MKATABA WA HALI BORA KATI YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA MASHAMBANI NA KILIMO TANZANIA (TPAWU) NA AFRICAN PLANTATIONS KILIMANJARO LIMITED (APKL)

New2

MKATABA WA HALI BORA KATI YA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA MASHAMBANI NA KILIMO TANZANIA (TPAWU) NA AFRICAN PLANTATIONS KILIMANJARO LIMITED (APKL)

I. UTANGULIZI:

Sisi chama cha wafanyakazi wa mashambani (TPAWU) tukiwa kama wawakilishi wa wafanyakazi tukijulikana kama "UNION" kwa upande mmoja, na African Plantation Kilimanjaro Limited (APKL) akijulikana kama "MWAJIRI" kwa upande mwingine, hapa kwa pamoja tunathibitisha kwa maandishi na kuweka sahihi zetu, kwa kunuia wenyewe na kwa hiari yetu, kwamba tumekubaliana kuhusu yafuatayo Yahusuyo maslahi bora zaidi ya ajira kwa wafanyakazi wote walioajiriwa.

2. UTAMBUZI:

2.1 Mwajiri anaitambua TPAWU kama sauti pekee na chombo chakufanya majadiliano yahusuyo haki za wafanyakazi wote walioajiriwa na APKL kuhusu mambo yote yahusuyo hali bora zaidi za uajiriwa na marupurupu mengine alimradi "UNION" inawakilisha zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya waajiriwa wote katika vikao vya majadiliano.

APKL na TPAWU wanakubaliana kuhakikisha kuwa wanachama wao wote wanalindwa na sheria na hakutakuwepo na vitisho vya aina yoyote.

2.3 Kuwezesha maofisa wa TPAWU au wawakilishi wao kuwasiliana na wanachama wa TPAWU waliopo mashambani bila kikwazo, APKL inakubali kuwa viongozi watawaruhusu maofisa wa TPAWU au wawakilishi kutembelea mashamba yake ili mradi ujio huo na malengo yake yamewekwa bayana na kutaarifiwa APKL kabla.

2.4 TPAWU inatambua haki ya kipekee aliyonayo mwajiri ambaye ni mwanachama wa chama cha waajiri ya kusitisha ajira ya mwajiriwa yoyote aliyeajiriwa naye kwa njia za kisheria au kwa makubaliano yaliyopo.

2.5 APKL na TPAWU kwa pamoja wanatambua lengo la kuhakikisha na kuendeleza ufanisi wa hali ya juu katika utendaji kazi katika idara zote husika.

a) Kufikia na kudumisha viwango vya juu vya utendaji kazi kwa idara zote za kampuni

b) Kuhakikisha viwango vya juu zaidi vya utendaji kazi na uzalishaji kulingana na taratibu za uchumi endelevu na kushirikiana kutimiza malengo hayo.

Uitishwaji mkutano katika mashamba:

2.6.1 TPAWU itakuwa na wajibu wa kuhakikisha inapata ruhusa na vibali vya kuitisha mikutano ya wanachama mashambani kabla.

2.6.2 Isipokuwa kwa hali ihusiayo dharura, na kwa vikao vihusuvyo chaguzi za viongozi wa matawi, ambavyo uongozi wa APKL utatoa ruhusa, endapo mwajiri atakuwa ametaarifiwa kabla na makubaliano yakawepo, au pale ambapo sheria imeruhusu vinginevyo, mikutano itaitishwa wakati wa saa za kazi. 

2.6.3 Kukubalika na kuzingatiwa kwa makubaliano:

APKL na TPAWU, kwa pamoja wanatambua faida zitokanazo na makubaliano haya na mengine yanayoweza kufikiwa wakati wowote na pande zote mbili, kupitia chombo cha majadiliano ya pamoja. Na hivyo kwa pamoja wanaamua kuwa makubaliano haya yatakuwa yanachapishwa na kusambazwa kwa wahusika wote. APKL imekubali itatoa ofisi ndogo kwa ajili ya shughuli za chama (tawi) kwa kazi za chama na vikao na vikao vya nidhamu.

3. WATAKAO FAIDIKA:

Makubaliano haya ya pamoja yatawahusu wafanyakazi wote walioajiriwa na APKL isipokuwa wale wenye mkataba maalumu ya umeneja, uhasibu, utawala, maeksipati na wasio raia wa Tanzania.

4. TAREHE MKATABA KUANZA KUFANYA KAZI NA KIPINDI UTAKAPODUMU:

4.1 Mkataba huu utaanza kufanya kazi rasmi kuanzia tarehe 01 Januari, 2015 na utadumu kwa muda miezi 24 na baada ya hapo kufanyiwa marekibisho.

4.2 APKL itathamini vikao kwa namna ambavyo kampuni inaweza.

4.3 APKL na TPAWU inakubaliana kuunda kamati ya nidhamu ya pamoja yenye wanakamati 18.

4.4 Bila ya kuathiri kifungu Na. 4.1 hapo juu mkataba huu utaendelea kufanya kazi hadi utakaporekebishwa na mkataba mwingine.

5. UANACHAMAWATPAWU:

Tumekubaliana kuwa uanachama ni jambo la hiari na kwamba ni suala kati ya mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu na TPAWU. Mfanyakazi atajiunga na TPAWU na kuwa mwanachama kwa kujaza fomu namba 6.

6. ADA/MICHANGO YA TPAWU NA UWASILISHWAJI WAKE:

6.1 Imekubaliwa kwamba kampuni itakata ada za TPAWU asilimia mbili (2%) ya mshahara kwa wanachama wa TPAWU kama ada ya mwezi. Imekubaliwa kuwa kampuni itawezesha ukataji huo wa 2% kutoka kwa wanachama na kuwasilisha ofisi ya TPAWU kanda kila mwezi kwa kuandika hundi.

6.2 Wajiriwa ambao si mwanachama wa TPAWU ambao watafaidika na mkataba huu watachangia ada sawa na wanachama wa TPAWU kama ilivyoanishwa na Sheria ya Mahusiano ya kazi Na. 6 ya mwaka 2004.

7. WASAA YA KAZI:

7.1 Imekubaliwa kuwa waajiriwa wote watapaswa kufanya kazi masaa arobaini na tano (45) kwa wiki. Siku za kawaida ni masaa nane (8) mfululizo, na jumamosi ni masaa matano (5).

7.2 Saa za kuanza kazi ni kuanzia 1.30 asubuhi na mapumziko ya chai saa 4.00 mpaka saa 4.15 asubuhi na mlo wa mchana saa 6.00 - 6. 45 mchana na kurudi kazini mpaka saa 10.00 jioni na jumamosi kuanzia saa 1.30 asubuhi mpaka saa 6.30 mchana.

7.3 Saa za ziada (overtime) italipwa kwa watakaofanya kazi zaidi ya masaa 8 ya kazi kwa makubaliano kama ilivyo katika sheria za kazi, na italipwa mara moja na nusu (1.5) ya saa ya kawaida.

7.4 Siku za mapumziko na sikukuu zitalipwa mara mbili (2) ya viwango vya malipo ya kawaida na Masaa ya ziada (overtime) italipwa mara mbili (2) ya malipo ya viwango vya kawaida.

7.5 Kampuni itamlipa mfanyakazi asilimia tano (5%) zaidi ya kiwango cha mshahara wake kwa kila saa alilofanya kazi usiku. Na kama ni overtime itaongezeka kwa asilimia tano. Masaa ya usiku m kati ya saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

7.6 Mwajiri atawapatia wafanyakazi chai ya rangi wakati wa saa za kazi na wafanyakazi watawajibika kujitafutia kitafunio.

7.7 Mwajiri atatoa usafiri endapo mfanyakazi atapangwa kazi shamba lingine na muda wa kuanza kazi utachukuliwa kuanzia pale safari ilipoanza.

7.8 Wafanyakazi watasaini kitabu cha mahudhurio (kwenye kitabu au kifaa cha eletroniki) anapoingia na kutoka kazini.

8. AJIRA/MUDA WA MAJARIBIO:

8.1 Wafanyakazi wataajiriwa na kupewa mikataba kulingana na aina ya kazi na sheria za kazi. Mkataba uanaweza kuwa wa kudumu, wa muda maalum, au kwa kipimo cha kazi.

8.2 Wafanyakazi wote wa kazi za kitaalam, walioajiriwa kwa mkataba wa kudumu, watakuwa kipindi cha majaribio cha miezi sita (6). Uthibitisho wa kumwajiri mhusika moja kwa moja utatolewa kimaandishi kwa aliyemaliza kipindi cha majaribio vyema.

8.3 Kipindi cha majaribio kwa wafanyakazi wasiohitaji taaluma maalum kitakuwa ni miezi mitatu (3), na baada ya hapo barua ya uthibitisho kazini itatolewa.

8.4 Kipindi cha majaribio kinaweza kuongezwa na uongozi akionekana inafaa/hitajika, na hakitakuwa zaidi ya miezi mitatu (3), hili litatokea pale ambapo uongozi utakuwa umeona mfanyakazi hakufanya vizuri wakati wa kipindi cha majaribio. Sababu za mwendelezo huo ni lazima zitolewe kwa mfanyakazi husika.

8.5 Kipindi cha majaribio kinaweza kusitishwa na upande wowote wakati wowote kama mwajiriwa ameona kazi husika haimridhishi au mwajiri akiona mhusika hafai kuwa mwajiriwa wa wakudumu.

8.6 Wakati wowote wa kipindi cha majaribio, mwajiri au mwajiriwa anaweza toa taarifa ya kusitisha ajira kulingana na sheria za kazi zinavyo elekeza.

9. LIKIZOYAUZAZI:

9.1 Mfanyakazi wa kudumu wa kike, atakayekuwa mjazito, atapewa punguzo la kipimo cha kazi, kuanzia mimba itakapokuwa na umri wa miezi sita (6) na kulingana na ushauri wa daktari.

9.2 Mfanyakazi mjamzito atakapokuwa anahudhuria kliniki iliyoidhinishwa, atakuwa analipwa siku 

yake kana kwamba yupo kazini. Taarifa itolewe kwa meneja wa shamba kuhusu siku za kliniki

9.1 Mfanyakazi mjamzito mwajiriwa wa kudumu, akipata tatizo la ujauzito wake kabla hajafikisha miezi sita (6); kazi atakazopewa ziendane na ushauri au ripoti ya daktari.

9.2Mfanyakazi wa kudumu wa kike atakuwa na haki ya kupata likizo ya uzazi ya siku tisini (90) kwa kujifungua mtoto mmoja na siku mia moja (100), kama atakuwaamejifungua zaidi ya mtoto mmoja. Likizo ya uzazi ni mara moja kila baada ya miaka 3.

9.3 Mwanamke mjamzito atatoa taarifa kwa mwajiri mwezi mmoja (1) kabla kwamba anakusudia kuanza likizo ya uzazi ili ofisi iweze kuandaa malipo husika. Baada ya likizo mwanamke huyo ataruhusiwa likizo nyingine ya uzazi baada ya miaka mitatu (3) kwa mujibu wa sheria. Baba wa mtoto (mwanamume) ambaye mkewe amejifungua atapewa likizo ya siku nne (4) kumsaidia mkewe kwa mujibu wa sheria.

9.4 Ikitokea mtoto kufariki katika kipindi cha likizo, likizo ya uzazi itasitishwa na mfanyakazi atachukua likizo yake ya kawaida ya mwaka. Mfanyakazi huyo anaweza tena kupata likizo ya uzazi hata kama atapata mimba kabla ya miaka mitatu (3) kwisha.

9.5 Muda wa unyonyeshaji mtoto kwa mfanyakazi wa kike aliye mzazi utakuwa ni masaa mawili (2) kwa kila siku ya kazi ya kawaida, na saa moja (1) kwa siku ya Jumamosi. Kipindi hicho kitadumu kwa mwaka mmoja (1).

10. KUSITISHWA AJIRA:

10.1 Pande zote mbili zinakubalina kuwa, hakuna mfanyakazi atakayeachishwa kazi bila sababu.

10.2 Kama ikihitajika kumwachisha kazi mwaajiriwa, basi sheria husika zitafuatwa kikamilifu.

10.3 Hakuna mfanyakazi atakayeachishwa kazi kutokana na sababu zifiatazo:-

a) Kwa kuwa ni mwanachama, au mwanakamati wa chama cha wafanyakazi au kuchaguliwa uongozi katika ngazi ya juu ya chama au kushughulikia masuala ya kiofisi ya chama.

b) Kwa kuwa ni mwanachama wa chama chochote cha siasa ndani ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania.

c) Kwa ajili ya rangi yake au dini yake, au kwa sababu ya mgogoro wa kidini ambao hausababishi utendaji wa kazi kuathirika, au kwasababu za kikabila.

10.4 Uachishwaji kazi kutokana na sababu za kiafya utazingatia sheria zilizopo.

11. LIKIZO YA MWAKA:

11.1 Mfanyakazi wa kudumu atakuwa anapata likizo ya siku thelathini (30) kila mwaka. Pia atapewa posho ya likizo ya shilling elfu thelathini (30,000/=) kila mwaka. Meneja atabandika orodha ya likizo kwenye mbao za matangazo za kampuni.

11.2 Likizo yoyote stahili ambayo haijachukuliwa kwa wakati, na ikitokea mfanyakazi husika ameachishwa kazi, basi likizo hiyo italipwa kikamilifu. 

11.3 Mfanyakazi ataruhusiwa kuchukua hadi siku nne (4) kwa mwaka kama likizo yenye malipo kwa kufiwa na mwana familia wa karibu kama vile baba, mama, mke, mume, dada wa kuzaliwa, kaka wa kuzaliwa au mtoto wa kumzaa.

11.4 Mfanyakazi mwanaume ambaye mke wake atakuwa amejifungua mtoto ataruhusiwa kuchukua likizo ya siku nne (4) ndani ya siku saba (7) za kujifungua mkewe. Likizo hii ni kwa mara moja katika kipindi cha miaka 3.

12. HUDUMAZATIBA:

12.1 Kampuni itatoa matibabu kwa wafanyakazi wa kudumu kwa hadi kiwango cha shilingi Elfu Sabini na Tano (Shs 75,000/=) kwa mwaka. Mfanyakazi atatakiwa kuchukua sick sheet kwa kuhudhuria matibabu.

12.2 Mwajiri atahakikisha kuwa wafanyakazi wote wa kudumu wamesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) au mfuko mwingine ili wafanyakazi wapate matibabu bure toka fao la matibabu la NSSF.

12.3 Wafanyakazi watakaokuwa wanafanyakazi katika idara nyeti, watakuwa wanachekiwa afya zao kama sheria za usalama na afya kazini ya mwaka 2003 inavyosema.

12.4 Kampuni itatoa huduma ya matibabu ya dharura kwa wafanyakazi watakaougua au kuumia wakiwa kazini.

13. UKIZO YA UGONJWA:

Mfanyakazi wa kudumu atakuwa na haki ya likizo yenye malipo kamili kwa ajili ya ugonjwa/kuugua, ya siku 63 na likizo yenye malipo nusu ya mshahara ya siku 63. Malipo haya yatawahusu wanaohudhuria hospitalini na kwa ushauri wa daktari.

14. MISHAHARA NA MARUPURUPU:

14.1 Kima cha chini cha mshahara kitakuwa shillingi Laki Moja Kumi na Saba Elfu (Tsh. 117,000/=) kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 17%, Kima hiki kitaanza kulipwa tarehe 1 Januari 2015.

Kutokana na utaratibu wa kulipa mshahara kupitia benki, Kampuni itachangia shillingi elfu tatu (Tshs. 3,000/=) kwa mwezi kama gharama ya usafiri.

Kwa wale wanaolipwa zaidi yaTsh. 117,000/= kwa mwezi watapata nyongeza ya asilimia 10% au zaidi kuendana ufanisi wa kazi wa mfanyakazi husika.

Endapo serikali itatangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisheria wakati mkataba huu unaendetea, APKL na TPAWU tutakaa na kujadili upya ongezeko la mshahara Mata vyokuwa kwa pamoja.

Kampuni itaangalia uwezekano wa kuwa na sera ambayo itawezesha kuongeza mshahara kwa wafanyakazi wenye bidii na utendaji mzuri kazini kwa kufuata pia miaka kazini.

APKL na TPAWU watakaa na kujadili ongezeko la mshahara kila mwaka.

14.7 Pale ambapo itawezekana kampuni itatoa mkopo kwa ajili ya kununulia baiskeli kwa

wafanyakazi wa kudumu Ili kurahisisha usafiri wa kuendea kazini. Pia kampuni itasaidia kwa kutoa mikopo ya ada za shule pale itakapowezekana.

15. KUSTAAFU:

15.1 Muda wa kawaida wa kustaafu utakuwa miaka 60, mfanyakazi anaweza kuamua kwa hiari kustaafu katika umri wa miaka 55.

15.2 Kampuni inaweza andeleza ajira ya mstaafu kwa makubaliano naye.

15.3 Aliyetimiza umri wa kustaafu kazi anaweza kuendelea na mkataba kama anakubali na mwajiri kuendelea.

15.4 Notisi (Taarifa) ya miezi sita (6) kabla inapaswa kutolewa kimaandishi na mwajiri/mwajiriwa anayehitaji kustaafu.

15.5 Malipo ya kustaafu yatakuwa na bakshishi kama ilivyo kifungu cha 16.

16. MALIPO YA UTUMISHI WA MUDA MREFU:

Imekubaliwa kwamba mwajiri atatoa bakshishi (bonasi) ya utumishi wa muda mrefu kwa mfanyakazi anayestaafu kama ifuatavyo:-

• Aliyefanya kazi miaka 10 Tsh. 172,500/=

• Aliyefanya kazi miaka hadi 15 Tsh. 258,750/=

• Aliyefanya kazi miaka 20 ni Tsh. 345,000/=

• Aliyefanya kazi hadi miaka 25 na zaidi ni Tsh. 431,250/=

Tanabihi (NB): Malipo haya yatakuwa yanabadilika kulingana na kushuka thamani ya fedha (inflation rate) ia na nana basi 

Mawasiliano/mazungumzo ya pande mbili yatazingatia pamoja na mambo mengine hatua mbadala, vigezo vya kuwapata wafanyakazi watakao punguzwa. Mambo ya kuzingatiwa wakati wa upunguzaji wa wafanyakazi pamoja na mengineyo pamoja na:-

. Ubora . Utendaji kazi . Taaluma

. Miaka aliyotumikia kampuni . Umri

. Hali ya kifamilia.

Kwa mujibu wa sheria za kazi viongozi wa TPAWU tawi watakuwa wa mwisho kupunguzwa kazi kama ikilazimu, na mawasiliano na uongozi wa TPAWU sehemu au kanda yatafanywa kuhusu hilo.

18. MALIPO YA UPUNGUZWAJI KAZI.

Malipo ya upunguzwaji kazi yatakuwa kama ifuatavyo:-

a) Kama yalivyoainishwa katika sheria za kazi

b) Asilimia 5 ya mshahara wa mhusika x miezi 12 mara miaka aliyofanya kazi.

19. MOTISHA:

19.1 Tumekubaliana na pande zote mbili kuwa, kwa ajili ya kuhamasisha mahudhurio kazini utendaji kazi mzuri na kufanya wafanyakazi waione kampuni ni yao na kujituma zaidi na utii kwa kampuni.

29.2 Kampuni itaweka utaratibu wa kuwezesha kupatikana kwa wafanyakazi bora ambao watakuwa wanapewa vyeti wakati wa sikukuu za mei mosi kila mwaka. Idadi yao itaweza kufika hadi watu kumi na wawili (12) na sio chini ya wane (4)kwa mwaka na watachaguliwa na menejimenti ya kampuni kwa kushirikiana na kamati yaTPAWU ya tawi .

19.3 Zawadi kwa wafanyakazi bora wa kawaida kiidara/sehemu itakuwa shillingi Laki moja na Hamsini Elfu (Tshs. 150,000/=) kwa kila mfanyakazi.

23.4 APKL imekubali kuwachagua wafanyakazi wane (4) bora zaidi watawawakilisha wengine katika sherehe za mei mosi mkoa na zawadi yao itakuwa shilling Laki Mbili (200,000/=) kila mmoja.

21. USALAMA KATIKA KAMPUNI NA MAENEO YA KAZI:

Tumekubaliana kuwa usalama katika kampuni ni jambo la umuhimu mkubwa na ni lazima liwe

miongoni mwa sera za kampuni ili kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na kampuni, maeneo ya makazi, wageni na mazingira kwa ujumla, 

Tumekubaliana kuwa kampuni itaendeleza sera ya kuhakikisha inatoa mafunzo ya kazi na uendelezaji wafanyakazi. Hili litasaidia kuongeza stadi za kiufundi na utendaji bora zaidi na uzalishaji zaidi.

22. POSHO YA KUJIKIMU SAFARINI NA WAKATI WA VIKAO:

Kampuni itatoa posho ya kujikimu kwa mfanyakazi atakayekuwa katika safari ya kikazi nje ya kampuni kama ifuatavyo:-

Jiji, Manispaa na Makao makuu ya mkoa 40,000/= (Elfu Arobaini)
Makao makuu ya wilaya 30,000/= (Elfu Thalathini)
Vijiji 20,000/= (Elfu Ishirini)
Posho ya safarini 10,000/= (Elfu Kumi)

Wakati wa vikao muhimu kati ya kampuni na TPAWU, kampuni itakuwa inagharamia chai/chakula na posho ya shilling elfu tano (Tshs. 5,000/=). Vikao hivi havitarajiwi kuzidi vine (4) kwa mwaka.

23. SARE ZA KAZI/VIFAA VYA KUJIKINGA:

23.1Kampuni itatoa kila mwaka pea moja au mbili za nguo za kazi kulingana na idara, sare ya kazi na vifaa vya kujikinga vinavyoendana na aina ya kazi kwa wafanyakazi wa kudumu.

23.2Mfanyakazi atalazimika kutumia sare na vifaa vya kujikinga kama atakavyoelekezwa na mwajiri. Endapo mfanyakazi atakiuka matumizi ya vifaa kinga hatua za kinidhamu zitachukuliwa.

23.3Mfanyakazi atawajibika kutunza kifaa cha kujikinga na mavazi aliyopewa na mwajiri. Uharibifu na upotevu utalipwa na mfanyakazi.

23.4Mwajiri atatoa mche mmoja wa sabuni kila miezi miwili kwa waliopewa mavazi ili kutunza usafi wake wa mavazi hayo.

24. VIFO NA MAZISHI:

24.1 Pande zote mbili zimekubaliana kwamba ikitokea mfanyakazi amefariki akiwa kazini, au nje ya eneo la kazi au akiwa likizo madhali bado ni mfanyakazi, na awe amemaliza mwaka mmoja (1) au zaidi kazini kampuni itagharamia gharama za sanda na sanduku.

24.2 Mwajiri atatoa Tsh. 300,000/= (laki tatu) kama rambirambi ya kifo kwa familia ya waliofiwa/marehemu.

24.3 Mwajiri atatoa Tsh. 200,000/= (laki mbili) kama rambirambi kwa mfanyakazi atakayefiwa na mtoto au mke/mume. Mfanyakazi atapewa likizo ya siku nne (4) kuhudhuria mazishi.

24.4Kampuni itagharamia kusafirisha maiti ya mfanyakazi aliyefariki hadi sehemu ya mazishi pale itakapowezekana.

25. MGOGORO KAZINI:

Migogoro yote ya kikazi kati ya mwajiri na mwajiriwa itatatuliwa kulingana na sheria za kazi. Hata hivyo migogoro na tofauti ambazo hazikuanishwa katika makubaliano haya itabidi kwanza yashughulikiwe na TPAWU ngazi ya tawi na meneja wa sehemu husika kwa lengo la kufikia muafaka na kurudisha mahusiano mema. Kama hakuna makubaliano basi suala hilo lipelekwe ngazi ya juu inayofuata na kama hakuna maafikiano suala hilo litatuliwe kulingana na taratibu na sheria za kazi husika.

26. SHERIA ZA KAZI:

Tumekubaliana kuwa, hakuna kipengele chochote katika mkataba huu ambacho kina lengo la kupingana na sheria za kazi kumhusu mwajiri, chama au mfanyakazi. Ikibainika hivyo, basi kipengele hicho kitafutwa na marekebisho yafanywe katika mkataba vipengele viendane na sheria zilizopo.

27. MIKUTANO:

APKL imekubali kufanya mkutano na wafanyakazi mara mbili (2) kwa mwaka kuendana na sheria.

Mbele ya mashahidi pande zote mbili zinaweka sahihi na mihuri kama inavyoonyesha hapa chini leo tarehe 22 Desemba 2014.

Kwa niaba ya kampuni:

Jina la Kampuni: Afican Plantations Kilimanjaro Limited

Jina la mhusika

cheo

Sahihi

Jina la mhusika

Cheo

Sahihi

Jina la mhusika

Cheo

Sahihi

TZA African Plantations Kilimanjaro Limited (APKL) - 2014

Start date: → 2014-12-22
End date: → Not specified
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → 2014-12-22
Name industry: → Agriculture, forestry, fishing
Name industry: → Growing of crops, market gardening, horticulture
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Name company: →  African Plantations Kilimanjaro Limited (APKL)
Names trade unions: →  TPAWU

SICKNESS AND DISABILITY

Maximum for sickness pay (for 6 months): → 53 %
Maximum days for paid sickness leave: → 126 days
Provisions regarding return to work after long-term illness, e.g. cancer treatment: → 
Paid menstruation leave: → No
Pay in case of disability due to work accident: → Yes

HEALTH AND SAFETY AND MEDICAL ASSISTANCE

Medical assistance agreed: → Yes
Medical assistance for relatives agreed: → No
Contribution to health insurance agreed: → Yes
Health insurance for relatives agreed: → No
Health and safety policy agreed: → Yes
Health and safety training agreed: → Yes
Protective clothing provided: → 
Regular or yearly medical checkup or visits provided by the employer: → No
Monitoring of musculoskeletal solicitation of workstations, professional risks and/or relationship between work and health: → 
Funeral assistance: → Yes

WORK AND FAMILY ARRANGEMENTS

Maternity paid leave: → 13 weeks
Maternity paid leave restricted to 100 % of basic wage
Job security after maternity leave: → No
Prohibition of discrimination related to maternity: → No
Prohibition to oblige pregnant or breastfeeding workers to perform dangerous or unhealthy work: → No
Workplace risk assessment on the safety and health of pregnant or nursing women: → No
Availability of alternatives to dangerous or unhealthy work for pregnant or breastfeeding workers: → No
Time off for prenatal medical examinations: → Yes
Prohibition of screening for pregnancy before regularising non-standard workers: → No
Prohibition of screening for pregnancy before promotion: → No
Facilities for nursing mothers: → Yes
Employer-provided childcare facilities: → No
Employer-subsidized childcare facilities: → No
Monetary tuition/subsidy for children's education: → No

EMPLOYMENT CONTRACTS

Part-time workers excluded from any provision: → 
Provisions about temporary workers: → 
Apprentices excluded from any provision: → 
Minijobs/student jobs excluded from any provision: → 

WORKING HOURS, SCHEDULES AND HOLIDAYS

Working hours per day: → 8.0
Working hours per week: → 45.0
Working days per week: → 6.0
Paid annual leave: → 30.0 days
Paid annual leave: → 4.0 weeks
Maximum number of Sundays / bank holidays that can be worked in a year: → 
Provisions on flexible work arrangements: → 

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Provision that minimum wages set by the government have to be respected: → No
Agreed lowest wage per: → Months
Lowest wage: → TZS 117000.0
Adjustment for rising costs of living: → 

Wage increase

Once only extra payment

Once only extra payment: → TZS 150000.0 %
Once only extra payment due to company performance: → Yes

Premium for evening or night work

Premium for evening or night work: → 105 % of basic wage
Premium for night work only: → Yes

Extra payment for annual leave

Extra payment for annual leave: → TZS 30000.0

Premium for overtime work

Premium for overtime work: → 150 % of basic wage

Premium for Sunday work

Premium for Sunday work: → 100 %

Allowance for commuting work

Allowance for commuting work: → TZS 3000.0 per month

Allowance for seniority

Allowance for seniority: → TZS 172500.0 per month
Allowance for seniority after: → 10 years of service

Meal vouchers

Meal allowances provided: → No
Free legal assistance: → 
Loading...