Likizo ya Uzazi

Ubaba, uzazi, likizo, sheria, ugonjwa, huruma, kila mwaka, mfanyikazi, mwajiri, mkataba, mtoto, ujauzito, kujifungua, kuzaa, sera, NSSF, fedha, faida, bima, michango, daktari, malipo, taifa Mywage Tanzania

Kando na Likizo ya Kila Mwaka, kuna aina nyingine za likizo ninazostahili?

Zaidi ya Likizo ya Kila Mwaka unastahili Likizo ya Uzazi/Ubaba, Likizo ya Ugonjwa na Likizo ya Huruma. Kuna aina za likizo zinazotolewa chini ya sheria. Hata hivyo, Mkataba wa Pamoja au sera ya kindani inaweza kutoa aina zaidi za likizo.

 Ninawezaje kustahiki Likizo ya Uzazi/Ubaba?

Likizo ya Ubaba iko chini ya Sehemu Ndogo ya D ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2014. Mfanyikazi hustahiki Likizo ya Uzazi/Ubaba baada ya kukamilisha miezi sita ya kufanya kazi kuanzia kuanzishwa kwa mkataba wake wa ajira. Kigezo kingine cha kustahiki Likizo ya Uzazi ni hitaji la sheria kwa mfanyikazi kutoa taarifa iliyoandikwa kwa mwajiri lenye lengo lake la kuchukua Likizo ya Uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe inayotarajiwa ya kujifungua. Taarifa hiyo lazima iwe na cheti cha matibabu.

Unastahiki Likizo ya Uzazi baada ya kukamilisha kazi ya miezi sita kuanzia tarehe ya kuanza ajira yako.

Je, mwajiri anaweza kukataa kunipa Likizo ya Uzazi kwa kushindwa kutoa taarifa kama inavyohitajika?

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 imeweka hii kama kigezo tu cha mtu kuweza kupata Likizo ya Uzazi. Haijasema chochote kuhusu kitakachofanyika ukikosa kutoa taarifa inayohitajika. Kwa hivyo inashauriwa mfanyikazi kutoa taarifa ya miezi mitatu kwa sababu mwajiri anaweza kukataa kukupa Likizo unayolipwa ya Uzazi kwa sababu ya kukosa kwako kufuata utaratibu uliowekwa

Je, ninastahili siku ngapi za Likizo ya Uzazi?

Katika Mzunguko wa Likizo (kipindi cha miezi 36) utastahiki siku 84 za Likizo unayolipwa ya Uzazi ikiwa utajifungua mtoto mmoja au siku 100 za Likizo unayolipwa ya Uzazi ikiwa utajifungua zaidi ya mtoto mmoja. Siku hizi zinajumuisha siku za mapumziko na Sikukuu za Umma. Hata hivyo kwa sababu ya matatizo yoyote yale ya kujifungua/kuzaa uwe unahitaji siku za ziada unaweza kujadiliana na mwajiri kuhusu uwezekano wa kutumia siku za Likizo ya Ugonjwa, au siku kadhaa kutoka kwa Likizo yako ya Kila Mwaka, au upate siku za ziada za likizo usiyolipwa.

Je, kuna hali yoyote chini ya sheria ambayo ikitokea itaniruhusu nipate siku 84 za ziada za Likizo ninayolipwa ya Uzazi katika mzunguko wa likizo?

Ndiyo. Ukijifungua na mtoto afe ndani ya mwaka mmoja wa kuzaliwa utastahiki siku 84 za ziada za Likizo unayolipwa ya Uzazi.  

Je, kuna kikomo cha mara ambazo ninaweza kuchukua Likizo ya Uzazi?

Kulingana na sheria zinazosimamia sekta binafsi mfanyikazi anaweza kuwa na hadi mihula minne ya Likizo ya Uzazi katika muda wake wa ajira akiwa na mwajiri mmoja.

Katika tukio kwamba nimemaliza mihula yangu minne ya Likizo ya Uzazi na niwe mjamzito bado ninaweza kuomba Likizo nyingine ninayolipwa ya Uzazi?

La. Huwezi kunyimwa Likizo yako ya Uzazi, lakini hutalipwa.

Je, ni lini ninaweza kuanza Likizo yangu ya Uzazi?

Mfanyikazi anaweza kuanza Likizo yake ya Uzazi wakati wowote kuanzia wiki nne kabla ya tarehe inayotarajiwa ya kujifungua au tarehe ya mapema kama itadhibitishwa na Daktari kuwa ni muhimu kwa afya ya mama au mtoto ambaye hajazaliwa.

Je, ninaweza kusimamishwa kazi nikiwa mjamzito au baada ya kurejea kazini kwangu kutoka kwa Likizo yangu ya Uzazi?

Ndiyo, unaweza kusimamishwa ajira yako ukiwa mjamzito au ukirejea kutoka Likizo ya Uzazi lakini sababu haistahili kuhusishwa na ujauzito wako au kujifungua. Mwajiri anaweza kukusimamisha kwa sababu nyingine kama vile utovu wa nidhamu au kutofanya kazi vizuri, lakini baada ya kufuata taratibu zilizowekwa.

Je, kuna malipo yoyote chini ya sheria ambayo ninastahiki kutoka kwa mwajiri wangu wakati wa Likizo ya Uzazi?

Mwajiri kulingana na sheria anahitajika kumpa mfanyikazi aliye katika Likizo ya Uzazi mshahara wake wa kawaida ambao mfanyikazi hupata kama angeenda kazini. Hata hivyo, ikiwa faida za ziada zimetolewa chini ya sera za kindani za shirika/kampuni basi mwajiri hana budi ili kulipa.

Je, kuhusu kulazwa hospitalini? Je, mwajiri wangu anawajibika kwa bili yangu ya hospitali inayohusishwa na ujauzito au kujifungua?

Sheria inasema kwamba mwajiri atakuwa na jukumu la kushughulikia bili za matibabu za mfanyikazi wake ikiwa mfanyikazi anaishi katika majengo ya mwajiri au imejadiliwa na imewekwa katika Mkataba wa Pamoja, au ikiwa mwajiri ana sera ya kindani ambayo inatoa huduma za kimatibabu kwa wafanyikazi.

Je, ni taasisi nyingine gani ambayo inaweza kushughulikia Faida zangu za Uzazi?

Baadhi ya hifadhi ya pensheni kama vile Mipango ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii huwa na bidhaa kuhusu Faida za Uzazi. Faida za Uzazi zina sehemu mbili, Huduma ya Matibabu ya Uzazi na Faida ya Fedha za Uzazi. Mwanamke aliyejisajili na NSSF anaweza kupokea hizi, bora afikie masharti yafuatayo:

  • Katika kipindi kati ya kujisajili mara ya kwanza na hifadhi na wiki inayotarajiwa ya kujifungua, awe amelipa michango 36.
  • Katika miezi 36 zinazotangulia wiki inayotarajiwa ya kujifungua, awe amelipa michango 12.

Ikiwa masharti haya mawili yametimizwa, mwanamke huyo atahitimu faida zote. Kama sharti lolote halijatimizwa, hatahitimu faida yoyote.

Loading...