhinishwa na Mrajis.

(d) Watumishi wote ambao hawaishi katika nyumba za mwajiri na siyo maafisa wanaostahili kupewa nyumba na mwajiri (Not Entitled Officers) watalipwa posho ya nyumba kwa viwango vya kulingana na makisio ya kila mwaka yaliyoidhinishwa na Mrajis.

(e) Meneja Mkuu, Wakuu wa Idara na Mameneja wa Matawi, pamoja na huduma wanazopewa na Mwajiri, atawalipia pia Ankara za maji na umeme katika nyumba wanazoishi kulingana na makisio yaliyoidhinishwa na Mrajis.

(f) Watumishi wote wanastahili kulipwa posho ya usafiri kulingana na viwango vilivyoidhinishwa, wakiwemo na watumishi wa Matawini.

13.1 Likizo ya mwaka itafuatwa kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi (Staff Regulations) za WETCU Ltd kifungu Na. 9.1 na nyongeza yake kama ifuatavyo:-

9.1 Mwajiriwa anayekwenda likizo atastahiki kusafiri na mkewe/mumewe watoto na wategemezi wasiozidi 4( kwa wanafunzi walioko masomoni wasiozidi miaka 25). Waambatanishe na Vyeti vya uthibitisho.

9.2 Siku za mapumziko (Jumamosi, Jumapili na Sikukuu zinazotambulika) zisihusishwe kwenye siku za likizo.

9.3 Posho ya likizo italipwa Tshs. 20,000/= x mume/mke na

watoto wasiozidi 4 (kwenda na kurudi) wakati wakisafiri kwa mara moja kwa miaka 2.

13.2 Likizo ya uzazi itafuatwa kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi za WETCU Ltd kifungu Na. 9.4 kama ifuatavyo:-

9.4 Likizo ya uzazi yenye malipo itatolewa kwa wafanyakazi wa kike isipokuwa tu wale walioajiriwa kwa masharti ya muda na kutwa. Mwajiriwa atalazimika kuonyesha cheti kutoka kwa Daktari chenye kuthibitisha kwamba anategemea kujifungua.

Wafanyakazi wa kike wanastahili likizo ya uzazi ya siku 90 ambayo inaweza kuchukuliwa kwa wakati mmoja au wakati wowote kati ya mwanzo wa mwezi wa 7 wa ujauzto hadi wakati wa kujifungua, kwa mfanyakazi wa kike anayejifungua mtoto zaidi ya mmoja atastahili likizo ya uzazi siku 100.

Hata hivyo mfanyakazi wa kike wakati akiwa mjamzito anaweza:-

9.4.1 Kwa mapendekezo ya Daktari kwa maandishi anaweza akachukua likizo yake yote ya uzazi yenye malipo au sehemu yake kabla ya mwezi wa saba wa ujauzito.

9.4.2 Likizo ya uzazi haitalimbikizwa kwa njia yoyote ile.

9.4.3 Likizo ya uzazi itatolewa mara moja katika kila baada ya miaka 3 isipokuwa pale mimba inapoharibika au mtoto kufariki kabla ya kutimiza miezi 20, baada ya kujifungua.

9.4.4 Mume ambaye mke wake amejifungua mtoto atapewa likizo, (Paternity Leave) ya siku 7 kwa ajili ya kumuhudumia mkewe na mtoto aliyezaliwa. (Siku hizo zichukuliwe ndani ya siku saba (7) tangu mama ajifungue,

9.4.5 Endapo mwajiriwa akizuiliwa kwenda likizo kutokana na kazi nyingi, mwajiri agharamie nauli kwa familia yake ili iende likizo.

13.3 Likizo ya ugonjwa itafuata kama ilivyofafanuliwa katika Kanuni za kazi za

WETCU Ltd kifungu Na. 9.10 kama ifuatavyo:-

9.10 Kwa mapendekezo ya Daktari anayetambulika, mwajiriwa anaweza akapewa likizo ya ugonjwa.

(i) Mwajiriwa yeyote chini ya masharti ya kudumu, atapokea mshahara wake kamili wa miezi 6 kisha nusu mshahara kwa kipindi cha miezi 6.

(ii) Mwajiriwa yeyote chini ya masharti ya muda atapokea mshahara wake kamili wa mwezi 1 na kisha nusu ya mshahara wake wa mwezi 1 unaofuatia.

13.4 Likizo ya kufiwa:-

Mfanyakazi akifiwa na Mume, Mke, Mtoto, Baba au Mama atapewa likizo ya siku 14 za kupumzika.

14.0 GHARAMA ZA MAZISHI:

14.1 Gharama za mazishi zitatolewa na Mwajiri.

Mfanyakazi akifariki, mwajiri atatoa sanduku/mbao, sanda na usafiri wa maiti hadi eneo la mazishi na atatoa rambirambi ya Tshs. 500,000/= kwa Familia ya marehemu.

14.2 Endapo mfanyakazi atafiwa na mke/mume, baba, mama na mtoto mwajiri atatoa sanduku, mbao, sanda na usafiri wa maiti hadi eneo la mazishi na rambirambi ya Tshs. 500,000/=.

14.3 Pamoja na kulipwa rambi rambi, Mwajiri atailipa familia ya marehemu mishahara ya miezi 6 kwa kiwango cha mshahara alichokuwa analipwa marehemu nje ya mirathi/malipo hayo yatalipwa mfululuzo kila mwezi hadi miezi sita.

14.4 Endapo mfanyakazi wa kudumu na wa Mkataba atafariki, Mwajiri atailipa familia ya marehemu mishahara ya miezi 3 x kipindi chote alichofanyia kazi kisichozidi kumi (10) ndani ya mirathi, ili kuiwezesha familia ya marehemu kujikimu kimaisha (Gharama za masomo kwa watoto wa marehemu, n.k.)

15.0 POSHO ZA SAFARI:

15.1 Posho za safari zitalipwa kama zilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi za WETCU Ltd kifungu Na. 10.1 (i) - (iii) kama ifuatavyo:-

Ngazi za Jumla za Posho (Aina za Posho)

1.1 Aina za posho zifuatazo zitakuwa/zitawahusu watumishi wote bila kujali masharti yao ya kazi.

(i) Posho za kujikimu (Subsistance Allowance) kwa safari za kikazi ndani na nje ya nchi.

(ii) Posho ya kujikimu ya nje (Outfit Allowance).

Vifungu hivyo vitafuata kanuni za Utumishi za WETCU Ltd kifungu 10:1-4

16.0 KUACHA NA KUACHISHWA KAZI:

16.1Kuacha kazi kwa mtumishi au mwajiri kumuachisha kazi mtumishi kwa sababu za kufaa; zitafuata Sheria, Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini.

17.0 TIJA/UFANISI/MAFUNZO:

17.1 Pande zote mbili zinakubaliana kuweka mipango ya kazi iliyo mizuri na kutoa elimu kwa wafanyakazi wa ngazi zote ili kuinua hali yetu ya kiuchumi na jinsi walivyo na jukumu kubwa katika kuweka Taifa letu hai na imara kiuchumi.

17.2 Mwajiri kwa kuzingatia umuhimu wa elimu ya wafanyakazi atagharamia mafunzo ya muda mrefu na mfupi yatolewayo ndani na nje ya nchi yenye lengo la kuendeleza taaluma ya wafanyakazi.

17.3 Endapo mfanyakazi ataenda masomoni, Mwajiri ataingia Mkataba na mfanyakazi huyo ili baada ya masomo arejee kufanya kazi. Endapo mwajiriwa hatapenda kuendeleza mkataba wa Ajira atawajibika kumlipa mwajiri gharama zote za masomo.

18.0 TUZO KWA MFANYAKAZI BORA/HODARI:

18.1Mfanyakazi bora/hodari atakayeteuliwa kwa ushirikiano wa pande mbili TPAWU na Mwajiri atatunzwa fedha taslimu zisizopungua Tshs. 300,000/= (laki tatu tu) au kitu chochote chenye thamani isiopungua Tshs. 300,000/= au zaidi kulingana na hali ya uchumi ya mwajiri.

18.2Endapo Mfanyakazi atachaguliwa kuwa mfanyakazi bora Kitaifa Mwajiri atamzawadia fedha zisizopungua Tshs. 1,000,000/= (milioni moja) au kitu chochote chenye thamani hiyo.

19.0 SHERIA/KANUNI/TARATIBU ZA KAZI:

19.1 Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi lazima ziheshimiwe na zitumike na pande zote zinazohusika na mkataba huu.

20.0 FIDIA YA AJALI KAZINI:

20.1 Mfanyakazi atakaeumia kazini atalipwa kwa mujibu wa sheria ya fidia

21.0 MKOPO WA MUDA MFUPI NA MREFU.

21.1Mikopo ya fedha na vyombo/vifaa vya ujenzi vitatolewa kwa watumishi kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi za WETCU Ltd vifungu Na. 6.12, 6.13 na 6.14 kama ifuatavyo:-

6.12 Meneja Mkuu anayo mamlaka ya kumkopesha mfanyakazi kiasi cha fedha kisichozidi jumuisho la mishahara ya miezi 3. Ambao utakatwa kwenye mshahara wake.

6.13(a) Mikopo ya dharura kwa ajili ya ununuzi wa samani, ukarabati

kwa wafanyakazi waliopotelewa na mali zao, utatolewa kwa idhini ya Meneja Mkuu. Kiasi kitakachokopeshwa hakitazidi jumuisho la mishahara ya miezi mitatu ya mkopaji. Mkopo kwa ajili ya ununuzi wa gari utaidhinishwa na Bodi.

(b) Meneja Mkuu anayo mamlaka ya kumkopesha mtumishi anaeanza Ajira kiasi cha fedha cha kutosha mshahara wake usiozidi mwezi mmoja.

(c) Meneja Mkuu anaweza kutoa mkopo pale ambapo anaona Mwajiriwa atautumia mkopo huo katika kulipia masomo yake ambayo yataweza kuinua kiwango cha ufanisi kazini. Kwa mfano; Waajiriwa wanaochukua kozi za CPA, ATEC n.k.

Njia ya kurejesha mikopo;

6.14(a) Mkopo wa mshahara kwa ajili ya kununulia vitu mbalimbali

utarejeshwa kwa njia ya makato sita yaliyosawa. Wakati ambapo mkopo uliotolewa wakati wa kuanza ajira au uliotolewa kwa ajili ya kulipia masomo utarejeshwa kwa njia ya makato tisa yaliyo sawa, ila tu pale ambapo Meneja Mkuu atakuwa ameelekeza vinginevyo.

(b) Mkopo kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli, utarejeshwa katika kipindi cha miezi 12 ununuzi wa jokofu na jiko la umeme/gesi katika kipindi cha miezi 24. Ununuzi wa vifaa vya ujenzi katika kipindi cha miezi 36.

(c) Mkopo kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki na magari utarejeshwa katika kipindi cha miezi 36.

22.1Mfanyakazi anaweza kustaafu kwa hiari anapotimiza umri wa miaka 55 na atalazimika kustaafu anapotimiza umri wa miaka 60.

22.2Mfanyakazi anaweza kustaafu kwa sababu za kiafya baada ya kuthibitishwa na daktari wa Hospitali ya Serikali au Hospitali inayotambulika kuwa hali yake haimruhusu tena kuendelea na kazi, au Bodi ya Madaktari.

22.3Mfanyakazi anayestaafu kwa umri wa kustaafu au kwa sababu ya kiafya ama kuisha kwa mkataba atagharimiwa usafiri wa kwenda kwao yeye, mke/mume, watoto na wategemezi wake wanaotambulika kisheria pamoja na mizigo yake. Kama ilivyofafanuliwa katika kanuni za kazi (Staff Regulations) za WETCU Ltd kifungu 18.3.

VIWANGO VYA USAFIRI NDANI YA NCHI NA UPENDELEO KATIKA

KUSAFIRI. (Kanuni za kazi za WETCU Ltd kifungu 18:3)

DARAJA LA KAZI DARAJA LA KUSAFIRIA KIASI CHA MIZIGO LIKIZO
Reli, Barabara, Maziwa, Huduma za Boti Pwani Ajira ya kwanza, Uhamisho,

Kusimamishwa Ajira, Kufukuzwa, Kustaafu.

Waajiriwa wenye kiwango cha mshahara cha WETCU 5 na zaidi DARAJA LA KWANZA Kg. 3,500 Kg 200
Waajiriwa wenye kiwango cha mshahara cha WETCU 2-4 na zaidi DARAJA LA PILI Kgs. 2,000

Kgs 100

(i) Upendeleo uliotolewa hapo juu utatolewa tu pale ambapo mwajiriwa anasafiri katika mazingira ambayo yanakubalika chini ya kifungu cha mazingira ambapo usafiri utatolewa hapo juu.

Kusafiri kwa daraja lililotajwa hapo juu kutategemea upatikanaji wa nafasi katika daraja hilo, hivyo dai lolote juu ya tofauti za nauli pale ambapo mhusika atakuwa amesafiri kwa daraja la chini kuliko lile analostahili, halitakubaliwa. Familia ya mhusika itasafiri katika daraja analostahiki kusafiria mhusika lakini pale ambapo kiwango cha mizigo kitazidi kile kilichoidhinishwa mhusika hatalipiwa gharama zozote za ziada kufidia gharama za mizigo iliyozidi.

zote, Mwajiri aendelee kumlipa mstaafu huyo posho ya kujikimu

inayolingana na mshahara wake pamoja na kumlipa posho ya nyumba, gharama za matibabu na gharama zilizopo kwenye kifungu Na. 14.0.

22.5 Mfanyakazi aliyeajiriwa kwenye Masharti ya Mkataba ambao unastahiki malipo ya bakshishi anapomaliza Mkataba wake, kwa mafanikio atastahili kulipwa malipo hayo ya bakshishi kwa kiwango cha asilimia 40 ya majumuisho ya mishahara yake yote ya kila mwezi kwa muda ajibfanya kazi. Malipo hayo yatalipwa pindi amalizapo Mkataba bila kujali kama atapewa fursa ya kuendeleza Mkataba mwingine.

22.6 Endapo mwajiriwa na mwajiri hawataendeleza mkataba mwajiri atamzawadia Mwajiriwa Bandari 2 za Bati na Cementi mifuko 30. Hapa ni kwa wafanyakazi wa mkataba kuanzia miaka 2 na kuendelea.

22.7 Mtumishi wa Mkataba kama atapenda kuendeleza Mkataba wake atatakiwa atoe taarifa ya nia yake hiyo miezi minne kabla ya kukamilisha muda wa Mkataba wake wa ajira aliyonayo. Na mwajiri atamjibu kabla ya mkataba wake kuisha.

22.8 Mtumishi atakayestaafu kwa mujibu wa sheria au kiafya atapewa marupurupu yafuatayo:-

(i) Mshahara wa mwisho anaopokea x miezi sita kila mwaka x miaka isiyozidi 20 kutegemea muda aliofanya kazi.

(ii) Mifuko ya sementi Mia (100) na bandali tano (5) za bati

23. UPUNGUZAJI WA WAFANYAKAZI:

23.1 Pande zote nnbili tumekubaliana kuwa hatua za kutatua migogoro ya kikazi kati ya Mwajiri na Wafanyakazi, tutazingatia Sheria zilizopo.

23.2 Tumekubaliana kuwa upunguzaji huu utafanyika tu baada ya Uongozi wa WETCU Ltd kushauriana na Uongozi wa Tawi la TPAWU, Ofisi ya Eneo TPAWU na baada ya kufikiria njia mbali mbali na kukubaliana na hali hiyo ikiwa pamoja na kuwahamisha wafanyakazi wenye ujuzi kutoka Idara moja kwenda nyingine.

23.3 Mwajiri aliarifu Tawi la TPAWU nia yake ya kupunguza watumishi, sababu na aonyeshe bayana Idadi ya watumishi anaotaka kupunguza, idadi kamili anayotaka wabaki kazini kabla ya kuanza zoezi la kupunguza.

23.4 Endapo mtumishi ataomba kupunguzwa kwa hiari yake mwajiri amruhusu.

(a) Juhudi ya kazi

(b) Uwezo wa kufanya kazi

(c) Muda wa kuwepo kazini/kuajiriwa

(d) Umri wa kukaribia kustaafu

(e) Masuala ya kifamilia

(f) Wale wote wanaopunguzwa kazi wawe wa kwanza kurejeshwa kazini endapo hali ya mwajiri itarejea kuwa nzuri ki-uchumi.

(g) Ikiwa njia zote zitashindikana katika zoezi la kupunguza kwa kuangalia kifungu

23.5 (a) - (e) hapo juu utaratibu wa "FILO" utafuatwa.

23.6 Zoezi la kupunguza halitawahusu Mwenyekiti, Katibu wa Tawi la TPAWU na kamati yake Endapo mazingira yatalazimisha kuwahusisha, Mwajiri atashauriana na Ofisi ya Eneo TPAWU pamoja na Afisa Kazi. Kabia ya kutekeleza zoezi la kupunguza viongozi wa Tawi la TPAWU.

23.7 Viongozi wengine ambao hawatahuska na zoezi la kupunguzwa ni Meneja Mkuu na Wakuu wa Idara, lakini hakuna pingamizi kwa yeyote kati ya waliotajwa akiomba kupunguzwa kwa hiari.

23.8 Wanaopunguzwa watagharamiwa usafiri wa kwenda kwao yeye Mke/Mume na watoto wake na wategemezi ambao anaoishi nao pia ofisi inawatambua na vyombo vyake kulingana na kifungu namba 22.3 hapo juu.

24.0 MIGOGORO KAZINI:

24.1 Pande zote mbili tumekubaliana kuwa hatua za kutatua migogoro ya kikazi kati ya Mwajiri na Wafanyakazi uzingatie Sheria za nchi zilizopo.

24.2 Mkataba huu hautarajiwi kufuta au kwenda kinyume na Sheria za nchi zilizopo.

24.3 Pale ambapo kifungu chochote katika Mkataba huu kitakuwa kinyume na Kanuni za Utumishi/Kazi za WETCU Ltd kifungu cha Mkataba huu

Kiheshimiwe.

25.0 HITIMISHO:

Mkataba huu umetiwa sahihi leo tarehe

Kwa niaba ya:- WETCU LTD

MWENYEKITI WA WETCU LTD

MJUMBE WA BODI YA WETCU LTD

Kwa niaba ya:- TPAWU

MWENYEKITI WA TAWI - TPAWU

KATIBU WA TAWI - TPAWU

KATIBU WA SEHEMU - TPAWU

TZA Western Zone Tobacco Growers Cooperative Union LTD (WETCU LTD) - 2012

Start date: → 2012-07-01
End date: → 2015-06-30
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → 2012-07-01
Name industry: → Agriculture, forestry, fishing
Name industry: → Growing of crops, market gardening, horticulture
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Names associations: → Western Zone Tobacco Growers Cooperative Union LTD (WETCU LTD)
Names trade unions: →  TPAWU

TRAINING

Training programmes: → Yes
Apprenticeships: → No
Employer contributes to training fund for employees: → No

SICKNESS AND DISABILITY

Maximum for sickness pay (for 6 months): → 100 %
Maximum days for paid sickness leave: → 365 days
Provisions regarding return to work after long-term illness, e.g. cancer treatment: → 
Paid menstruation leave: → No
Pay in case of disability due to work accident: → Yes

HEALTH AND SAFETY AND MEDICAL ASSISTANCE

Medical assistance agreed: → Yes
Medical assistance for relatives agreed: → Yes
Contribution to health insurance agreed: → Yes
Health insurance for relatives agreed: → No
Health and safety policy agreed: → Yes
Health and safety training agreed: → No
Protective clothing provided: → 
Regular or yearly medical checkup or visits provided by the employer: → Yes
Monitoring of musculoskeletal solicitation of workstations, professional risks and/or relationship between work and health: → 
Funeral assistance: → No

WORK AND FAMILY ARRANGEMENTS

Maternity paid leave: → 13 weeks
Maternity paid leave restricted to 100 % of basic wage
Job security after maternity leave: → No
Prohibition of discrimination related to maternity: → No
Prohibition to oblige pregnant or breastfeeding workers to perform dangerous or unhealthy work: → 
Workplace risk assessment on the safety and health of pregnant or nursing women: → 
Availability of alternatives to dangerous or unhealthy work for pregnant or breastfeeding workers: → 
Time off for prenatal medical examinations: → 
Prohibition of screening for pregnancy before regularising non-standard workers: → 
Prohibition of screening for pregnancy before promotion: → 
Facilities for nursing mothers: → No
Employer-provided childcare facilities: → No
Employer-subsidized childcare facilities: → No
Monetary tuition/subsidy for children's education: → No
Paternity paid leave: → 7 days

WORKING HOURS, SCHEDULES AND HOLIDAYS

Working hours per day: → 8.0
Working days per week: → 5.0
Paid annual leave: → 28.0 days
Paid annual leave: → 4.0 weeks
Rest period of at least one day per week agreed: → Yes
Maximum number of Sundays / bank holidays that can be worked in a year: → 
Provisions on flexible work arrangements: → 

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Provision that minimum wages set by the government have to be respected: → Yes
Adjustment for rising costs of living: → 

Once only extra payment

Once only extra payment: → TZS  %
Once only extra payment due to company performance: → Yes

Extra payment for annual leave

Extra payment for annual leave: → TZS 20000.0

Premium for overtime work

Premium for overtime work: → 200 % of basic wage

Premium for Sunday work

Premium for Sunday work: → 100 %

Allowance for commuting work

Meal vouchers

Meal allowances provided: → No
Free legal assistance: → 
Loading...